Picha: Hali ya Uchaguzi mdogo Kiboriloni ilivyokuwa hadi CHADEMA wanachomoza na Ushindi

Dec 21, 2011
71
75
DSCF0003.JPG DSCF9986.JPG DSCF9990.JPG DSCF0031.JPG DSCF0039.JPG DSCF0011.JPG DSCF0012.JPG DSCF0013.JPG DSCF0014.JPG DSCF0006.JPG

Msimamizi wa Uchaguzi mkuugenzi wa manispaa ya Moshi,Shabani Ntarambe amemtangaza Frank Kagoma (Chadema)kuwa diwani wa kata ya Kiboriloni baada ya kupata kura 1019.amewashinda Willy Tuli wa CCM aliyepata kura 255 na Aidan Mzava wa UDP aliyepata kura 2,Jumla ya kura 1288 zimepigwa katika vituo 14.

Matukio zoezi la uchaguzi kata ya Kiboriloni.
Kituo cha KDC.
Katika kituo cha KDC zoezi la upigaji kura uliendelea kwa usalama huku ikishuhudiwa idadi ya wananchi waliojitikeza kwa ajili ya upigaji kura iki pungua kadri muda ulivyokuwa ukiendelea na baadae iliongezeka mara baada ya watu kutoka makanisani.

Hata hivyo wafuasi wa Chadema na CCM nusura wa zichape baada kikosi cha usalama cha Chadema,Red Brigade kushtukia mchezo mchafu wa kutoa rushwa kwa wapiga kura unaodaiwa kufanywa na viongozi wa vijana wa CCM.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 5:30 katika barabara ya KDC jirani na Ikulu ndogo ambapo wanaodaiwa kuwa ni wanaccm walikuwa wakiwavizia wananchi wanao ishi maeneo hayo na kisha kuwaingiza katika moja ya nyumba iliyoko jirani na kupatiwa kiasi cha fedha kabla ya kuruhusiwa kwenda kupiga kura katika kituo cha KDC.

Kutokana na hali hiyo kikosi cha Red Brigade kililazimika kuweka kambi katika eneo hilo ndipo ilipozuka hali kurushiana maneno na matusi kati ya wafuasi hao nusura ya kukunjana mashati kabla ya kusuruhishwa na viongozi wao.
Kituo cha sokoni.

Zoezi la upigaji kura lilifanyika kwa amani isipokuwa kulitokea hali ya sintofahamu baada ya moja kati ya maduka ya Nyama yaliyopo jirani kabisa na kituo cha kupigia kura lilifahamika kama Rafiki Butcher kudaiwa kugawa Nyama kwa wananchi walifika katika duka hilo.

Madai hayo yaliibuliwa muda mfupi baada ya baadhi ya viongozi wa CCM kufika katika duka hilo na kuanza kuwashambulia kwa maneno wauzaji hao huku wakitoa amri ya kutaka kufungwa kwa duka hilo kwa madai ya kuwa lilikuwa likitumika kushawishi wapiga kura kwa kuwagawia Nyama.

Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Michael Mwita alisikika akimuamuru mwenyekiti wa CCM kata ya Kiboriloni kumuondoa mara moja muuzaji wa Nyama katika duka hilo kutokana na kwamba Jengo lenye maduka hayo linamilikiwa na CCM.

Kutokana na hali hiyo askari waliokuwepo katika eneo hilo pamoja na maofisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa walilazimika kufanya uchunguzi wa kimya kimya ili kujiridhisha na tuhuma zilizotolewa katika duka hilo.
Katika kituo cha shule ya Msingi Kiboriloni.

Hali ya vurugu ilitokea katika shule ya msingi Kiboroloni baada ya mkuu wa polisi wilaya ya Moshi (OCD) Kasindo kutaka kuwatawanya wapiga kura na baadhi ya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa zaidi ya mita 100.

Kutokana na hali hiyo zaidi ya wafuasi 10 walizolewa na kupelekwa kituo cha polisi cha kati ambao baadae waliachiwa huru baada ya viongozi wa Chadema mkoa na wilaya kufika kituo ni hapo .
 
watuachie moshi yetu, ndio zito alitaka kufanya mkutano na vi dvd vyake???????????
 
Nikitazama picha hizi, na hasa jinsi polisi walivyovaa inaonyesha chaguzi za Tanzania sio mahali salama. Serikali inategemea kuwa lazima vurugu zitazuka, ndio maana wanawaandaa polisi hivyo.
Mahali ambako CDM inahisiwa kushinda basi Polisi humwagwa kwa wingi ili 'kudhibiti vurugu' zinazoweza kutokea.
Najiuliza kwa nini tumefikishwa hapo, hali sisi tunajidai ni nchi ya amani? Serikali haijiulizi ni kwa nini wapenda amani hawa wanawachagua 'wapenda vurugu' huku wakilindwa na watu waliotayari wakati wowote 'kuzuia vurugu'?
Ni matumaini yangu kuwa 'vurugu' hizi tutazishuhudia sehemu mbalimbali nchini mwakani (kama tulivyoona Njombe). Je serikali imejiandaaje 'kudhibiti vurugu' tarajiwa nchini? Inao askari wa kutosha? Inayo magari ya maji ya kuwasha kila kituo cha kupigia kura? Lets wait and see.
 
Back
Top Bottom