PICHA & HABARI; Jinsi CHADEMA walivyoiteka Makambako jana!!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Wananchi wa Mkambako wakionyesha vidole viwili kama ishara ya kukikubali Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)


Mh. Alatanga Nyagawa akiimbisha wimbo anaouita wimbo wa jimbo(Asiyependa shule ni mjinga kabisa) ambapo wananchi waliitikia kwa kishindo.




Mkutano wa CHADEMA uliofanyika jana Makambako katika viwanja vya polisi uliteka hisia za mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo hasa kutokana na yale yaliyozungumzwa na viongozi tofauti tofauti wa chama hicho. Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Mh. Silinde mbunge wa Mbozi, Mh. Joseph Mbilinyi almaarufu kama Sugu, Mch. Msigwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini, Mh. Thomas Nyimbo, Mh. Alatanga Nyagawa na viongozi wengineo wa chama katika ngazi ya wilaya.


Wakiongea kwa nyakati tofauti tofauti viongozi hao pamoja na mambo mengine walisisitiza umuhimu wa wananchi wa Makambako kufanya mabadiliko katika chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kwa kuwachagua viongozi wa CHADEMA kwa sababu ndio viongozi makini na wenye kutetea maslahi ya umma na si maslahi ya wachache kama wafanyavyo CCM. Jambo hili lilisisitizwa zaidi na Mh. Silinde na pia Sugu ambao walikili kusikitishwa na mwenendo wa CCM wakidai kwamba chama hicho hakifai kuendelea kupewa nafasi ya kuiongoza nchi kwani kimeonyesha mapungufu makubwa kwa kushindwa kuleta maendeleo katika nchi na kuwaacha wananchi wakiwa maskini wa kutupwa.


Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Njombe akiwasalimia wananchi wa Makambako kwa ishara ya vidole viwili.

Mh. Silinde anayejiita sauti ya simba akizungumza na wananchi


Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Rais wa Mbeya akikaribishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Mh. Thomas Nyimbo.


Mh. Mbilinyi naye akiunguruma ndani ya viwanja vya polisi


Naye Mch. Msigwa hakuwa tofauti sana na wenzake kwani pamoja na mambo mengine yeye alijaribu kutofautisha umakini wa wabunge wa CCM na wale wa CHADEMA wawapo bungeni kwamba iko wazi kwamba wabunge wa CHADEMA huwa makini kwa kila jambo walifanyalo nje na ndani ya bunge. Pia alisisitiza umuhimu wa wananchi hasa wa Makambako kuhakikisha kwamba wanajivua gamba kwa kuhamia chama makini cha CHADEMA na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa chama kwa kujitolea kwa hali na mali pasipo kusubiri misaada. Kwa kudhihirisha hilo kwa vitendo aliwaomba muda huo huo wananchi wakichangie chama kiasi chochote cha fedha walichokuwa nacho mifukoni ambapo wananchi walichangia kwa moyo mmoja na kupata kiasi kikubwa cha fedha cha zaidi ya shilingi 1,500,000/= kwa muda mfupi.




Mch. Msigwa akizungumza na wananchi wa Makambako kwenye mkutano.


Mch. Msigwa akipokea fedha kutoka kwa wananchi wa Makambako za kusaidia kuendesha chama


Boks likipitishwa kwenye umati wa watu mkutanoni kuchangia fedha za kuendeshea chama


Mch. Msigwa bado anaendelea kupokea chapaa

Wakitoa ushauri kwa wananchi wa Makambako, viongozi hawa wamesisitiza kwamba makosa yaliyofanywa awali kwa kumchagua Mbunge wa sasa Deo Sanga asiye na elimu yasirudiwe tena bali wamchague Mbunge wa CHADEMA pasipo kuangalia umaskini wake bali umakini katika kusimamia na kufuatilia shughuli za kimaendeleo.


Mh. Thomas Nyimbo ndiye aliyekomelea msumari wa mwisho kwa kuwataka wananchi waachane na ubabaishaji wa CCM na kujiunga CHADEMA ambapo licha ya kuzungumza mambo mengi lakini pia alikaribisha wale wote waliokuwa tayari kurudisha kadi za CCM kwake wakazipeleke jambo ambalo liliitikiwa na wananchi wengi waliopita mbele na kukabidhi kadi hizo. Akikazia zaidi aliwaambia kwamba yeyote anayebaki na kadi ya CCM nyumbani kwake hiyo ni laana kwa kuwa chama hicho kwa sasa kimesha laaniwa tofauti na kipindi cha Nyerere ambapo chama hicho kilikuwa kizuri kisicho na matatizo. Mbali ya kuitikia wito huo wa kurudisha kadi pia wananchi wengi walijiunga na CHADEMA idadi iliyofikia zaidi ya 1,000 katika matawi mbalimbali ya mji wa Makambako.



Mh. Thomas Nyimbo naye akitoa neno kwa mbwembwe bila kusahau kawaida yake ya kuingizia maneno ya Kibena kuonyesha msisitizo


Umati wa watu waliofurika uwanja wa polisi huku wakipunga mikono kuonyesha ishara ya kukikubali chama.
 
kweli watu wana machungu all the way from Iringa watu wanachangai chama...hivi chadema wana account ? au ipo kwenye website yao ..
 
Sasa ni dhahiri kabisa CCM ijiandae kuwa chama cha upinzani 2015 hii Taarifa na picha si habari njema hata kidogo kwa CCM, na sidhani kama kuna mtu wa kawaida wa kuichangia pesa CCM.
 
hii sio ausha? Mboma tunaambiwa chadema iko arusha tu? ritz vip uko wap teh...teh....teh makambako haituangushi tena jah pipo alisema yd atagombea mcmu mmja tu. Te 2015 ccm wakihonga ulanzi tunalewa na kula CDM CHAMA kubwa MNYAMA
 
Lazima itakuwa Arusha hapa.
Feedback acha utata lol...

Naona unataka kuwakurupua vilaza waliokariri...

Hakika hii habari imenifurahisha sana, na imetoa majibu kwa wale wanaopiga kelele "Arusha arusha".....

Maendeleo ya sehemu yanaletwa na wenyewe!

Mzee Thomas Nyimbo amenifurahisha sana.
Mungu awajalie nguvu na afya tele!
 
Last edited by a moderator:
Hapa hakuna kulala wala nini...

Mpaka kieleweke!!
:violin:
 
Waliokuwa wanasema Oooh mbona kila siku Arusha wapo wapi??

TUMBIRI wa JF,
P.O BOX - PM JF.
 
Wananchi Tanzania nzima wako tayari kwa mabadiriko!umakini wa viongozi wa Cdm,utaiondoa Ccm kabla ya,au 2015.
 
Back
Top Bottom