Picha: JK amtuma kaka yake mazishi ya ofisa usalama aliyeuawa mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
THURSDAY, DECEMBER 13, 2012MAZISHI ya aliyekuwa ofisa Usalama wa Taifa (mstaafu) mkoa wa Mbeya RSO Joseph Nelson Mwasokwa, aliyeuwawa usiku wa kuamkia Desemba 9, mwaka huu Jijini Mbeya, yamefanyika katika Kijiji cha Ibungu wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kaka wa rais Kikwete Selemani Kikwete akinigia wilayani kyela kwenye mazishi ya marahamu mzee mwasokwa
Aliyekuwa mkuu wa mkoa mbeya Mwakipesile akiongea na mzee Mwambulukutu kwenye mazishi ya marehemu Mwasokwa
Waombolezaji

Katika mazishi hayo, Rais Jakaya Kikwete aliwakilishwa na kaka yake Selemen Kikwete ambaye pia alipata nafasi ya kutoa pole kwa waombolezaji ambao hawakuruhusiwa kuuona mwili wa marehemu bali kilichoruhusiwa kuangaliwa ni picha yake iliyokuwa juu ya jeneza.

Mbali na Seleman Kikwete, viongozi mbalimbali nwalihudhuria msiba huo akiwemo Mkurugenzi mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Tanzania Ndugu Othuman, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya mstaafu John Mwakipesile na viongozi kadhaa waandamizi wa Serikali.

Marehemu Mwasokwa akatwa na kitu chenye ncha kali kisogoni ambako wauaji ambao hawajajulikana walifanya kitendo hicho kisha kuulaza mwili wake kifudifudi nje ya geti la nyumba yake eneo la Block T jijini Mbeya.

Taarifa za Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, zimesema kuwa wauaji wanaonekana kuwa walitumia panga ambapo marehemu alikutwa na majereha makubwa sehemu za shingoni, kichwani, mabegani na mkono wa kushoto.

Kwa hisani ya Kalulunga
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
HIVI ALI HASSAN MWINYI na MKAPA walituma Kaka zao na Dada zao kwenye DHIFA ya TAIFA kama KILIO???

Au Kaka yake PIA ni MJUMBE wa NEC-CCM?
 
Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,519
0
Mnyonge Mnyongeni, ila Haki yake Mpeni, Angeenda LAZIMA kuna watu wangekuja na malalamiko kibao hapa kuwa oooh "RAIS WA KUHUDHURIA MISIBA..etc Sasa hajaenda bado kuna watu wana-complain!!!! kweli uongozi ni mzigo wa mwiba.
 
Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,124
0
Nadhani kali kuliko zote ni pale Mwl Nyerere alipobariki mdogo wake Joseph Nyerere awe mwenyekiti wa Youth league sasa UVCCM na akaruhusu mke wa makamu wake wa Rais Bi sofia kawawa kuwa mwenyekiti wa UWT Taifa kwa kisingizio kuwa wamechaguliwa na 'wanachama WENYEWE bila ya kupingwa'.
 
Chiya Chibi

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
484
195
Umejuaje kamtuma? Kwan haiwezekan mzee Sele kujiwakilisha mwenyewe msiban? Nadhan officially amemtuma RC ama kiongoz mwingne wa serikal. Anyway R.I.P
 
Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,445
2,000
Jk kumtuma kaka yake sioni shida
na sio lazima ahudhurie kila msiba
mambo mengine sio ya kuhoji hoji
ni utu zaidi na sio siasa kila kitu
 
Kindimbajuu

JF-Expert Member
Jul 8, 2009
710
195
HIVI ALI HASSAN MWINYI na MKAPA walituma Kaka zao na Dada zao kwenye DHIFA ya TAIFA kama KILIO???

Au Kaka yake PIA ni MJUMBE wa NEC-CCM?
kwani seleman kikwete alimuwakilisha rais jakaya kikwete au jakaya kikwete au familia ya mrisho kikwete? tusichanganye mambo , tusiwe wepesi kuona makosa , tukifanya hivyo ni raisi hata sisi kukosea..... picha ninayoiona mimi ni kuwa either marehemu anafahamika kwa familia ya mrisho kikwete au kwa familia ya suleman kikwete....
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,254
2,000
Inawezekana ni marafiki na labda walisoma wote!tuache hizo!au ukute wameoleana maana huyu mzee ameoza kijana wake mwaka huu kama sikosei!
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,318
2,000
HIVI ALI HASSAN MWINYI na MKAPA walituma Kaka zao na Dada zao kwenye DHIFA ya TAIFA kama KILIO???

