KWELI Picha hii ya wanyama wanaoonekana wakiwa mbugani imetengenezwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Salaam wana JamiiCheck

Hii picha inanipa ukakasi kuitofautisha kama imetengenezwa na Akili mnemba au ni ya kweli, wataalamu wa masuala haya naomba msaada wa kupata uhalisia wa picha hii tafadhali.

photo_2024-11-19_09-19-36.jpg

 
Tunachokijua
Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Kadri muda unavyokwenda ndivyo ambavyo teknolojia hii inaimarika kutokana na maboresho yanayofanyika kutokana na namna ambavyo watu wanatumia kulingana na mahitaji yao na ndio maana watu wanahofia juu ya siku zijazo kushindwa kutofautisha maudhui halisi na yale yaliyotengenezwa na teknolojia ya akili mnemba kutokana na kuongezeka kwa ufanisi wa utendaji wake mfano mzuri ukiwa ni maudhui ya video na picha.

Picha hii inayowaonesha wanyama mbugani inahofiwa juu ya uhalisia wake kama imetengenezwa ama ni halisi.

Je ni upi uhalisia wa picha hii?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa picha hiyo si halisi bali imetengezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba. Kifaa cha utambuzi wa maudhui ya picha yaliyotengenezwa kwa teknolojia hii kinabainisha kuwa asilimia 99 picha hiyo imetengenezwa kwa Akili Mnemba.

Aidha picha hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanathibitisha kuwa si halisi, uwepo wa tembo mdogo ambaye anaonekana kuwa na umbo la sehemu ya kichwa tu pasipo na miguu wala sehemu nyingine ya mwili, Twiga aliyepo upande wa nyuma miguu yake ya mbele upande wa juu inaonekana kuwa imeungana tofauti na twiga halisi ambao sehemu hiyo ina utengano, Tembo wawili waliopo katikati wanaonekana wameungana katika sehemu ya mgongo.

Mapungufu hayo katika picha hiyo si ya kawaida kwa wanyama kama Tembo na Twiga, hivyo kuthibitisha kuwa picha hiyo imetengenezwa.​
Hii ni picha ya kutengenezwa ( AI)

1. Mkonge wa tembo mtoto ni mrefu kupita uhalisia.

2. Ukiangalia idadi ya tembo ni 4, lakini chini ya tembo mtoto kuna kichwa cha tembo kisicho kuwa na kiwiliwili.

3. Mguu wa mbele wa pundamilia ( pundamilia wa katikati) ana mguu mwembamba zaidi kuliko mguu mwingine.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom