PICHA & HABARI: Sheikh ISSA PONDA na Watu Wengine 49 Mahakamani Kisutu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA & HABARI: Sheikh ISSA PONDA na Watu Wengine 49 Mahakamani Kisutu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 18, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  SHEIKH ISSA PONDA NA WATU WENGINE 50 WAPANDISHA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU LEO

  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda, leo amepanda kizimbani na watu wengine 50 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwashawishi baadhi ya Waislamu kuvamia Kiwanja katika eneo la Chang'ombe jijini Dar es Salaam, kuwashawishi Waislamu kutojitokeza katika zoezi la Uandikishaji katika Sensa ya Watu na Makazi.

  [​IMG]
  Karandiga lililowabeba Sheikh Issa Ponda na wenzake
  [​IMG]
  Wanahabari wakiwa kazini
  [​IMG]
  Wanahabari wakirekodi kuwasili kwa Sheik Issa Ponda Mahakamani Kisutu leo
  [​IMG]
  Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda, na watu wengine 50 wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka mbalimbali
  [​IMG]


  [​IMG]
  Mmoja wa washtakiwa akitelemshwa kutoka kwenye karandinga

  Katibu wa baraza la Waislam Tanzania Shekhe Issa Ponda amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa mashitaka matano.


  Alifikishwa mahakamani hapo na kupoandishwa kizimbani na watu wengine 49 akiwemo bibi wa miaka 100 kwa msafara wa magari ya polisi na ving'ora likiwemo gari la maji ya machozi kwa kasi ya ajabu na kushushwa haraka. Hata hivyo baada ya kukana mashitaka yao walirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.

  Ponda, aliyewasili peke yake, alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahakama na kuunganishwa na washitakiwa wenzake. Wote walisomewa mashitaka hayo mbele ya hakimu Stewart Sanga na wakili wa serikali Jumanne Kweka.

  Wote kwa pamoja walidaiwa kula njama, na katika maelezo ya kosa walidaiwa Oktoba 12, mwaka huu katika eneo la Chang'ombe Markasi katika Wilaya ya Temeke jjijni Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa.

  Shitaka jingine wanadaiwa wote kwa pamoja kuingia kwa nguvu kutaka kufanya makosa, huko huko Chang'ombe kwa jinai na bila sababu za msingi walivamia Ardhi katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali

  Shitaka la tatu walidaiwa kujimilikisha kwa nguvu, maelezo ya kosa walidaiwa wote kwa pamoja walivamia kiwanja hicho pasipo kuwa na uhalali na katika hali ya uvunjifu wa amani, walijimilikisha mali hiyo ambayo ni mali halali ya kampuni ya Agritanza

  Aidha katika shitaka la nne ambalo ni la wizi kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, washitakiwa waliiba vifaa vya ujenzi walivyovikuta katika kiwanja hicho vyenye thamani ya shilingi 59,650,000 ambavyo ni kokoto, nondo na saruji mali ya kampuni ya Agritanza.


  Shekhe Ponda peke yake ameshtakiwa kuchochea kwa nia ya kuhamasisha utendaji kosa katika maeneo tofauti kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, kama katibu wa baraza la Waislam Tanzania, huko Temeke eneo la Chang'ombe, jijini Dar es salaam.

  Washtakiwa wote walikana mashtaka hata hivyo walirudi rumande kwa sababu hakimu aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo hakuwepo na hivyo kusomwa mbele ya hakimu Sanga ambaye alisema hana mamlaka.

  Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana ya Shekhe Ponda kwa kile alichotaja kuwa ni kwa usalama wa Ponda na pia kwa maslahi ya Jamhuri. Kesi hiyo itatajwa Novemba mosi mwaka huu na kwamba upelelezi haujaamilika.

  Pamoja na jitihada za wakili wao Juma Nasoro kuwaombea dhamana wateja wake lakini jitahada hizo ziligonga mwamba.

  Msafara wa zaidi ya magari kumi uliondoka na washitakiwa hao huku likiwemo gari lile la maji ya machozi maaskari wa barabarani, askari magereza na fidifosi huku Ponda akiwekwa katika gari la vioo vya giza kama alivyoletwa.


  THURSDAY, OCTOBER 18, 2012 - MICHUZI BLOG
   
 2. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,182
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Huyu mungu huyu
   
 3. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 888
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru Mkuu kwa taarifa detailed
   
 4. Kocha

  Kocha JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 2, 2008
  Messages: 375
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ujinga ni kitu hatari sana,huyu Ponda na kundi lake ujinga ndio unawasumbua,sasa kuna hatari ya vita ya kidini TZ halafu nasikia tetesi kwamba JK kaenda kuandaa hifadhi OMAN ili mambo yatakapo haribika yeye akimbilie OMAN
   
 5. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,736
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ngoja akaolewe na Manyapara huko.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,718
  Likes Received: 21,804
  Trophy Points: 280
  hiii 'movie' ni very funny...

  baadhi ya wakristo wanapata hofu kuubwa

  while majority ya waislam hawana hata habari....

  kiwaambia watu hii haitakuwa news after two weeks..hawataamini...

  everything is just ridiculous ...lol
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  A shred of sanity and truth. A positive and spiritual message, bringing people together rather than preaching separatism, if ones spiritual beliefs are practiced properly, violence and this need to be the only one that has the truth or the correct way, should never be a part of it. That goes for all systems of belief.

  FUNDAMENTALISM is dangerous whether Christian or Muslim....

  RELIGION = HIGH EGOES + HYPOCRISY.
   
 8. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa mzito sana kuchangia thread za vurugu za waislam. Lakini nimeona niseme tu kwamba sikubaliani na njia wanazotumia masheikh wetu hawa katika kufanikisha wanachoamini. Sheikh Ponda angeweza kutumia njia halali kuhamasisha wenzie kuipinga bakwata. Anazifahamu ila amechagua njia haramu. Sheikh Farid nae angeweza kabisa kuupinga muungano kwa kuhamasisha wenzie kwa njia halali na kwakweli tunaoupinga muungano tungemuunga mkono. Ila nae amechagua njia haramu. Wameachwa kwa muda mrefu sana lakini sasa uvumilivu umefika kikomo. Sintawasapoti sio kwa uislam wao wala mtazamo wao, ila kwa njia zao. Na sasa natamani wakae ndani maana sitaki hata kuwasikia tena. Hakuna tena zuri kutoka kwao maana haramu huzaa haramu!
   
 9. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,153
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Shehe ponda na hao wafuasi wake, wote wapumbavu
   
 10. Root

  Root JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 24,240
  Likes Received: 10,433
  Trophy Points: 280
  Dah hadi tarehe 1 heheh atajuta aiseee serikali imemuweza

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kumbe makosa yenyewe ndio haya? mimi nilidhani Sheikh Ponda amehusika na vurugu za Mbagala kumbe maswala ya Kiwanja.. jamani kiwanja kile ni cha waislaam na Sheikh Mkuu aliingia deal na kukiuza kinyume cha waislaam wenyewe kujua..
  Sheikh Mkuu Simba amekuwa akiuza mali za Waislaam kwa kujinufaisha yeye hivyo hawa vijana wamefanya kweli makosa kuvamia eneo ambalo tayari limeisha uzwa lakini pia nani anayempa mamlaka Shiekh Mkuu huyu wa Bakwata kuuza mali za Waislaam? Hili ni tatizo la Waislaa wenyewe hivyo tunashangilia kipi haswa....
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,063
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Duh!Anyways,siwezi kushangazwa na hilo,haiwezekani kabisa awepo huko Oman na nchi ipo kwenye matatizo makubwa kama hayo,rais yeyote yule anayejali taifa lake,basi angesitisha safari hiyo.Lisemwalo lipo.
   
 13. mgweno1

  mgweno1 New Member

  #13
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we ndio mzembe kweli!umeacha kuongelea ya ponda unamvamia jk amekosea nini?
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,133
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 160
  Point noted!

   
 15. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 7,447
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  Kwangu Ponda is just another kind of Patient who tries his best to dent others psyche to create people of his kind to look a like.
  I urge the authorities to either treat him as a patient or a terror, this kind of treatment will be a good message to the followers of him.
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,718
  Likes Received: 21,804
  Trophy Points: 280
  noted?
  umeelewa?
  au ume assume umeelewa?
   
 17. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  lazima bodi ya wadhamini ilikubali otherwise yeye kama shekh mkuu haneweza kuuza. hao jamaa hawaitaki bakwata mpango ndiyo huo. by the way achane ubinafsi eti ni mali ya waislam , kwani mlichanga hela kununua hicho kiwanja? kama sivyo kwanini kinapouzwa muulize?
   
 18. J

  John the babtist Member

  #18
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nasubiri kesho nione busara au ujinga wao
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 18, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu ikiwa huelewi kitu uliza kwanza ufahamishwe na sii kurukia vitu tu ili mradi unafikiri unaelewa kumbe hujui kitu. Hiyo bodi ya wadhamini ni kina nani kama unawajua..Hao hao wajumbe wa Bakwata yenyewe ambayo waislaam hawaitaki isipokuwa kwa kulazimishwa na serikali. Nambie mjumbe yeyote wa baraza (Board) hilo ambaye sio mwana CCM kwanza? sasa inakuwaje viongozi wa dini ni makada wa chama cha siasa kama sii kuwadhalilisha waislaam.

  Wanamuonea Sheikh Ponda kama walivyoweza kuwazima kina Sheikh Kassim na nilijua mapema kukamatwa kwa Sheikh Ponda kunahusiana tu na maswala ya Bakwata na sio madai ya watu hapa JF.. Unaweza sana kumchukia Sheikh Ponda na pengine analeta vurugu nchini lakini binafsi yangu yeye na Dr. Slaa ni wakombozi wangu wa kweli.
   
 20. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu hata mimi sasa naanza kuelewa vyema, mwanzoni sikumuelewa ponda anagombana kwanini na huyo shekhe mkuu,
  hili tatizo wasilipo litatua vyema bado lita kuja kulipuka baadae.
   
Loading...