Au Kaka yake PIA ni MJUMBE wa NEC-CCM?

Nani kasema hii ni dhifa ya kitaifa? Kwa minajili gani hii ni dhifa ya kitaifa?

Kwa nini JK kama Jakaya asiweze kuwakilishwa na kaka yake? Unajuaje kama JK hakuwa na mahusiano ya binafsi na marehemu hata kabla ya kuwa rais na hapa anarehemu kwa minajili hiyo kuendeleza ukaribu wa familia ya Kikwete na familia ya marehemu kwenye wakati huu mgumu?
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
kwani seleman kikwete alimuwakilisha rais jakaya kikwete au jakaya kikwete au familia ya mrisho kikwete? tusichanganye mambo , tusiwe wepesi kuona makosa , tukifanya hivyo ni raisi hata sisi kukosea..... picha ninayoiona mimi ni kuwa either marehemu anafahamika kwa familia ya mrisho kikwete au kwa familia ya suleman kikwete....

Ndio Maana Rais akamtuma kaka YAKE? Basi wasingesema JK amemtuma Kaka yake... Wangeweka KICHWA cha HABARI KINGINE... Kiswahili KIPANA... NA NI BORA zaidi ya HIVYO ILIVYOANDIKWA!!!
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
Nani kasema hii ni dhifa ya kitaifa? Kwa minajili gani hii ni dhifa ya kitaifa?

Kwa nini JK kama Jakaya asiweze kuwakilishwa na kaka yake? Unajuaje kama JK hakuwa na mahusiano ya binafsi na marehemu hata kabla ya kuwa rais na hapa anarehemu kwa minajili hiyo kuendeleza ukaribu wa familia ya Kikwete na familia ya marehemu kwenye wakati huu mgumu?

Shughuli za KITAIFA ziwe ni KILIO au SHEREHE zinaitwa DHIFA>>>>
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,318
2,000

Shughuli za KITAIFA ziwe ni KILIO au SHEREHE zinaitwa DHIFA>>>>

Sija question dhifa, nime question "kitaifa".

Kwa nini huu msiba uwe wa kitaifa mpaka kufanya "dhifa ya kitaifa"?

Kama Kikwete anajuana nao ki-MsogaMsoga na katuma ujumbe wa familia kama rafiki wa familia utasemaje hapo?
 
Kindimbajuu

JF-Expert Member
Jul 8, 2009
710
195

Ndio Maana Rais akamtuma kaka YAKE? Basi wasingesema JK amemtuma Kaka yake... Wangeweka KICHWA cha HABARI KINGINE... Kiswahili KIPANA... NA NI BORA zaidi ya HIVYO ILIVYOANDIKWA!!!
sielewi unataka kuzungumza nini. nimekwambia kuwa ninachokiona hapo ni mahusiano binafsi ya kifamilia na si vinginevyo. sasa habari kusema JK amemtuma kaka yake ni kosa?.wangeandika raisi amemtuma kaka yake ni sawa hapo tungesema ni walakini. JK ni jakaya kikwete, sioni tafsiri nyingine ya JK au wewe kwako JK inasimama kwa maneno gani?. jakaya kutumana na ndugu yake ktk mambo yao binafsi isiwe mjadala kwetu wananchi... haswa ikiwa hawavunji sheria za nchi. niambie kwa uelewa wako ni ishara gani imeonyesha kuwa taasisi yetu ya uraisi iliwakilishwa na kaka wa mkuu wa hiyo taasisi kwenye mazishi ya afisa mstaafu wa usalama wa taifa?. tusimame ktk ukweli tukiongeza chumvi kwa ukweli tunafanya hata ukweli mdogo tulio nao ukatiwa walakini
 
Kulikuwa kuna haja ya kuutangazia ULIMWENGU?
 
Chum Chang

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
999
0
Kaka yake Kikwete na Marehemu walikuwa marafiki

Je kwa kuwa kaka yake Kikwete aruhusiwi kwenda kuzika?
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,702
2,000
Ni assasination plot ama ni majambazi?Maana wanaposema walimlaza kifudifudi mbele ya geti lake inaonyesha kama vile walimwua makusudi halafu wakamweka hapo?Anyways,poleni sana wafiwa na RIP mzee Mwasokwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom