PICHA: KILI STARS ILIPOKWAA KISIKI LEO NAMBOOLE, ni HUZUNI TUPU ni YALEYALE HADI HANS POPPE

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Wachezaji wa Bara wakijadiliana baada ya kufungwa na Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge usiku wa leo kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. Uganda walishinda 3-0 na kutinga fainali, ambako watamenyana na Kenya Jumamosi.

SURA ZA HUZUNI; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia akifuatilia mchezo kati ya Bara na Uganda. Kushoto wake ni Waandishi wa Habari wa Tanzania, Somoe Ng'itu juu na Zaituni Kibwana pembe ni kabisa Z.H.

Mwinyi Kazimoto akiwa amezibiwa njia kwa staili hadi ya kulala kama unavyoona hapo

Cheki ulinzi huo langoni mwa Uganda, Ngassa na Bocco peke yao wangefanya nini

Amri Kiemba anakokota ngoma

John Bocco akiwa amezibiwa njia

John Bocco leo aliwekewa ulinzi mkali, kama unavyona hapa

Mrisho Ngassa akidhibitiwa na beki wa Uganda

Mwinyi Kazimoto akijaribu kufumua shuti mbele ya beki wa Uganda

Kipa kadaka, Ngassa na Bocco leo hoi

Kocha wa Stars, Kim Poulsen baada ya mechi

Kapteni Kaseja haamini macho yake

Emmanuel Okwi akifuatilia mchezo benchi baada ya kuumia na kutoka

Bocco mawindoni, lakini ulinzi wa kutosha ulimynima mabao leo
 
Ugonjwa WETU ni ULE ULE... Kichwa cha MWENDAWAZIMU!!
 
Ugonjwa WETU ni ULE ULE... Kichwa cha MWENDAWAZIMU!!

Vikombe kadhaa tumevichukua Tanzania ikiwamo kombe la Kagame, unataka tufurahi sisi tu wakati kila nchi inatuma timu iliyoaminika? Ni zamu yao kushinda, wachezaji wetu warudi kujipanga upya.
 
Mimi ningekuwa kocha au TFF ningetumia common sense ndogo tu.....kuwatumia kwenye Kili Stars asilimia kubwa ya wachezaji waliobeba kombe la Kagame!
Simple, siyo?
 
Afadhali wamefungwa, make walishaanza kutengeneza taswira za kwenda kuuza sura bungeni na vi-dreads fyao.
 
Ndiyo faida ya kuchagua wachezaji toka timu moja na wengine ni wa benchi tu.
 
Vikombe kadhaa tumevichukua Tanzania ikiwamo kombe la Kagame, unataka tufurahi sisi tu wakati kila nchi inatuma timu iliyoaminika? Ni zamu yao kushinda, wachezaji wetu warudi kujipanga upya.

Oh yeah kwa VILABU tumefanikiwa kuliko kwa TIMU ya TAIFA na YA TAIFA ndio kichwa cha MWENDAWAZIMU
 
Mayanga mdebwedo huo, acheni usimba na uyanga wenu sasa mlitaka aje jerry tegete? Kiukweli timu ni nzuri na mapungufu ni madogo tu, pale uganda pagumu wadau kumbuka cameroon walikwaruzwa halikadhalika nigeria waliona cha mtema kuni pale, hii timu huyu jamaa poulsen akikaa nayo muda atatufurahisha, msipende shortcut wadau, kumbukeni mbuyu na unene wake ulivyoanza kuota.
Timu yetu ilikua natatizo la kushinda ugenin sasa kiana wameanza.karibu mashujaa wetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom