PICHA: KILIO cha MIAKA 50 ya UHURU Barabara LAMI RUKWA... Makandarasi WENGI ni WAKICHINA - Angalia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
KILIO CHA MIAKA 50 YA UHURU NA BARABARA MKOANI RUKWA CHAELEKEA UKINGONI, LAMI YAENDELEA KUTANDAZWA KWA KASI




Hali ilivyo hivi sasa ya barabara ya Tunduma Sumbawanga. Na ujenzi bado unaendelea. Taarifa juu ya ujenzi wa barabara kuu inapatikana hapo chini.


Wakandarasi wakiendelea na ujenzi


TAARIFA FUPI YA MIRADI MIKUBWA YA BARABARA ZINAZOENDELEA KUJENGWA MKOANI RUKWA NA KATAVI

1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – LAELA (95.31KM)

Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Aarsleff-BAM International Joint Venture V.O.F Kutoka Denmark na Uholanzi kwa gharama ya dola za Kimarekani 97 Milioni chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 49.9% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri na ulipangwa kwisha 31 Januari 2013 ingawa majadiliano kuhusu kuongeza muda wa kumaliza kazi bado yanaendelea.

2. SEHEMU YA LAELA – IKANA (64.2KM)
Sehemu hii inajengwa na Kampuni ya China New Era International Engineering Corporation kutoka China kwa gharama ya Sh. bilioni 76.1 chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa na unategemea kukamilika 31 Mei 2013.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi 31 Octoba, 2012 yalikuwa yamefikia 64% ya kazi zote zilizopangwa. Kwa ujumla mradi unaendelea vizuri.

3. SEHEMU YA IKANA – TUNDUMA (63.7KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Consolidated Contractors Group S. A (Offshore) (CCC) kutoka Ugiriki chini ya Mhandisi Mshauri Egis BCEOM International kutoka Ufarasa kwa gharama ya Sh. bilioni 82.5. Maendeleo ya jumla ya mradi hadi sasa yamefikia 43% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 9 Septemba 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi uliongezwa hadi tarehe 31 May 2013.

2. SUMBAWANGA – NAMANYERE – MPANDA NA KIZI – KIBAONI (245KM)

2.1. SEHEMU YA SUMBAWANGA – KANAZI (75KM)

Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O'Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufikia tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 23.6% ya kazi zote zilizopangwa. Kasi ya maendeleo ya kazi inasuasua kwa madai kuwa mkandarasi hajalipwa kiasi chote anachodai. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012, hata hivyo muda wa kumaliza kazi bado unajadiliwa.

2.2. SEHEMU YA KANAZI – KIZI – KIBAONI (76.6KM)

Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya China Hunan Construction Engineering Group Corporation kutoka China, chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O'Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania, kwa gharama ya Sh. 82.84 bilioni.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 30% ya kazi zote zilizopangwa. Mkandarasi anaendelea na kazi ingawa kwa kasi ndogo kwa madai ya kuchelewa kulipwa. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 15 Desemba, 2012, lakini haitawezekana. Hivyo muda wa kumaliza bado unajadiliwa.

3. SUMBAWANGA – MATAI – KASANGA PORT (112KM)

Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company Ltd. chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O'Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd, kutoka Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh. 133.30 bilioni.

Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufika tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 28% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and Build Contract). Kwa sasa kazi zinaendelea vizuri baada ya kusuasua siku za nyuma. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 13 Januari, 2013 lakini itabidi muda wa utekelezaji kuongezeka kutokana sababu mbalimbali.




Kwa lugha isiyo rasmi tunasema "Mkeka"


Kazi bado inaendelea



Posted by Hamza Temba at 4:52 AM
 
Rukwa ruka, our slogan enzi zile mkoa unaanzishwa mwaka 1974 ulivomegwa kutokea Tabora
 

Hii PICHA ya MWISHO HICHO KIDARAJA ni cha WATOTO au kwa MAGARI MAKUBWA???

HAWA WATU WANAJUA KULA PESA zetu na Ni WACHINA HAWA...

Hicho ni kidaraja cha kupishana gari moja moja. Kwa nini wasipanue tangu mwanzo?
 
Hongera serikali lakini hii siyo efforts za kujivunia! Ni wajibu wa serikali
 
Wachina Sumbawanga 2 Kasanga Port wamepumzka mpaka Next year.Hawa watu wanaomaliza Ud,udom,n.k.why wasipewe hata ka contracts?Wiz mtupu.Cku zao zinaesabika
 
Nchi inayoshindwa kuwadhamini wahandisi wake wakapata mkopo ili waweze kuanzisha kampuni za ujenzi wa barabara. Wafute kodi kwenye uingizaji wa magari ya ujenzi yanayoingizwa na wahandisi wazawa ili kufacilitate wazawa waweze kuanzisha kampuni. Mbona wanaosimamia ni wabongo kwani hao wachina wanafanya nini?
 
wabongo wapewe tenda hizo si watafia bar, na wengine mtawakuwa wamenatana na wake za watu. chezea mbongo apate hela mbuzi tu balaa
 

Hii PICHA ya MWISHO HICHO KIDARAJA ni cha WATOTO au kwa MAGARI MAKUBWA???

HAWA WATU WANAJUA KULA PESA zetu na Ni WACHINA HAWA...
Tukisema tutaambiwa tunabeza, lakini nimeangalia hiyo barabara na nimeona si ya kiwango kuwa barabara inayojengwa wakati huu wa sasa. Kwa macho yangu barabara hii ni nyembamba mno, kitu ambacho kitachangia katika kuleta ajali nyingi. Ingefaa wajenge barabara pana ambapo magari yataweza kupishana vizuri.
 
aISEE BARABARA HIYI NIMEPITA NIKIWA STD 3 1984 IKIWA VUMBI HAHAHAHA. HOPE ONE DAY NTAPITA TENA HUKO KWA WATANI ZANGU WAFIPA. POSUTAAAAAAA! NSWA WAPO HUKO PANDE ZA KATANDALA? NSWA=KUMBIKUMBI
 
Tukisema tutaambiwa tunabeza, lakini nimeangalia hiyo barabara na nimeona si ya kiwango kuwa barabara inayojengwa wakati huu wa sasa. Kwa macho yangu barabara hii ni nyembamba mno, kitu ambacho kitachangia katika kuleta ajali nyingi. Ingefaa wajenge barabara pana ambapo magari yataweza kupishana vizuri.

Kwanini Waifyatulie PICHA? MPIGA PICHA AMECHOKA? au ndio MOJA ya UZEMBE wetu... Hatuko SERIoUS kwenye KAZI la TAIFA LETU???
 

Hii PICHA ya MWISHO HICHO KIDARAJA ni cha WATOTO au kwa MAGARI MAKUBWA???

HAWA WATU WANAJUA KULA PESA zetu na Ni WACHINA HAWA...

Haya madaraja yapo kadhaa katika njia hii na hayajajengwa na Mchina, yamejengwa na Tanroads pamoja na hiyo lami yake.
 
Jamani hii barabara ni highway kweli mbona muonekano wake ni kama barabara iliyo chini ya kiwango au ni macho yangu tu. Manake ukifananisha na hawa wenzao wanatengeneza kutoka Iringa mjini kuja mafinga naona kuna touti kubwa sana !!!
 
Tatizo ya hizo box culvert (madaraja) nyingi ni nyembamba, hazikutakiwa zitunike kwenye njia mpya. TANROAD walitaka hizo culverts zibaki kama zilivyo (ku-save cost na kusababisha hajari).

Pia Barabara hizo zinajengwa ziki target urunium.
 
aISEE BARABARA HIYI NIMEPITA NIKIWA STD 3 1984 IKIWA VUMBI HAHAHAHA. HOPE ONE DAY NTAPITA TENA HUKO KWA WATANI ZANGU WAFIPA. POSUTAAAAAAA! NSWA WAPO HUKO PANDE ZA KATANDALA? NSWA=KUMBIKUMBI
karibu ule Nswa dogo ndo kipindi chake hiki.
 

Attachments

  • MTOKO.jpg
    MTOKO.jpg
    30.8 KB · Views: 50
Mkuu mleta uzi

Hapa vipi ni double road!?

" (95.31KM)
Sehemu hii inajegwa na Kampuni ya
Aarsleff-BAM International Joint Venture
V.O.F Kutoka Denmark na Uholanzi kwa
gharama ya ($USD)za Kimarekani 97 Milioni"
 
Apo namwamini uyo Mdenimark JV hao wachina sina imani nao kabisaaa
wanaweza toa kitu substandard
wazungu wanajenga 95km kwa 150billion wakati mchina anajenga 64km kwa 76billion ebu angalia ratio izo wakati barabara ni iyo iyo ila wamepewa kila mtu kipande chake
Wazungu husema cheap things are expensive yataja kutukuta haya
 
Sumbawanga - Namanyere - Mpanda nimepita three months ago mbona hamna kazi yoyote inayoendelea? hiyo na hapo inaonyesha kazi itaisha mwakani au wataleta ready made barabara?
 
Bado Serikali haijaheshimu wajibu wake wakuheshimu mkataba,hii ni chanzo cha kuchelewesha mipango mbalimbalimbali ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom