Picha inaonesha Kalvin Patrick Yondani akitia saini kuchezea Yanga jana Usiku Tansoma Hotel... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha inaonesha Kalvin Patrick Yondani akitia saini kuchezea Yanga jana Usiku Tansoma Hotel...

Discussion in 'Sports' started by mzee wa njaa, Jun 7, 2012.

 1. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yondani_akisign_kuichezea_yanga.jpg

  Mchezaji Kelvin Yondani akisaini mkataba wa usajili mbele ya kiongozi wa Yanga Seif Ahmed usiku huu, katika picha hii Yondani anaonekana akiwa amevaa fulana na timu ya taifa ambazo zimeanza kutumika mwezi mmoja uliopita baada ya stars kuingia mkataba na TBL KUPITIAKilimanjaro.

  Taarifa nilizozipata hivi punde Yondani amefuatwa kwenye kambi ya timu ya Taifa iliyopo kwenye Hotel ya Tansoma jijini Dar Es Salaam.


  Kauli ya Rage Ismail mbona inapishana na anachofanya Yondani kwenye picha hiyo..

  Source: Shafii Blog.
   
 2. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  na h izo pesa hapo mezani ndizo za usajiri? hana bank ama? TZN bwana ndio maana hatuendelei
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  simba wanamkongwe ila yanga wanakinda lakini majina sawa Kelvin Patrick Yondani
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  huyo anae msainisha anafahamu Yondani ana mkataba Simba?
   
 5. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mkuu,so Huyu Yondani aka yo-nje kasaini jana right?kama ni kweli basis Aden Maharage kajidhalilisha lol!
   
 6. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,680
  Trophy Points: 280
  Karibu Yanga Kelvin Yondani.
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mzee wa Njaa nawe bwana...
  Kwani humjui Ismael Aden (Maha)Rage wewe?...huyu si ndiyo aliyeutangazia Uma wa watanzania msimu wa usajili wa mwaka jana kuwa wamemtuma Kaburu akamalizane na Keneth Asamoah na Club yake aliyoitaja ya Hearst of Oak kule Ghana,hivi kweli leo hii tunaomjua (Maha)Rage tunaweza kweli kushangaa statement yake,katika maisha yangu sijawahi kuona Kiongozi mwenye Courage ya kuongea uongo(si mara 1 wala 2)kwa Public kama (Maha)Rage,sijawahi kwakweli.
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu Yondani anauza BUNDUKI kisha anannunua RUNGU?
   
 9. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mbona hiyo ya Asamoah ni ya zamani?
  Mkuu chukua ya juzi juzi eti wameshamsajiri NIZAR na watamvalisha jezi na kumtambulisha siku ile ya mechi ya Yanga na Simba,matokeo yake wakamtambulisha Sumae na wakamvalisha jezi lol!siku za Maha-Rage simba zinahesabika pia.Maana ata wao simba watachoka na propaganda zake.
   
 10. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Doh asante kwa kunikumbusha Kiongozi,Mzee wa ajabu sana huyu na mimi nasema huyu Mzee (Maha)Rage atakuja kuondoka vibaya pale kuliko hata alivyoondoka Nchunga Yanga,wee mwache.
   
 11. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nilistaaf kushughulika na Soccer ya bongo yaani kitendo cha usajili ni kitendo cha wengine kusema tumemsajili na wengine wakasema wakwetu kwani mpaka wakuu wa vilab wakalumbana wakalumbana kwa suala dogo ka hili je? masuala mtambuka wataweza? hii ndio bongo
   
 12. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Nahisi kama kawaroga vile!kwanini wasijadili ya kwao na badala yake wanajadili ya yanga?huo kama MAHA-RAGE kawaroga ili wasimpopoe?
   
 13. Arsenal

  Arsenal Senior Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wenye alili tumetulia tu, kwenye form iyo Yondani kalikosea jina lake na mwaka wake wa kuzaliwa makusudi ili msiweze mshitaki kwaio ni kama mmempa unsecured loan Yanga...i love Bongo
   
 14. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Nasikia CANAVARO nae kasaini Simba leo!
   
 15. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,806
  Likes Received: 642
  Trophy Points: 280
  Yaani hata mie nimechoka kabisa, miburungutu ya pesa hiyo wameiweka mezani eti kama uthibitisho. yaani hovyo kabisa hawa jamaa, hili ni tatizo la kujifunza na labda kuwa na elimu ya jinsi mambo ya kimichezo yanavyotakiwa kuenda na sio kukurupuka hovyohovyo namna hiyo.
   
 16. M

  Masuke JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Wewe Anselm na Spika, kocha Minziro hamjamlipa mshahara wake wa miezi mitatu halafu mnaonyesha mabulungutu kwa Yondani namna hiyo akiyaona atajisikiaje?
   
 17. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rage alisema wamemchukua Nizar kumbe uongo na wala sitashangaa hili na Yondani. Hizi ni magumashi katika soka la bongo.
   
 18. M

  Masuke JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hapa ngoma nzito, huyu dogo anaweza asicheze mpira miaka miwili, Rage naye kashaonyesha mkataba ambao Yondani kasaini.
   
 19. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Acha kusoma magazeti ya Shigongo mtoto!Ebu njo leo jioni hapa mitaa ya twiga na jangwani uone mikakati endelevu yetu.
   
 20. M

  Mafuluto JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,602
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  ...photoshop? huyo pembeni mwenye jezi nyekundu mbona kafichwa..? Na Yondan si kashakanusha ??

   
Loading...