Picha: Kashfa nzito "tegeta zoo", simba atafuna mtoto. Mmiliki bwana kusaga anataka kuifunika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha: Kashfa nzito "tegeta zoo", simba atafuna mtoto. Mmiliki bwana kusaga anataka kuifunika.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nsanu, Jun 26, 2012.

 1. n

  nsanu Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarehe09/06/2012 ndugu Titus Mahanga, aliiruhusu familia yake kwenda TegetaZoo kuangalia wanyama. Kwa wale msioifahamu Tegeta Zoo ipo TegetaKibaoni 2km kutoka ilipo barabara kuu. Hii Zoo inamilikiwa na bwana Wilison Kusaga.

  Mtoto aliyeshambuliwa na simba anaitwa Newton Titus (5), aliongozana na binamu zake Diana (8),
  Lucy (28).
  Taratibuza pale Zoo unapofika usalama ni juu yako, Mtoto Newton Titus (5)pamoja na binamu zake baada ya kuingia ktk Zoo walianza kuzunguka nakuangalia wanyama mbalimbali, walipofika karibu na banda la Simba binamu wao (Lucy-28) akaenda chooni akawaacha binamu zake (Newton na Diana) nje wamngoje. MtotoNewton (5) akatumia muda huo kwenda banda la simba, chakushangaza banda la simba halikuwa na msimamizi yeyote isitoshe uzio au fensi ya banda lilikuwa halina kufuli bali mlangou mebanwa tu kwa kutumia komeo, mtoto Newton (5) akaenda kufungua ulemlango wa banda la Simba ndipo akakumbwa na hiyo dhahama, kulikuwa naSimba wawili wakamshambulia vibaya sana mtoto. Wakati tukio hilo likiendelea mtoto mwingine anayeitwa Diana (8) akakimbia kwenda kumuita binamu wao aliyekuwa chooni ambaye anaitwa Lucy (28) alipotoka choonikwa taharuki akakuta Newton (5) akishambuliwa na Simba, Lucy akaziraipale pale. Bahatinzuri alitokea mtalii mwingine mwenye asili ya Asia akamwokoa mtoto Newton kutoka ktk makucha ya Simba na kumkimbiza hospitali kwa gari yake (Mico dispensary iliyopo tegeta).

  Mtoto Newton kajeruhiwavibaya kichwani, pajani na kiunoni. Mtoto baada ya kupewa matibabu pale dispensary mke wa mmiliki wa Zoo Mrs Kusaga akalipia gharama ya Tshs. 64,000/=, chakusikitisha hakuwahi kutoa tena msaada wa aina yeyote kwa mtoto Newton wala kujulia maendeleo ya mtoto.
  Baba wa mtoto bwana Titus Mahanga alipeleka malalamiko police Tegeta naakapewa RB, police wakamwita Mrs Kusaga kwa mahojiano lakini hakuna kitu ambacho kimefanyika mpaka sasa, zaidi ni police kumtisha bwana Titus Mahanga asijaribu kumshitaki bwana Willilson Kusaga.

  WanaJF
  BwabaTitus Mahanga anataka ushauri wenu wa kisheria juu ya bwana Willium Kusaga mmiliki wa Tegeta Zoo, ikumbukwe kama banda la Simba (uzio)ungefungwa kwa kufuli mtoto Newton asingepatwa na dhahama iliyomkutakupelekea kuatarisha maisha yake. Mpaka sasa hivi mtoto bado haliyake sio nzuri. Na kwa mujibu wa daktari anadai mtoto akiri yakeishavurugika, atakuja kuwa katili au mjinga.

  Namba ya mzazi bwana Titus Mahanga 0717 / 0767 – 441044
  Gongola Mboto – Dar es salaam.
  1.JPG
  mtoto Newton akiwa na Baba yake.

  2.JPG
  mtoto akipatiwa huduma na daktari

  3.JPG
  Nyama ya paja ikiwa imenyofolewa na simba


  4.JPG
  mtoto akiwa na majera ya simba kichwani
   
 2. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  hazina ushahidi
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  mnh, kuna issue nacheck hapa nje mara moja. nakuja
   
 4. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Familia ya mtoto, itafute wakili wafungue kesi Mahakamani.
   
 5. T

  Teresia Mahimbi JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii si mara ya kwanza..kuna kipindi mwaka jana Simba alitoroka na kuleta mtafaruku tukawa tunawah kujifungia ndani..Usimamiz hii zoo ni sifuri kabisaa sishangai sababu naifahamu ni jiran na mtaa wetu Tegeta Block F
   
 6. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,411
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  Utalii wa ndani!?
   
 7. n

  nsanu Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unataka ushaidi gani zaidi ya huu? hacha kutokwa mapovu.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hapo wenye zoo wanamakosa na watu wazima waliokwenda na huyo mtoto zoo wana makosa, hiyo hadithi ya kwenda chooni na mwingine kufatwa Inchon haina mshiko wala ukweli ndani yake. Wote (wenye zoo) na waangalizi wa huyo mtoto walikuwa wazembe.

  Hapa Serikali lazima iingilie kati, hawa wenye ma zoo wana utaalam wa hizi zoo au wanapewa tu vibali kiushikaji? faida ya hiyo zoo kwa taifa ni nini au kwenda kuwatesa tu wanyama?

  Kama ni mimi Tanzania ingeweka zoo ya wale wanyama adimu tu na hiyo zoo iwe inafanyia kazi kuwaongeza idadi yao na sio kwa ajili ya kuwafungia tu kuwacha watu wakatazame. Wange promote hawa watoto wawekewe huduma za kuwapeleka mbuga za wanyama wakajionee live. Faida inayopatikana kutoka kwa watalii wanaokuja kutazama hawa wanyama ingemegwa na kuanzisha idara ambayo itakuwa inawachukuwa mashuleni na kuwapeleka mbuga za wanyama hawa watoto zetu. Inawezekana, ni mipango tu.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Hiyo zoo naona kuna walakini. Pengine hawajajua nini wanatunza ndani ya zoo yao
   
 10. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Kwanza nawapa pole wanafamilia kwa tukio hilo.

  Nimesikitishwa tu na hao wazazi kuruhusu watoto wadogo hivyo kwenda eneo hatarishi kama hilo. Hao wenye zoo walipoweka tangazo kuwa usalama ni juu yako mwenyewe walijua tukio kama hilo laweza tokea wakati wowote maana wanyama wa porini si rafiki wa binadamu tena inapotokea wamewekwa kwenye gereza na kuangaliwa na adui zao bila kuwa na uwezo wa kuwakabili. kwa hilo tangazo tayari linawaondoleeni nguvu ya kisheria maana mlitakiwa muwe makini lakini hamkufanya hivyo watoto wakaachwa kisa chooni. Huyo binamu anawezaje kuwaacha watoto wadogo 5yrs kwenye tundu la simba kwa kisingizio cha choo!? kimsingi huyo ndo alitakiwa awe mtuhumiwa namba moja maana yeye angekuwa makini wala ajali hiyo isingetokea na nyie wazazi muwe watuhumiwa namba 2 kwa kuruhusu watoto wasiojua lolote kwenda eneo hatarishi kwa maisha yao.

  Msijisumbue na mahakama maana hamtoshinda tuhuma hizi zinawaangukia ninyi wenyewe. mtibieni mtoto apone. Mungu kamsaidia hakufa basi mshukuruni.
   
 11. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  I'm breathless
   
 12. n

  nsanu Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ok na kwa nini fensi ya banda la simba lisifungwe kwa kufuli? badala yake wao wamerudishia kwa komeo tu kana kwamba ndani ya banda wapo sungura.
   
 13. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,047
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Mimi kwangu Nyoka na simba sina muda nao hata kama wanaonyeshwa bure. Hata hivyo waweza kuta wazazi hawakujua kuwa watoto walienda huko. Walikuja kuambiwa baadaye kuwa mtoto wako ameenda huko. Lakini tuelekeze katika kutiunza wanetu kwani wengi wao siku hiz watundu sana, kwa nini alifungua lile geti?
   
 14. B

  Baniani Mzuri Senior Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Bado hatujapata mwanasheria wa kuchangia vilivyo kwenye hii thread
   
 15. MANI

  MANI Platinum Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Labda wanamfananisha na paka !
   
 16. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  inaonekana wanyama wanateswa hivyo wanahasira na watesaji, wanaona waanzie kwa bwana mdogo iwe fundisho, hii ni kama wewe ukimtesa house girl , ujue na wewe ukitoka ni lazima mtoto ale konde la uso
   
 17. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Negligence in part of Zoo owner kwani kulitakiwa kuwe na Mwangalizi tena mwenye silaa in case chochote kitaenda mrama na aongoze watu wote wanaonda kuangalia ,wanayama huwa wanakumbuka asili once in a while.

  Hapa fidia ni muhimu na hata kiubinadamu ilipaswa mwenye zoo ndio achukue jukumu la kuzungumza na familia sio kungoja kwenda mahakamani kama ni mtu mwenye busara maana hata wakienda huku ni Lawyers ndio watafaidi hizo fee tu hamna jingine na hakimu naye kama vipi anakula kidogo hapo. Aaaaaaaaaaaaaah hii nchi !
   
 18. GP

  GP JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nimeipenda hii
   
 19. n

  nsanu Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alafu kibaya zaidi mwanzo kulikuwa hakuna tangazo linalosema ulinzi ni juu yako, baada ya hili tukio ndio wameweka hilo tangazo la ulinzi eti ni juu yako, what a shame!. Hii Zoo inabidi serikali waifungie, nimejaribu kuchunguza watu wengi sana wanamalalamiko mengi kuhusu hii Zoo. Kuendelea kuwepo kitakuja kutokea jambo baya zaidi ya hili.
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  badala ya kuwapa watoto hela wakanywe sipi juice mpango mzima mnajifanya wazungu kwenda kuangalia midubwana ya porini haya sasa kararuriwa na simba....hebu mtupishe bwana tuko bize na mambo ya bajeti na punguzo la pawa tila na matreka ya suma JKT pamoja na kukagua matofali huku msoga tutarudi baadaye ku deal na hiyo issue ...
   
Loading...