mchongameno
Member
- Feb 9, 2012
- 26
- 16
Kwa kweli tukio kama hili halijawahi kutokea tangu tunapata Uhuru. Ni tukio la kihistoria ambalo kamwe halitasahaulika. Jambo la kushangaza Watawala hawana hata wasiwasi. Hivi tunaelekea wapi Watanzania? Serikali Kuu chini ya Rais na mawaziri hawazungumzi lolote. Bunge hali kadhalika hawataki hata lijadiliwe. Tukumbuke hao wabunge ndio tumewchagua hili watuwakilishe. Je Wananchi watakuwa na Imani na Serikali, Wabunge na atendaji wengine wa Serikali? Je kama nchi itaingia kwenye machafuko Viongozi wa Serikali wana la kujitetea? Je taasisi muhimu kama iIDARA YA USALAMA WA TAIFA kuna mnachomshauri Rais? Au mpo kwa ajili ya kuwadhibiti wapinzani tu kwenye chaguzi mbalimbali? Maana nasindwa kuelewa Nini maan ya IDARA YA USALAMA WA TAIFA. Ipo kwa ajili ya kulinda Uslama wa nani? Je hili haliwezi kusababisha Usalama wa nchi ukapotea? Basi kama hakuna majibu mazuri kwenye hili ni bora Idara hiyo Isiwepo kabisa. Nina hakika ujumbe huu mtaupata na kuufanyia kazi. Siku zote yanapotokea masuala kama haya mnasingizia Wapinzani ndio wachochezi? Je hili nalo mnalizungumziaje wamehusika? Ninyi kama Serikali mmeshachukua hatua gani tangu mgomo uanze takribani wiki tatu sasa?