PICHA:Hivi ndivyo Mh:Mwigulu Nchemba alivyohitimisha kampeni kwa kishindo Arusha,Avuna CHADEMA

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Naibu katibu Mkuu wa CCM Tanzania bara Mh.Mwigulu Lameck Nchemba Madelu akiwasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani Jijini Arusha kata ya kimadolu hii leo tar.15/06/2013

Mapokezi yamepamba moto

Mamia ya wananchi na wanachama wa kata ya kimadolu wakiwa tayari kusikiliza mkutano wa hadhara wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani kwenye kata yao.

Mnapo sema CCM imejaa wazee"kwani sisi ni wazee?"

Juliana Shonza ambaye ni mmoja wa wanachama wa CCM wanaopigania chama kwenye kampeni za uchaguzi wa udiwani jijini Arusha.Juliana amewaomba wananchi kudumisha amani siku ya kesho kwenye zoezi la upigaji kura.

Huyu ni kada wa CCM anayefahamika kwa jina la Mtela mwampamba.Amepata nafasi ya kuwa mmoja ya safu ya makada wa CCM walioongoza timu ya kampeni jijini Arusha.Amewaomba wananchi wa Arusha na wana-Kimadolu kujitokeza kupiga kura.Amesema sanduku la kura ndio sehemu sahihi ya kuimaliza CHADEMA na upinzani kwenye uchaguzi huu mdogo wa udiwani unaotarajiwa kufanyika kesho jumapili.

Aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA na mtu wa karibu wa Mbunge wa Arusha Ndugu Niko,sasa ni mwanachama wa CCM amesema"Licha ya kuwepo dalili za kundi la Lema kuleta vurugu hapo kesho kwenye uchaguzi naomba wananchi mjitokeze mapema sana kupiga kura.Kwa wale wakristo tukitoka kanisani tukapige kura kwa mgombea wa CCM Bi.Edna Jonathan Saul

"Kapigeni kura,usalama upo na hakuna wa kuwatisha"Mh.Mwigulu nchemba

"Upinzani wamewafanyia nini?Huyo diwani wao anagombea iliaende Halmashauri akafanye nini?Sera na ilani inayotekelezwa niya CCM.Kumpeleka mpinzani halmashauri ni kutafuta kurudi tena kwenye hali ya maandamano na kelele ambazo hazileti maendeleo"Naibu katibu Mkuu CCM.

Kazi na dawa.Pichani ni kijana aliyejitokeza kurudisha kadi ya CHADEMA Mbele ya Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara,Mh.mwigulu Nchemba

"Mmeionaaaaaaaa?Kijana amejitambua anarejea kwenye chama cha watu wenye nia na maendeleo,CCM chama cha kitaifa"Naibu Katibu Mkuu Mwigulu Nchemba

Kijana akiwa amependeza kofia na kitambaa cha CCM,Huku Mh:Mwigulu Nchemba akionesha kadi ya CHADEMA kama ishara ya kupata mpiga kura mwingine kwenye uchaguzi wa kesho tar.16/06/2013

Karibu sanaa nyumbani,CCM Oyeeeeeeeeee.Viva CCM Vivaaaaa

Naibu katibu mkuu akisisitiza jambo."Naomba sana chukua muda wako kidogo tu nenda kapige kura ndipo uendelee na mambo mengine.Nendeni mkaipe ushindi CCM,Nendeni mkakaribishe maendeleo ndani ya kata ya kimadolu.Hao wapinzani wapo bize kupigania kuingia Halmashauri waende wakapambane na meya na sio kuwaletea maendeleo.Niambieni ni kitu gani hata kidogo tu walichowafanyia hao wapinzani hapa Arusha na kwenye kata yenu?"Mwigulu nchemba

Mamia ya Wanachi wakiwa na utilivu wa hali ya juu wakimsikiliza Naibu katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba

"Mmemuonaaaaa?Huyu ndiye chaguo la kimadolu.CCM ndio chama cha kuwaletea maendeleo.Chuki mnazojazwa kuhusu CCM na serikali yake nizauongo kwasababu wao hawanachakuonesha walichokifanya kwaajili ya Kimadolu.Mchagueni Bi.Edna Jonathan saul mujihakikishie kata yenu kufikiwa na maendeleo ya halmashauri."

