Picha: Kinana aitikisa Mbeya mjini

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
Kwa wale wakazi wa Mbeya Mnakumbuka Huu uwanja ulikuwa unaitwa uwanja wa Slaa kutokana na Mkutano wake wa 2010,lakini Leo Mwanaume amebadili jina unaitwa Uwanja wa Kinana,Mbeya Mjini hapa Rwanda Nzovwe amevunja Rekodi

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo jioni kwenye viwanja vya Ruanda Nzovwe, Mjini Mbeya leo jioni.

Maelfu ya wananchi wakaiwa wamefurika kwenye viwanja vya Ruanda Nzove kwenye mkutano huo

SOTE NI CCM: Wananchi wakimpungia mikono Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akilipiwahutubia maelfu ya wananchi katika mkutano huo

Nape akisisitiza jambo kwenye mkutano huo

'Tanzania, Tanzaniaaaa Nakupenda kwa moyo woteee…." Nape akiimba pamoja na wananchi wimbo huo wa kuamsha ari ya uzalendo katika baada ya kuwahutubia maelfu ya watu kwenye mkutano huo.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge Mteule Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano huo

Bryson Mwasimba aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, akitoa ya moyoni alipopewa fursa ya kusalimia wanancjhi kwenye mkutano huo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi wenzake wakiwa kwenye
meza kuu wakati wa mkutano huo. Meza kuu hiyo ilikuwa tofauti kabisa na
zile zlizozoeleka ambazo huwa na mapambo mengi huku zikiwa na sehemu
ya kukinga jua. Utaratibu wa majukwa na meza kuu vya aina hii ndiyo
mtindo wa sasa katika mikutano ya CCM. Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk. Norman Sigala, Kattibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya

Katibu Mkuu wa CCM, na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwapungua mikono wananchi walipokuwa wakipita barabarani wakienda kwenye mkutano huo

SISI NI VIJANA WA CCM: Vijana waliokuwa kwenye mkutano huo wakipiga picha kwa simu zao ili kupata kumbukumbu.

Mbona sura ni zile zile mikutano yote?! au wafuasi ndo wanafuata mikutano kila wilaya?
 
wamekuwa wakitangaza ,mambo huko wakiwa huko wakiahidi ahadi zingine lipi amelitekeleza???? hamuwezi tudanganya watanzania mpaka sasa jamani mbona hamsikiii?????
 
watanzania wanapenda matukio... hata aje mkitikila watajikusana tu.... tusubiri kipindi cha uchaguzi tujue mbivu nambichi
 
watanzania wanapenda matukio... hata aje mkitikila watajikusana tu.... tusubiri kipindi cha uchaguzi tujue mbivu nambichi

Upo sawa kabisa,Watanzania kwa kuwa wengi hawana kazi hivyo hawakosi kujaa kwenye matukio.Uwingi wa watu sio ishara ya kukubalika.Hii sio kwa CCM tu bali kwa Chadema pia.

Ila naamini wananchi wa Mbeya hawatarudia kosa la kuweka mbunge wa level Sugu,naamini ata Mbeya ina watu makini wa kuweza kuwa Wabunge Makini.
 
Safi sana nimefurahi kuwaona wanambea tena ni watu wenye afya vijana na wanaonekana wasomi safi sana tunataka matukio ya ukweli kama haya tupambane kwa hoja na sio vioja, viva ccm.
 
Walikuwa wanahutubia kuhusiana na nini?, au ili mradi tu wamesomba watu kwa malori?
 
Wanambea siwalaumu kwa kumchagua sugu ila nawakubali ni wanamabadiliko walimpa waone ni nini atafanya sasa wameona kila kukicha afadhali ya jana watampa mwingine tena safi wanambea mko juuuuu.
 
Safi sana nimefurahi kuwaona wanambea tena ni watu wenye afya vijana na wanaonekana wasomi safi sana tunataka matukio ya ukweli kama haya tupambane kwa hoja na sio vioja, viva ccm.
Mkuu, mimi nakushauri tu, hupendezi kushabikia CCM, hao CCM wameshaonyesha wazi kuwa hawana uchungu na nchi yetu,
Wanaingia mikataba ya kilaghai, wanaachia madini yetu yanasombwa, wanajilipa mamishahara makubwa ili hali mama zetu wanajifungulia sakafuni, hata vitanda tu hakuna mahospitalini, wewe kwa nini uwashabikie?

Hilo lisomali linakashfa ya kubeba meno ya tembo wetu kwenye meli zake na kutoroshea ughaibuni, CCM tuwamwage mkuu, sio watu wazuri.
 
Upo sawa kabisa,Watanzania kwa kuwa wengi hawana kazi hivyo hawakosi kujaa kwenye matukio.Uwingi wa watu sio ishara ya kukubalika.Hii sio kwa CCM tu bali kwa Chadema pia.

Ila naamini wananchi wa Mbeya hawatarudia kosa la kuweka mbunge wa level Sugu,naamini ata Mbeya ina watu makini wa kuweza kuwa Wabunge Makini.

Nani, jangili Kinana!! Huyu mwenye meli kabisa za kubebea meno ya tembo! Huyu huyu?
 
Nilikuwepo kwenye huu mkutano akina nape kama wana akili nadhani wamegundua ugumu wa mbeya kwa upande wa ccm, make hata watu kuitikia ccm hoyee! wanaona aibu, kuna tofauti kubwa kati ya shamra za mikutano ya chadema na hii ya ccm, mwenye akili hahitaji maneno mengi waka kushawishiana nadhani kila kitu kilikuwa wazi
 
Taswira acha kudanganya umma,watu walisombwa kwa ujira wa tsh 30,000/- kama unabisha tembelea maeneo ya kabwe,mwanjelwa walikosombwa vijana wengi kaulize utapata majibu na baada ya kutoka huko walilewa sana na kuanza kuimba nyimbo za Chadema,Chadema,Chadema peoples power!!!!! Wengi wakisema tunakula CCM tunalala Chadema.. Hao wanawake wawili mwishoni wanaopiga picha mmoja ni changudoa maarufu hapa mjini anamiliki grocery inaitwa vumilia naye ni mmoja wa waliosombwa kupelekwa mkutanoni kwa ujira wa 30,000/-
 
Nilikuwepo kwenye huu mkutano akina nape kama wana akili nadhani wamegundua ugumu wa mbeya kwa upande wa ccm, make hata watu kuitikia ccm hoyee! wanaona aibu, kuna tofauti kubwa kati ya shamra za mikutano ya chadema na hii ya ccm, mwenye akili hahitaji maneno mengi waka kushawishiana nadhani kila kitu kilikuwa wazi

Mkuu hata mimi nilikuwepo,wengi waliohudhuria ni wale walioletwa kwa malipo. Mbeya hakunaga CCM!
 
@Nape anaipenda sana chadema mpaka ameamua kushona gwanda la magamba?... Viva CDM
 
mikoa ya mbeya,arusha,kilimanjaro,mwanza
kigoma,mara walishaamka siku nyingi
hawawezi kudanganyika, hapo wamekuja kuchukua kanga kofia na pesa
kura zao chadema..
wananchi hawataki mikutanao washawachoka wamekuja kujua kama kuna kipya
msidhani wingi huo wanawasupport na wizi wenu wa pembe za ndovu ufisadi na mikataba feki.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom