PICHA: Katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha aliyejeruhiwa kwa BOMU

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
download+(9).jpg

Katibu wa bakwata Mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarimu Jonjo akiugulia maumivu katika wodi ya majeruhi ,katika hospitali ya mkoa mount Meru baada ya kulipuliwa na bomu la kutupwa na mkono akiwa amelala usingizini nyumbani kwake na watu wasiofahamika majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo. Picha na Josefu Ngilisho.

Picha na Michuzi Blog



THURSDAY, OCTOBER 25, 2012




DSCN6189.JPG


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magessa Mulugo akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa BAKWATA mkoa wa Arusha Bw. Abdulkarim Jonjo anayeuguza majeraha aliyoyapata baada ya kutupiwa bomu nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo eneo la mtaa wa kanisani kata ya Sokoni jijini Arusha.
DSCN6193.JPG

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Afande Liberatus Sabas akiangalia maganda yanayosadikiwa kuwa ya hilo bomu lililotipiwa dirishani katika nyumba ya Katibu wa BAKWATA wa mkoa huo usiku wa kuamkia leo
DSCN6196.JPG

Dirisha lilikotupiwa hilo bomu.

Picha zote na Mahmoud Ahmad
 
Jamani, POLE SANA... Ni watu gani hao Wanafanya UNYAMA wa KUTUMIA MABOMU?
NCHI HII INAELEKEA WAPI???
 
Tutaendelea kusema hapa kuwa Farid/Ponda ni magaidi... Subirini... there is much more to come
 
Haya nayo sasa makubwa!! Kama tumefikia hapa inatisha yafaa hatua za ziada za usalama zichukuliwe zaidi.
 
Ushauri kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama: Ongezeni doria katika mipaka yetu ili kuzuia uingiaji wa silaha ndogo ndogo nchini vinginevyo tutakuwa kama palestina au afuganistan!
 
Jamani, POLE SANA... Ni watu gani hao Wanafanya UNYAMA wa KUTUMIA MABOMU?
NCHI HII INAELEKEA WAPI???

Nadhani kuna watu wanapinga jambo fulani kwa style hii, si unajua baadhi ya watu wameamua kubadirisha style ya kupinga mambo? kwa mfano anaweza akawa anatoa maoni yake ya kupinga muungano kwa kuvunja Bar na kunywa bia alizozikuta.
 
hiyo ni BAKWATA dhidi ya PONDA (jumuiya)


BOKO HARAM huuwa waislam wenye msimamo wa kati huko nigeria.

MRC Kenya wamemshambulia na kumuua chifu wa mombasa mwenye msimamo wa wastani
 
Hii ni ishara ya kulea vyombo vya habari kama redio and TV imaan ambazo zinaendelea kutamba na kuamsha hisia za waislam kwa data ambazo hazijafanyiwa utafiti kupitia wahadhili wa MOROGORO Muslim University. Inatia huruma. Bush aliwahi kusema there are bad and good Muslims. Hii ndo vita iliyopo.
 
Pole utadhi. lakini wanasema mwosha huoshwa! sasa kama mlifurahia makanisa kuchomwa moto, kumbuka vita havina macho au walidhani hiyo nyumba yake ni ya mberoya? maskini pole sana! nakutakia upone haraka
 
Najiuliza tu, wanaupimaje huo msimamo wa wastani? Urefu wa sarawili na madera unahusika?
hiyo ni BAKWATA dhidi ya PONDA (jumuiya)


BOKO HARAM huuwa waislam wenye msimamo wa kati huko nigeria.

MRC Kenya wamemshambulia na kumuua chifu wa mombasa mwenye msimamo wa wastani
 
Dah imekuwaje tena hawa wenzetu wamefikia kutupiana makombora? Inatisha na hii ni signal kwa serikali yetu shupavu!!
 
Hao watakuwa wafuasi wa ponda waliotaka kumpindua mufti si bure!maskini tanzania,nasikia uamsho wanapanga kwenda kuchukua mafunzo somalia!
 
Back
Top Bottom