Mh.Mwigulu nchemba akihitimisha mkutano wa hadhara kwa kumnadi mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM Bi.Edna saul.Nanukuu"Huyu ndiye diwani wenu mpya,kwa muda wa miaka miwili ijayo atawaletea maendeleo mliyoyakosa kwa miaka miwili iliyopita.Wakuamua kuwa yeye awe diwani hapo kesho ni nyie wanakimadolu kujitokeza kwa wingi kupiga kura"


"Nawaombeni kudumisha amani na upendo,kuna maisha nje ya siasa,tusishabikie vyama vya siasa tulitetee Taifa letu.Ichagueni CCM Kurejesha amani na utulivu ndani ya jiji la Arusha na kufuta taswira mbaya iliyoanza kujengeka kuwa Arusha ni jiji la Vurugu na maandamano.".Mh.Mwigulu Nchemba

"Thamani ya kijana sio kiroba,kama kweli wanawathamini basi wasingekuwa wanazunguka na Helkopta angani zaidi ya Milioni 200 halafu wakishuka wanakuja kuomba miamia zenu.Huu ni upuuzi ambao manatakiwa kuukataa kwa kumchagua Bi.Edna Jonathan saul mgombea wa CCM."


"Tutawashindia hapa hapa.Wao wameshindwa kuwaheshimu wakamfukuza diwani.CCM itawapa diwani bora na kwamanufaa ya wanakimadolu na sio mtu binafsi"
 
embu acha ushamba, watu tunajadili jinsi watu wa arusha walivopata majanga unaleta habari za jinsi kampeni za CCM zilifona, hao waliojeruhiwa pengine hata kufariki si ndo wapiga kura mnaowategemea hiyo kesho? Halafu hivi nyie ni wanachama wa CCM au wasaidizi wa Mwigulu mtandaoni, maana we na nduguyo Mwampamba nado kazi yenu humu, ya kumsifia Mwigulu. kwan yeye sio memba humu jf?
 
ushindi wa kuua

Hakuna cha ushindi bali ni ukosefu wa sera ndo unaowasababisha kuwa watekaji, watesaji na wauaji wa binadamu wenzano wasio na hatia.Damu za watu waliokwisha kuuawa kisiasa zinawalilia na Mungu atajilipizia kisasi
 
Wewe ha hao wenzio hamfai kabisa kama siasa hamuwezi rudini vijijini

Juliana Shonza

wili iliyopita niliweka habari za ndani za kiinteligensia......ambayo ilikuwa ni moja ya mbinu chafu za ccm lakini mods waliiondoa ghafla. Taarifa yangu ingeokoa maisha ya watu lakini mods waliiondoa....... Niliwaambia waziwazi habari za kiinteligensia ambazo mwigulu nchemba alizisimamia.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na mkuu wa mkoa, usalama taifa wawili pamoja na makada watatu wa ccm juliana shonza na mwigulu nchemba. Jumla ilikuwa watu 8 nikiwemo. Haya mambo ilikuwa ni katika kukidhoofisha chadema katika uchaguzi unaokuja na pia kuwaogopossha mashabiki wa chadema kutokwenda kupiga kura. Tukio la leo halikujadiliwa sana, ila kikubwa ilikuwa ni kumhusisha lema na mauaji. Na kisha kumpoteza moja kwa moja

mpango ilikuwa ni kwamba, polisi wamkamate kibaka, kisha wamvalishe sare za makamanda wa uvccm. Baada ya kukamatwa akatwe katwe mapanga, damu yake na simu wapewe polisi ambao wangemfuata lema na kuyapandikiza ndani ya gari lake (yaani kwenye boot ya gari lake pindi angefuatwa) baadaye mwili wa marehemu ungetupwa barabarani eneo la kimandolu. Lengo ilikuwa ni kuwapa wananchi sababu ya kutokuichagua cdm. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo mwigulu amezisomea uchina.

Bomu lilijadiliwa lakini halikupewa kipaumbele, nashangaa ndio iliyotumika. Mtu wa kwanza kuhojiwa hapa ni mwigulu nchemba. Kati ya hawa watu nane nilikuwepo. Mkuu wa mkoa arusha naye aandike statement kuhusiana na hili tukio…..

Mods tafadhali msiondoe hi thredi.……
 
Last edited by a moderator:
Nanukuu.. "huyo diwani wenu aende halimashauri akafanye nin? Ilani inayotekelezwa ni ya CCM...". Kumbe! Kwa hiyo hata kama amechaguliwa na wananchi ambao kodi zao ndizo bajeti ya halmashauri hatakiwi!!
 
Mshauwa watu na sasa mnatuletea picha za watoto! Yani mkutano mzima mmeambulia kadi moja! Aibu...
 
Haya shonza et al.
Baada ya kazi ngumu mchana, tunawatakia pumziko jema usiku huu.
Na hii baridi .....sijui!
 
Nashngaa huyu nae anajiona kafiiika. Jana Mwingulu alikupiga kate au?
 
Mi ninachoona ulichoweka hapa ni mapenzi kati yako na Mwigulu na sio mkutano wenye mafanikio. Ungeweka tu kwenye FB page yako ingekusaidia kuliko kujichora hapa kuwa unatumia mwili kuponya njaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom