Picha: Heche ang'aka Makete matumizi ya gari za serikali katika kampeni za CCM

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Wakati TANZANIA ikiwa katika miaka zaidi 20 ya kupractise siasa za vyama vingi tangu mwaka 1992 imeendelea kuonekana dhamira ya srikali ya CCM ni kuidhofisha serikali kila inapobidi ili mradi kuimarisha chama cha mapinduzi bila kujali hasara zinazowakumba walipa kodi hayo yamesemwa na mwenyekiti wa vijana CHADEMA TAIFA bwana JOHN HECHE SUGUTA alipokuwa akizungumza na wanachi,wa kijiji cha ISILILO, kata ya LUWUMBU wilaya ya MAKETE baada ya kukutana na magari zaidi ya matano yenye namba za STK, DFP, (kama yanaavyoonekana katika picha) yakiwa katika kampeni za CCM 'katika hili ndugu zangu itabidi mkurugenzi atueleze ni waraka namba ngapi, wa SERIKALI unaelekeza gari za serikali kufunga bendera za CHAMA CHA MAPINDUZI NA KUFANYA KAZI HIZI ZOTE!!?
kwa bajeti ipi?
la sivyo sisi kama wapigania mabadiliko hili nalo litakuwa swala la kufanyia kazi na sasa naenda kwa mkurugenzi kwa nia njema saana ya kiutaratibu nikiamini kuwa sio kwamba hajui analofanya ila nataka nijiridhishe kuwa anatumiwa na anatumiwa na nani nianze nao hatua kwa hatua 'ALISEMA HECHE KWA HISIA KALI' hatuwezi kuvumilia maswala kama haya kama CCM hawajatosheka kututumia tutawasaidia kujua kuwa tumechoka kutumiwa kwa haraka zaidi kwa mtindo wa peoples power

NOTE
Ikumbukwe kwamba ni juzi tu MH MAGUFULI ALIONYA MATUMIZI MABAYA YA MAGARI YA SERIKALI JE YUKO TAYARI KUPOKEA USHAHIDI HUU WA BWANA HECHE NA KUANZA NA HAWA WA MAKETE?

nakala View attachment 69096View attachment 69098View attachment 69099View attachment 69100View attachment 69101
 
Hapa sasa ni kuomba Mungu kisulisuli cha M4C kifanikiwe 2015, hizi picha na tarehe zihifadhiwe.
 
Magufuri mwenyewe shida tupu, alienda Igunga akawatisha wananchi ili wamchague Kafumu matokeo yake Mahakama ikatengua matokeo ya uchaguzi. Hapa tatizo ni ccm, hakyanani tukiiondoa ccm madarakani hii nchi ndo itatengemaa. Bila kuiondoa ccm madarakani hii nchi itaendelea kuwa na uozo wa kutisha.
 
Walivyokuwa washenzi, watakwambia yalikuwa kwenye miradi vijijini.
 
kwa nini mkuu? tunambiwa anatumia FORD RANGE ILA INASEMEKANA YUKO FASTA SAANA AKIPIGA KIKAO NA WANACHAMA ZAKE NI UTAFITI NA MIKUTANO TU
Aisee,mkuu anastahili pongezi sana maana jana alikuwa Vwawa Mbozi,Leo makete na nijuavyo safari ya Vwawa to makete simchezo na ni majuzi tu alikuwa Rukwa,kwa kweli anstahili pongezi za dhati.
Naamini Mungu akimjalie afya njema atafika mpaka Tamota kule Bumbuli-Tanga kwenda kukutana na makamanda na wapambanaji wa kule akina Amir Sheshe na Mbelwa kama sikosei.kazi nzuri ahsante kwa updates kamanda!
 
Heche mwenyewe ni mzigo atamng'akia nani?hana mpya huyo asubiri 2015 akagaragazwe tarime na nyambari nyangwine
 
sasa jamani ndio kusema kuwa kuna haja ya ccm yenye magari aina hii hii tunayoiona aina ya 1HZ tena kila wilaya wameshindwa kuyatumia kwa kazi zao wanachukua mpaka DFP kwa maswala binafsi tena bila hata sababu za msingi na kwa staili hii mbona wanachochea migogoro na mlipuko usiokuwa na msingi
 
huna hoja wewe kaa chini.
 
Heche mwenyewe ni mzigo atamng'akia nani?hana mpya huyo asubiri 2015 akagaragazwe tarime na nyambari nyangwine
ni mzigo uliotoka wapi maana mizigo na hawa mchwa wa kijani ambao lowassa akisema kaa wanakaa inuka wanainuka chuchumaa wanatii wamo humu kwa sababu hata chuo walipigiwa chapuo, wana komputa sababu wana msaada wa ccm wanaishi kwa simu za mjinga na kwa sifa hizi hawana uwezo wa kuikosoa serikali hata inapokosea na kwa namna hiyo hata wabunge mambumbumbu aina ya nyambari wa tarime kwao ni lulu na naamini wewe ni miongoni mwao
 
Hii tabia ni kawaida katika wilaya hizi zilizo mbali na wakosoaji. Nilitaka kuanzisha uzi kulingana na taarifa niliyoipata. Ccm wamekuwa wakijaziwa mafuta na halmashauri ya wilaya kwa shughuli zao zote wanazozifanya. Hata kwenye hizi kampeni licha ya kwenda na magari hayo yote gari lao hujazwa mafuta kwa hela zetu za kodi. Hii inatokana na viongozi wa halmashauri kuwa wabadhirifu wa mali za umma hivyo kuishia kujipendekeza. Kuna miradi mingi ambayo dili zake hupigwa bila kupata wataalamu wa kufanya kazi hizo hasa miradi ya barabara. Kila mwaka wanachofanya ni kuhamisha vumbi kutoka pembeni mwa barabara na kuzijaza barabarani. Likipita gari au kukiwa na upepo hata unga huwezi kuanika. Mtanyaji wangu kaniambia hata kwenye safari binafsi za viongozi wa ccm gari lao hutumia mafuta kwa fedha za halmashauri. Kweli tutafika?
 
Aisee,mkuu anastahili pongezi sana maana jana alikuwa Vwawa Mbozi,Leo makete na nijuavyo safari ya Vwawa to makete simchezo na ni majuzi tu alikuwa Rukwa,kwa kweli anstahili pongezi za dhati.
Naamini Mungu akimjalie afya njema atafika mpaka Tamota kule Bumbuli-Tanga kwenda kukutana na makamanda na wapambanaji wa kule akina Amir Sheshe na Mbelwa kama sikosei.kazi nzuri ahsante kwa updates kamanda!
umenena vema mkuu...chama kinahitaji watu kama hawa ili kiendelee........
 
Back
Top Bottom