Picha hii inabeba taswira ya Wananchi na Viongozi wa CCM tulionao Miaka 50 ya Uhuru

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,672
2,000

Nadhani inabidi Watanzania tutoke hapa tulipo, na tujitambue, kwa maana kwamba, tuondokane na dhana ya kuitwa nchi masikini bila kutambua huu umasikini tunaotajwa ni upi. Tufike mahala tuwe SMART vichwani mwetu kama Watanzania wenye umasikini wa mali bali utajiri wa akili, japo nchi yetu ina rasilimali nyingi, ila tuangalie upande wa rasilimali watu kwanza.


Duniani, hasa kwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea, hakuna mahali kunafanyika siasa za kipumbavu kama hizi zinazofanywa na hawa watu wanaojiita CHAMA CHA Mapinduzi. Kwa kuitazama picha hii hapo, ni wazi wananchi hao hawana wakijuacho kichwani, hawana malengo yoyote katika maisha yao, ni wananchi wanaoishi kwa sababu wapo, na wala hawana tumaini lolote in the near future.

Tunataka wananchi wanaomsikiliza mwanasiasa, wanamuuliza maswali, juu ya mipango ya nyuma ambayo haijakamilika, wanamuuliza juu ya mipango mipya, utekelezaji wa ahadi, wananchi wanaopima kama ahadi wanazopewa zinatekelezeka au hazitekelezeki, wananchi waliotayari hata kuandika ahadi zinazotolewa kwa kumbukumbu ya baadae, apate kuhoji na ajue ni wapi alidanganywa, ni wapi pameshindikana, ni nini cha kufanya.

Tanzania inataka Wananchi wanaoijua KATIBA ya nchi, ubora na mapungufu yake, haki zake, na sheria zinazomhusu, kama masuala ya uchaguzi, polisi, haki za raia, haki ya kuishi, uhuru wa mawazo nk. Wananchi wanaosikiliza kwa heshima na adabu kwa kujua kwamba huyu anayezungumza hapa mbele nikimpa ridhaa kwa kura yangu atakuwa mwakilishi na kiongozi wangu katika kutatua kero zote kwa kadiri ya makubaliano.

Niseme tu: Elimu na Akili ni vitu viwili tofauti, japo vikikutana hufanya kazi kubwa sana. Kuwa na akili kwatosha, kwani sio wote duniani wanakwenda kusoma shule mpaka elimu ya juu, tena kuwa na elimu pasipokuwa na akili ni kazi bure. Ila wote twahitaji kuwa na akili ya kutambua na kupambanua jambo, na kuona mbele.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wengi wao sifa hizi hawana, kama ionekanavyo katika picha hii, wengi wanaangalia kama amekula ugali mchana, inamtosha, kesho na mwaka kesho hajui, mtu kama huyu hawezi kutambua kuwa kodi zinamuelemea, hawezi kutambua umuhimu wa katiba kwa maisha yake, yeye atasubiri kuhongwa pesa na wagombea wake, akapige kura, apewe t-shirt ya kijani, apewe kofia, anunuliwe pombe, maisha yaendelee. Mia
 

Attachments

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
4,690
2,000
sehemu kama hizi ukijidai ukawa wanadhani unataka kupindua nchi wasema mwe!
 

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,463
0
Akina CHENGE wanachota mabilioni ya ESCROW wengine wanacheza tu vigodoro vya CCM kwa kupewa miguo ya kijani tu.
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
umeandika halisi halisi ya wanachama wa ccm ni kweli tumefika mahali tunatakiwa kubadilika miaka ya 50 ya kudanganyana imefikia tamati sasa hatuwezi kukubali watu wachache wachezea rasimali zetu wizi sekta zote kumeoza bado viongozi wanaendelea kutuibia kama hizi pesa escrow mpaka sasa raisi yupo kimya hakuna hatua yeyote aliyochukua kwa ufupi ndani ya ccm hakuna aliye wote ni mafisadi na wezi wakubwa wa rsaimali zetu .Mungu saidie opesheni FUTA DELETE CCM NCHI NZIMA iwe ya mafanikio tumeshachoka
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,910
2,000
Akina CHENGE wanachota mabilioni ya ESCROW wengine wanacheza tu vigodoro vya CCM kwa kupewa miguo ya kijani tu.
inasikitisha sana unamkuta mtu mzima na akili zake timamu anaisifia ccm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom