PICHA: Kikaragosi cha muungano Tz na Znz

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,059
4,053
395043_311184548981641_1377948550_n.jpg

Je kuna ukweli hapa?
Mimi naona Wazanzibari wao wanafaidika zaidi na muungano ukilinganisha na sisi
 
395043_311184548981641_1377948550_n.jpg

Je kuna ukweli hapa?
Mimi naona Wazanzibari wao wanafaidika zaidi na muungano ukilinganisha na sisi

Aliyetengeneza hiki kikaragosi bila shaka atakuwa mwanauamsho, chini ya Shehe Faridi. Na sisi tunaitaka Tanganyika yetu. Hawa Wazanzibari wamezidi sana kutudharau. Ama kweli shukrani ya punda ni kuishia kukupiga mateke, hata umsaidie vipi.
 
Wanzanzibar wanawapa nini watanganyika mpaka tunaona watanganyika wanafaidika na Muungano?
 
Siku muungano ukivunjika wanawake wa ZANZIBAR watajuta kuzaliwa kwani utawala wa SHARIA ya kiislam utaanzishwa ambapo watazuiwa kwenda shule, wakikamatwa wamezini watapondwa mawe hadi kufa. Muungano ukivunjika itapatikana PEMBA na UNGUJA-nje ya muungano hakuna ZANZIBAR
 
Watanganyika tusimfanye nyerere kutokua na akili katika kuunganisha zanzibar na tanganyika.hiyo picha ndo hali halisi yamuungano.ukiwauliza watanganyika muungano unawanufaisha vp wazanzibar?atakujibu wapemba wamejaa kariaokoo wanamaduka.wao wanaiyona hiyo ndo faida.nyerere ameufanya muungano huu ili tanganyika ijibebeshe koti la muungano na sio vengine.kibonzo ni reality beyond the truth
 
Wanzanzibar wanawapa nini watanganyika mpaka tunaona watanganyika wanafaidika na Muungano?
Huoni hapo anachopewa? Vinginevo Watanganyika wangedai MUUNGANO sahihi wa serikali TATU ati. WANAFAIDIIIIIIIIIIIIII.
 
Siku muungano ukivunjika wanawake wa ZANZIBAR watajuta kuzaliwa kwani utawala wa SHARIA ya kiislam utaanzishwa ambapo watazuiwa kwenda shule, wakikamatwa wamezini watapondwa mawe hadi kufa. Muungano ukivunjika itapatikana PEMBA na UNGUJA-nje ya muungano hakuna ZANZIBAR
Kufa muungano hatuombei ila UBORESHWE kwa kuwa na serikali TATU. Muungano DAIMA MBELE!!!!!!!
 
Huoni hapo anachopewa? Vinginevo Watanganyika wangedai MUUNGANO sahihi wa serikali TATU ati. WANAFAIDIIIIIIIIIIIIII.
Mimi naona picha hii haina ukweli bali ni upotoshaji tu,tangu lini mtu aliyekondeana kama huyo Mzanzibar akawa na uwezo wa kumlisha mtanganyika?Naona ingefaa hicho kijiko kingekuwa kinatoka kwa mtanganyika kwenda kwa mzanzibar ingeleta maana.
 
Hii ndo hali halisi kwani malikia wa mchwa hutafuta mwenyewe chakula ndugu yangu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom