PICHA: Kamati ya Bunge yatembelea Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

JNICC+019.jpg
Jengo la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam linavyoonekana kwa nje baada ya kukamilika. Jengo hilo linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa lipo Makutano ya Barabara za Shaaban Robert na Garden Jijini Dar es Salaam.

JNICC+042.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule (kushoto) akimkaribisha Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.), Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
JNICC+065.jpg
Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.
JNICC+073.jpg
Wajumbe wa Kamati ya NUU na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati akiwakaribisha.
JNICC+175.jpg
Mhe. Azzan akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya NUU na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia ni Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje.
JNICC+144.jpg
Katibu Mkuu, Bw. Haule akitoa maelezo kuhusu Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama waliotembelea kituo hicho
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Ina Maana Serikali ya CCM; Ndio BYE-BYE ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTER???

Wachina Wamejenga kwa MKOPO?
Sasa ni Wamevunja All Connections with Arusha?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kituo safi sana! Tunaomba kingine kijengwe Kigoma au Songea ili tubalansishe maendeleo ya nchi yetu. Kila kitu Dar?
 
JNICC+065.jpg

Katibu Mkuu, Bw. Haule akiwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere walipokitembelea hivi karibuni.

Viongozi wa Tanzania wanasafiri sana lakini sijui ni kwanini hawajifunzi? Kwenye hiyo picha katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya nchi za nje amesimama wakati anaongea! Huu ni ushamba na ni uncessary 'distraction' kwa wale wanaokuliza maana unakuwa juu sana - facial contact inakuwa kwa tabu, wao wamekaa chini wanaangalia juu kukusikiliza!

Ushamba huu umeenea kila ofisi za serikali. Hivi hawajufunzi huko wanakokwenda? Wanafikiri ni alama ya heshma lakini huu ni ushamba na kama nilivyosema unawafanya wanaokusikiliza waanze kuangalia juu kama wanatazama ndege inaruka!
 
Wakazania (watanzania) mmezidi ushamba na ulimbukeni. Kila kitu nyerere! Nyerere!, kwani majina mengine hayapo? Uwanja wa ndegekimataifa (ule mchafu) dar, chuo cha kivukoni, campus ya mlimani, uwanja wa sabasaba dar, uwanja wa nanenane morogoro, uwanja wa mpira shinyanga vyote jina hilo hilo la nyerere, inatia kinyaa sasa. Mbona mnamfanya awe kama mzimu wa tambiko kwa kila kitu kutumia jina hilo hilo kana kwamba ana utukufu fulani. Kwa kweli mnaniudhi sana.
 
Kipo wapi hiki? Je mama Maria Nyerere atanufaika vp na makusanyo maana mmemtupa sana kule 7 7 mnakula wenyewe hata airport bibi haambulii chochote
 
Ina Maana Serikali ya CCM; Ndio BYE-BYE ARUSHA INTERNATIONAL CONFERENCE CENTER???

Wachina Wamejenga kwa MKOPO?
Sasa ni Wamevunja All Connections with Arusha?

usikonde, bado Arusha pako more attractive kwani DAR hapana hadhi kwa ajili ya miundombinu mibovu, ila HIKI KITUO kitapunguza biashara za Serena and the like.

Itasaidia sana kwa mikutano inayofanyika hapa DAR

Inapendeza kama Kigoma, Mwanza, Mtwara, Iringa, Sumbawanga napo panaInternational conference centres
 
Wakazania (watanzania) mmezidi ushamba na ulimbukeni. Kila kitu nyerere! Nyerere!, kwani majina mengine hayapo? Uwanja wa ndegekimataifa (ule mchafu) dar, chuo cha kivukoni, campus ya mlimani, uwanja wa sabasaba dar, uwanja wa nanenane morogoro, uwanja wa mpira shinyanga vyote jina hilo hilo la nyerere, inatia kinyaa sasa. Mbona mnamfanya awe kama mzimu wa tambiko kwa kila kitu kutumia jina hilo hilo kana kwamba ana utukufu fulani. Kwa kweli mnaniudhi sana.

Ushindwe na ulaaniwe!
 
Toa mawazo yako wewe ungependa paitweje, siyo kukosoa bila kutoa mwelekeo, ndo maana hata mitihani ya shule ya msingi mnafeli mnaanza kusema Ndalichako...!
 
namwalimu atafundishaje darasani unataka nae akae,kwa sababu wanafunzi wamekaa.wewe ndio mshamba ambae unataka tuige kila kitu ulaya.
 
toa mawazo yako wewe ungependa paitweje, siyo kukosoa bila kutoa mwelekeo, ndo maana hata mitihani ya shule ya msingi mnafeli mnaanza kusema ndalichako...!

acha ulimbukeni, kwani kuna ulazima kulisheheneza jina la nyerere kwenye kila taasisi.
 
Wakazania (watanzania) mmezidi ushamba na ulimbukeni. Kila kitu nyerere! Nyerere!, kwani majina mengine hayapo? Uwanja wa ndegekimataifa (ule mchafu) dar, chuo cha kivukoni, campus ya mlimani, uwanja wa sabasaba dar, uwanja wa nanenane morogoro, uwanja wa mpira shinyanga vyote jina hilo hilo la nyerere, inatia kinyaa sasa. Mbona mnamfanya awe kama mzimu wa tambiko kwa kila kitu kutumia jina hilo hilo kana kwamba ana utukufu fulani. Kwa kweli mnaniudhi sana.
Sasa kuna majina gani yenye mvuto? Mkapa, Kikwete, Lowassa, Chenge, Rostam? Bila bila hapo, Nyerere ndo jina lenye mvuto kama huamini nenda kasikilize hotuba zake, kama kaongea jana vile.
 
Back
Top Bottom