Picha: Kashfa nzito "tegeta zoo", simba atafuna mtoto. Mmiliki bwana kusaga anataka kuifunika.

Huu uzembe ni wa huyo dada aliyeacha watoto bila uangalizi wa mtu mzima. Na huyo mtoto ni mtundu sana maana alifungua komeo ya uzio wa nje na kuwafuata simba wakiwa kwenye uzio wa wanapoishi. Almanusra hao simba walikuwa wamefungiwa ni ile mikono ya simba kupitia kwenye nondo za uzio wao ndio iliyomdhuru mtoto lau kichwa cha simba kingeweza kupitiliza kwenye nondo mtoto angeliwa hai.

Ieleweke kuwa simba walikuwa wamefungiwa na huo uzio wa awali mtu akisimama hawezi kudhurika na hao wanyama simba. Jambo la busara ni settle nje ya koti la sivyo watuhumiwa sio wenye zuu na wafanyakazi wao tu bali hata familia ina makosa.
 
Hawezi kulipwa kitu. Hilo Onyo unapoingia Zoo lina maana kubwa sana kisheria la sivyo lisingewekwa. Hata unapoenda kupaki gari mahala ukakuta bango la park at your own Risk fikiria mara mbili kabla hujapaki ama kuna mlinzi au hakuna; wanapoandika Onyo sigara ni hatari kwa maisha yako... yoote hayo yana maana kisheria kuwa hicho kitu unachotaka kutumia si salama na hakuna atakae wajibika kwa madhara yoyote utakayoyapata kwa namna yoyote ile. Huyo mwenye Zoo hata hiyo 64000 aliotoa ni ubinadamu tosha.

Hao simba wenyewe walikuwa na Huruma vinginevyo wangeweza kumparamia Shingoni kama kinguruwe mwitu wakamchania chania mbali.
Swala ni je wizara husika inaruhusu zoo zisiwe na wasimamizi?
 
Ni swali tu bandugu: Je na mwenye zoo naye akihitaji fidia
kwa sababu mtoto akuwa chini ya uangalizi wa karibu wa
watu aliokuja nao ambao pia walipaswa kuhakikisha
anakuwa chini ya uhangalizi! Sheria imekaaje hapo?

hapa members watakuona wewe ni mbaya, but, wanasahau kuwa watoto wote walitoka nyumbani bila mwangalizi na hivyo walikuwa exposed to all calamities, imagine huyo binamu mkubwa alipoitwa alipoteza fahamu- je, kama angekutana na mwizi wa watoto barabarani angeweza kuwatetea hawa binamu zake?, mtoto amemfuata simba ndani ya cage yake harafu baba zima anamuanika mwanaye kwenye forum ati anataka msaada wa kisheria; wa kushindana na irresponsibility yake?!
 
pole mwenye mtoto aliyejeruhiwa,mungu akupe nguvu mwanao apone!mungu atamjibu mbaya wako sawa na matendo yake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom