Nimekutana na hii taarifa nahitaji kujua kama ni kweli tukio hili limetoa Masese Uganda.
- Tunachokijua
- Tarehe 16 November 2024 Kumekuwapo na picha inayosambaa mtandaoni ikimuonesha mwanaume mmoja akiwa amefariki huku akiwa na majeraha katika paji la uso na amelala kwenye mtumbwi. Picha hiyo imeambatana na ujumbe unaosema kuwa mtu huyo ameuliwa na jeshi la UDF (Uganda Peoples’ Defence Forces) kitengo cha ulinzi wa wavuvi (Fisheries protection unit - FPU) huko Masese Jinja siku ya nyuma yake yaani tarehe 15 November 2024. Angalia hapa, na hapa.
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa picha hiyo haihusiani na taarifa inayodai kuwa ni mauji ya mvuvi wa huko Masese, Jinja. Kwa kutumia google image reverse tumebaini kuwa picha hiyo imekuepo mtandaoni tangu April 30, 2024 ikiwa imeambatana na taarifa kuwa mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Charles Wanya, mwenye miaka 46 ameuliwa na Jeshi la FPU huko Ziwa kyoga. Mathalani mtu mmoja aliyetuma picha hiyo katika mtandao wa X aliandika kuwa.
FPU today at Kitwe landing site, Agwingiri S/C murdered in cold blood Mr. Wanya Charles (46yrs), & took all his fish & nets. Why do you take a life just for fish? @GovUganda must withdraw the FPU from the lake & close that detach at Bangala in Amolatar.
Akiwa na maana kuwa, “Leo FPU huko Kitwe, Agwingiri S/C imemuua Bwana Wanya Charles (miaka 46) na kisha kuchukua samaki wake wote. Kwanini mnachukua maisha ya mtu kwa sababu ya samaki tu? @GovUganda ondoeni FPU ziwani na mfunge kizuizi kilichopo Bangala huko Amolatar”
Watu waliochapisha taarifa hiyo siku ya April, 30,2024 wamehifadhiwa hapa na hapa.
NBS Tv ya nchini uganda walichapisha taarifa kupitia mtandao wa X tarehe 1 May 2024 wakieleza kuwa Katika Wilaya ya Amolatar, kuna wito mpya wa uchunguzi wa madai ya mauaji ya Kitengo cha Ulinzi wa Uvuvi cha UPDF baada ya kupigwa risasi hivi majuzi kwa mvuvi mwenye umri wa miaka 46. Charles Wanya anadaiwa kupigwa risasi kichwani katika eneo la Kitwe.
Tovuti ya Nilepost walichapisha taarifa tarehe 1 May 2024 na kueleza kuwa siku ya Jumanne ya tarehe 30 April 2024, Wanya akiwa na rafiki yake kwenye ziwa Kyoga huko wilaya ya Amolatar kwenye mtumbwi wao waliona kundi la watu wenye silaha wakiwa kwenye mavazi ya kijeshi likiwafuata. Wanajeshi hao walipowasogelea na kutaka kuwakamata inadaiwa kuwa Wanya alikataa na kuwashambulia wanajeshi hao ambao walilazimika kufyatua risasi zilizompata Wanya kwenye paji la uso nilepost walieleza wakimnukuu msemaji wa polisi eneo la Kyoga kaskazini SP Patrick Jimmy Okema.