Picha kali za Instagram na Facebook ni tatizo kwa vijana wa leo

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,876
3,616
Utandawazi umekuwa mkubwa sana. Vijana wanapenda kuwa inspired na vijana wenzao ambao kimuoneokano na picha nzuri za Photoshop wanazo-post mtandaoni na kuonyesha mafanikio fake yanavyo waharibu vijana wengine. Na kuhisi kama vile kila anaepost picha kali Instagram au Facebook basi amefanikiwa?

Kiuhalisia hali haipo hivyo; mtu anaweza kupost picha aliyopiga kwenye nyumba ya watu au gari ya mtu. Au hata anaweza kupiga picha na aina fulani ya watu ambao wamefanikiwa kweli ili kuonekana katika jamii kama na yeye ni katika wanaoelekea kufikia malengo yao lakin kiupande mwingine hii ni dalili ya msongo wa mawazo au depression yan kuonyesha upande ambao hata hauna.

Mtu anaweza kupost picha kali insta ukatamani maisha yake lakin kwa upande wa pili inawezekana maisha yako ni mauri kushinda yeye.

Mfano, nawajua watu wanapost picha katika mandhari mazuri hadi unaogopa lakini baada ya muda mtu huyo anakuomba buku aweke bandle hapo ndio unajiuliza.
 
Yule mwamba alieua juzi sinza ukifuatilia insta yake anaonekana mtu wa bata. Najiuliza bata linaingilia vipi na stress za kichwan
Hahah Maisha ya ku pretend mitandaoni hayo mkuu.

Maisha yako binafsi ya Bata unahitaji kuyaonyesha mitandaoni ili mtu upate approval kutoka kwa Nani?Msongo wa mawazo is real mkuu.
 
Mtoto wa kiume anaenda na kibegi cha nguo location kupiga picha na kupost status au insta kama hamisa mabeto.
 
Nataka wadogo zangu wanifate mimi. Nimefuta picha zangu zote facebook 31 years now naelekea uzeeni, naitafuta akhera yangu
 
Back
Top Bottom