PICHA: JK: Aongoza Kikao Cha Kamati Ya Ulinzi Ya SADC Jijini Dar es Salaam

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

POSTED ON DECEMBER 7, 2012Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya uchumi na maendeleo ya Kusini (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ili kushiriki kikao cha kamati hiyo.Pembeni ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao.


Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete( Wanne Kushoto) akiwa na viongozi SADC waliopo katika kamati hiyo.Wengine katika picha ni Rais Wa Afrika ya Kusini Jackob Zuma(Watatu kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia),Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano(wapili kushoto) na kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.


Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini(kulia) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz SalomaoMwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano,Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini( wa pili kulia).Picha na Freddy Maro,Ikulu.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

Mikutano MINGI inafanyika IKULU... Ni KUSAVE PESA za KUKODI KUMBI??
 

Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
2,000
Hawa wote ni supporters wa Joseph Kabila. Safari hii misheni za Kagame kule Goma zimedhibitiwa vizuri.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Ulitaka ifanyike wapi? ofisi ya Rais ipo Ikulu.

MIKUTANO ya SADCC inafanyika kwenye HOTELI VYUMBA vya MIKUTANO au A CONFERENCE CENTER...
IKULU sio pa KUCHEZEA kama HIVYO... NADHANI HAIJUI IKULU ya SOUTH AFRICA ikoje... Kama anaweza kubeba NDEGE na kusafiri kila KONA kweli kukodi CHUMBA CHA MIKUTANO ni SHIDA? na KUNA CONFERENCE CENTER MPYAAA imejengwa kwa MKOPO wa CHINA... Angalau wangejaribu kutumia HUO au wa BENKI KUU n.k
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
JK hana uwezo wa kusimamia ulinzi na usalama kwenye hili eneo la kusini mwa Africa kwa sababu ameshindwa kuimarisha usalama wa raia ndani ya nchi. Kwake kumemshinda atawezaje ya wenzake?
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,261
2,000

MIKUTANO ya SADCC inafanyika kwenye HOTELI VYUMBA vya MIKUTANO au A CONFERENCE CENTER...
IKULU sio pa KUCHEZEA kama HIVYO... NADHANI HAIJUI IKULU ya SOUTH AFRICA ikoje... Kama anaweza kubeba NDEGE na kusafiri kila KONA kweli kukodi CHUMBA CHA MIKUTANO ni SHIDA? na KUNA CONFERENCE CENTER MPYAAA imejengwa kwa MKOPO wa CHINA... Angalau wangejaribu kutumia HUO au wa BENKI KUU n.k
Ni kikao cha kazi mkuu, wapo viongozi wachache , muda mwingine kiusalama ni muhimu vikao vidogo kama hivyo vikafanyikia IKULU huitaji kuwa na security arrangenment and palnning kubwa na pia unapunguza usumbufu kwa raia wakati wa arrangement ya usalama kama kikao kingefanyika hotelini. IKULU ni secured so hakuna gharama za ziada za kusecure maeneo mengine kwa ajili ya kikao cha watu wachache jumlisha na ishu ya mafoleni nk, kiusalama na kiuchumi ni sahihi kikao hicho kufanyika IKULU. Mwisho tu intelejensia pia inahusika, ukitaka kupeleka kikao katika hoteli fulani mathalani blue pearl nk ni lazima ujue wapangaji waliopo kwa siku hiyo pia.
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,683
2,000

MIKUTANO ya SADCC inafanyika kwenye HOTELI VYUMBA vya MIKUTANO au A CONFERENCE CENTER...
IKULU sio pa KUCHEZEA kama HIVYO... NADHANI HAIJUI IKULU ya SOUTH AFRICA ikoje... Kama anaweza kubeba NDEGE na kusafiri kila KONA kweli kukodi CHUMBA CHA MIKUTANO ni SHIDA? na KUNA CONFERENCE CENTER MPYAAA imejengwa kwa MKOPO wa CHINA... Angalau wangejaribu kutumia HUO au wa BENKI KUU n.k

Ikulu panatosha kwani wako wangapi? Wacha ulimbukeni, ati wakodi ukumbi unafikiri pesa za walipa kodi ni za kuchezea?


BTW Mugabe yuko wapi? Au kasusa?

 

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,387
2,000
Ina maana kwenye SADC Rwanda na DRC hawamo mbona hawajatuma wawakilishi, nikumbusheni jamani maana tokea enzi zile za Civics sijajibrush tena kuhusiana na nchi wananchama wa haya makundi
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Ikulu panatosha kwani wako wangapi? Wacha ulimbukeni, ati wakodi ukumbi unafikiri pesa za walipa kodi ni za kuchezea?BTW Mugabe yuko wapi? Au kasusa?Haya Matusi; Umeona nimeongelea ULIMBUKENI? KILIMANJARO HOTEL iko KARIBU wangeenda huko... IKULU sio NYUMBA ya MIKUTANO... na WAPIGA PICHA ... UMEISHA WAHI KUIONA IKULA ya SOUTH AFRICA na kikwete kaisha kwenda huko MARA 10?
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,683
2,000
Haya Matusi; Umeona nimeongelea ULIMBUKENI? KILIMANJARO HOTEL iko KARIBU wangeenda huko... IKULU sio NYUMBA ya MIKUTANO... na WAPIGA PICHA ... UMEISHA WAHI KUIONA IKULA ya SOUTH AFRICA na kikwete kaisha kwenda huko MARA 10?

Matusi ni yapi? Ikula ndio nini? Au ndio unaanza kuongea kibwiko?
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Matusi ni yapi? Ikula ndio nini? Au ndio unaanza kuongea kibwiko?


BADO NI IKULU na MAPARTY


President Jakaya Mrisho Kikwete receives a new CD from South Africa song bird and UNICEF's Goodwill Ambassador Yvonne Chakachaka during a dinner he hosted for members of the 5th Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) Partners Forum at the State House in Dar es salaam.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Matusi ni yapi? Ikula ndio nini? Au ndio unaanza kuongea kibwiko?


Is a typo ERROR and U MAKE IT A BIG DILL... Angalia IKULU ni HOTELI PIA

gavi10.jpg
 

NdasheneMbandu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
940
0
Inachekesha sana kwa jinsi kikwete na zuma wanavyoonekana utadhani ni marais wa nchi zinazofanana kiuchumi. Tena basi mwingine anaweza akadhani nchi anayoongoza kikwete ni more developed than ya mwenzake zuma kumbe ni kinyume chake tena sana sana sabmna sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom