MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Hatimaye Humphrey Polepole ala kiapo cha Ukuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara baada ya mjadala mrefu kuhusu uteuzi wake kama ulivyofanywa na Rais Magufuli tarehe 18 Aprili 2016.
Baada ya kiapo, Polepole amewaahidi wana Musoma kuwatumikia kwa nguvu zake zote huku akitanguliza weledi, Uadilifu, na nidhamu. Amewaomba wakaaji wa Musoma ushirikiano wa karibu kikazi kwa sababu umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo alimtaka kufanya kazi ndani ya falsafa ya Rais Magufuli inayosema 'HapaKaziTu' ili kuisimamia kikamilifu Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Sherehe ya kumuapisha ilihudhuriwa na viongozi wote wa Kamati za Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, viongozi wa dini mbali mbali, ndugu, jamaa na marafiki.

MKUU wa wilaya ya Musoma,Humphrey Polepole,akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo.
Humphrey Polepole akisaini kiapo.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Muhongo akitoa nasaha baada ya kumuapisha Humphrey Polepole.
Humphrey Polepole akizungumza maneno mawili matatu baada ya kuapa na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma.
Viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama wakishuhudia tukio.
Viongozi wa dini mbali mbali wakishuhudia tukio la kuapishwa.
Mkuu wa Mkoa, Mulongo na Mkuu wa Wilaya, Polepole wakiwashukuru watu waliohudhuria hafla hiyo.
Picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara.