Picha: Heche ang'aka Makete matumizi ya gari za serikali katika kampeni za CCM

huna hoja wewe kaa chini.
weka wewe hoja maana tunajua nyie magamba zenu udini tu kutaka sisi na wakristu tusielewane ili nyie muishi mpate mtaji wa kutunyonya
vipi kaka LAKE OIL HUJAPATA BADO PA KUJISHIKISHA WEWE MAANA NAWE MJUZI WA UDAKU
 
Hii tabia ni kawaida katika wilaya hizi zilizo mbali na wakosoaji. Nilitaka kuanzisha uzi kulingana na taarifa niliyoipata. Ccm wamekuwa wakijaziwa mafuta na halmashauri ya wilaya kwa shughuli zao zote wanazozifanya. Hata kwenye hizi kampeni licha ya kwenda na magari hayo yote gari lao hujazwa mafuta kwa hela zetu za kodi. Hii inatokana na viongozi wa halmashauri kuwa wabadhirifu wa mali za umma hivyo kuishia kujipendekeza. Kuna miradi mingi ambayo dili zake hupigwa bila kupata wataalamu wa kufanya kazi hizo hasa miradi ya barabara. Kila mwaka wanachofanya ni kuhamisha vumbi kutoka pembeni mwa barabara na kuzijaza barabarani. Likipita gari au kukiwa na upepo hata unga huwezi kuanika. Mtanyaji wangu kaniambia hata kwenye safari binafsi za viongozi wa ccm gari lao hutumia mafuta kwa fedha za halmashauri. Kweli tutafika?

KAka ni ni tufanye mbona haki inaporwa saana nchi hii tena kwa kasi saana ni namna gani tufanye?
 
umenena vema mkuu...chama kinahitaji watu kama hawa ili kiendelee........
wengine wanafurahia kuvuruga chama.Napenda sana Heche the way anvyofanya kwa kweli kwa upande wa BAVICHA chama kilipata mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kwa kweli tunahitaji vijana wenye moyo huu wakati wote.
 
Heche mwenyewe ni mzigo atamng'akia nani?hana mpya huyo asubiri 2015 akagaragazwe tarime na nyambari nyangwine
mbona wewe unaiga ID za watu humu vipi mkuu?

tatizo la hii wilaya inadhani bado kuna chama kimoja tu cha siasa Waulize kilicho tokea Tunduma kwa kutumia magari ya serikali kwenye shughuri za chama
 
Heche mwenyewe ni mzigo atamng'akia nani?hana mpya huyo asubiri 2015 akagaragazwe tarime na nyambari nyangwine

Aise, kweli CCM mnafikiria kwa kutumia MASABURI yaani NYAMBARI ambaye hajui hata kujenga hoja amshinde heche? hajawahi kuchangia mchango wowote wa maana akiwa mbungen aise kweli u cant see your weakness , kwa taarifa ukickia heche kachukua form jua ni MBUGE moja kwa moja
 
Nadhani sisi wote ni watu wazima hakuna watoto mleta mada ebu nipe ushahidi kuwa hizo gari zimetumika kwenye mkutano wa CCM.

Pro-Chadema JF msiwe kama mamba mnameza kila kitu mnaletewa picha mdanadanganywa kama watoto wadogo mlivyokuwa na upofu na Chadema mnashindwa hata kuhoji.
 
Tabia ya ccm kutumia magari na rasilimali za serikali ni kawaida sana.kiufupi ccm wanaamini nchi ni yao. Mabadiliko ni muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa letu!
 
Wakati TANZANIA ikiwa katika miaka zaidi 20 ya kupractise siasa za vyama vingi tangu mwaka 1992 imeendelea kuonekana dhamira ya srikali ya CCM ni kuidhofisha serikali kila inapobidi ili mradi kuimarisha chama cha mapinduzi bila kujali hasara zinazowakumba walipa kodi hayo yamesemwa na mwenyekiti wa vijana CHADEMA TAIFA bwana JOHN HECHE SUGUTA alipokuwa akizungumza na wanachi,wa kijiji cha ISILILO, kata ya LUWUMBU wilaya ya MAKETE baada ya kukutana na magari zaidi ya matano yenye namba za STK, DFP, (kama yanaavyoonekana katika picha) yakiwa katika kampeni za CCM 'katika hili ndugu zangu itabidi mkurugenzi atueleze ni waraka namba ngapi, wa SERIKALI unaelekeza gari za serikali kufunga bendera za CHAMA CHA MAPINDUZI NA KUFANYA KAZI HIZI ZOTE!!?
kwa bajeti ipi?
la sivyo sisi kama wapigania mabadiliko hili nalo litakuwa swala la kufanyia kazi na sasa naenda kwa mkurugenzi kwa nia njema saana ya kiutaratibu nikiamini kuwa sio kwamba hajui analofanya ila nataka nijiridhishe kuwa anatumiwa na anatumiwa na nani nianze nao hatua kwa hatua 'ALISEMA HECHE KWA HISIA KALI' hatuwezi kuvumilia maswala kama haya kama CCM hawajatosheka kututumia tutawasaidia kujua kuwa tumechoka kutumiwa kwa haraka zaidi kwa mtindo wa peoples power

NOTE
Ikumbukwe kwamba ni juzi tu MH MAGUFULI ALIONYA MATUMIZI MABAYA YA MAGARI YA SERIKALI JE YUKO TAYARI KUPOKEA USHAHIDI HUU WA BWANA HECHE NA KUANZA NA HAWA WA MAKETE?

nakala View attachment 69096View attachment 69098View attachment 69099View attachment 69100View attachment 69101

Kama ni ushahidi kuwa yamewekewa bendera za ccm sijaiona hata moja kwenye gari hizo. labda kama kuna ushahidi mwingine strong, lakini wa bendera, hakuna picha inayoonyesha bendera
 
ccm,ccm,ccm shikwa pataamuu.
ongoza ujambazi,rushwa njenje aaa aaaaaaaaaa ccm shikwa pataamuuu.:majani7:
 
Wakati TANZANIA ikiwa katika miaka zaidi 20 ya kupractise siasa za vyama vingi tangu mwaka 1992 imeendelea kuonekana dhamira ya srikali ya CCM ni kuidhofisha serikali kila inapobidi ili mradi kuimarisha chama cha mapinduzi bila kujali hasara zinazowakumba walipa kodi hayo yamesemwa na mwenyekiti wa vijana CHADEMA TAIFA bwana JOHN HECHE SUGUTA alipokuwa akizungumza na wanachi,wa kijiji cha ISILILO, kata ya LUWUMBU wilaya ya MAKETE baada ya kukutana na magari zaidi ya matano yenye namba za STK, DFP, (kama yanaavyoonekana katika picha) yakiwa katika kampeni za CCM 'katika hili ndugu zangu itabidi mkurugenzi atueleze ni waraka namba ngapi, wa SERIKALI unaelekeza gari za serikali kufunga bendera za CHAMA CHA MAPINDUZI NA KUFANYA KAZI HIZI ZOTE!!?
kwa bajeti ipi?
la sivyo sisi kama wapigania mabadiliko hili nalo litakuwa swala la kufanyia kazi na sasa naenda kwa mkurugenzi kwa nia njema saana ya kiutaratibu nikiamini kuwa sio kwamba hajui analofanya ila nataka nijiridhishe kuwa anatumiwa na anatumiwa na nani nianze nao hatua kwa hatua 'ALISEMA HECHE KWA HISIA KALI' hatuwezi kuvumilia maswala kama haya kama CCM hawajatosheka kututumia tutawasaidia kujua kuwa tumechoka kutumiwa kwa haraka zaidi kwa mtindo wa peoples power

NOTE
Ikumbukwe kwamba ni juzi tu MH MAGUFULI ALIONYA MATUMIZI MABAYA YA MAGARI YA SERIKALI JE YUKO TAYARI KUPOKEA USHAHIDI HUU WA BWANA HECHE NA KUANZA NA HAWA WA MAKETE?

nakala View attachment 69096View attachment 69098View attachment 69099View attachment 69100View attachment 69101
Kwa bahati mbaya sana Heche anazidi kunidhihirishia kuwa ni kweli ana pupa,mie ni shabiki wako lakini nataka kukushauri kuwa uwe unafikiri mbali na kufanya utafiti kabla ya kulaumu!Mimi ni mpambanaji kama ww mwenzangu lakini mambo mengine haya hayana ukweli!Hayo magari hayakuwa kwenye kampeni za CCM bali waliokuwa humo kwenye magari ni wajumbe wa kamati ya mipango na fedha wa Halmashauri (w) Makete wakikagua shughuli za maendeleo!Hawakwenda LUWUMBU tu bali MATAMBA na kwingineko!Hatukwepi ukweli kuwa madiwani wote wa wilaya ya makete ni wa CCM,na ukweli kuwa kuna kazi ngumu sana kwa cdm kuweza kupata kura za kutosha kwa udiwani wa kata hii kwani wananchi hawana uelewa kabisa!Kibaya zaidi ni kuwa mgombea wa CDM hayuko amejaa mizaha,utakumbuka Km siku tano zilizopita alikutwa kalewa chakari wakati anatakiwa kwenda kuhutubia mkutano!Mie ni shahidi wa haya kwani naishi nao huku lakini hii iwe ni changamoto kuwaamsha wananchi wajue nini kinaendelea nchi hii!Wananchi wa kule ni waaminifu kwa chama chao CCM kiasi kwamba ukihama wanakutenga na kijiji!Hali ni mbaya hiyo jana kwenye mkutano ambao ulifanyiaka Usililo kijiji anachotoka mgombe udiwani wa kata ya Luwumbu idadi ya wasikilizaji wa kampeni ya CDM haikuzidi watu kumi mpk wakati mie napita!Anywau hii ndo hali halisi na Heche ni shahidi wa haya!Lakini sio kweli kuwa Hayo magari yalikuwa kwenye kampeni,Nakushauri heche maadam una gari ya M4C sogea mbele kidogo utaona shughuli iliyowapeleka wajumbe wa kamati hiyo ya mipango na fedha (w)!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom