Picha: Grigori Rasputin na Familia yake wakiwa St. Petersburg

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
1622284889516.png

Rasputin with his wife and daughter Matryona (Maria) in his St. Petersburg apartment in 1911

Rasputin ni mzaliwa wa Urusi, alikuwa mshika dini sana na alijitangazia uwezo wa kuponya magonjwa. Hii ilikua sababu ya kumuweka karibu na ukoo wa Kifalme. Alimtibu mtoto wa Mfalme Nicholas II ambae alisumbulaiwa na ugonjwa wa haemophilia.

Ukaribu huu na familia ya Kifalme ulisababisha Rasputin kupata vitu vingi na nguvu katika jamii ya Kirusi. Wazee wenye hekima hawakupenda haya na walifanya mpango wa kumuua Rasputin 1916.

Ukaribu wa Rasputin kwa Tsar Nicholai II inasemekana ukichochea mapinduzi ya Kijamaa yaliyouangusha utawala wa Tsar nchini Urusi.
 
Haha Huyu jamaa nilisoma Historia yake namna alivyowaingiza Mkenge akina Czars Nicholas na wenzie
 
Wenyewe walimwita Bogus Holy man of Russia. Gregory Rasputini alikuwa ni mtu aliyependwa sana na familia ya Tsar Nicholas Alexander wa Russia na alikuwa mmoja wa washauri wakuu wa Mfalme.

Warusi wengi hawakumpenda wakidai ushauri wake ulikuwa unampotosha Mfalme lakini kwa kuwa mke wa Mfalme aliyeitwa Tsarina Alexandra alikuwa akimpenda sana Rasputini haikuwa kazi rahisi kumtenganisha Rasputini na familia ya kifalme.

Baadhi ya watu walidai ulikuwepo uhusiano wa kimapenzi baina ya Rasputini na Tsarina Alexandra. Rasputini aliuawa kwa njama zilizopangwa dhidi yake na maofisa wa serikali.
 
Nilipokuwa kijana, jambo pekee nililopenda sana Urusi (nilikwenda mara mbili kwenye mikutano) ni kuwa kulikuwa na wasichana wazuri sana ambao walikuwa rahisi sana kuelewana hasa kama hujui kirusi na wao wanajua maneno machache ya Kiingereza.
 
Nilipokuwa kijana, jambo pekee nililopenda sana Urusi (nilikwenda mara mbili kwenye mikutano) ni kuwa kulikuwa na wasichana wazuri sana ambao walikuwa rahisi sana kuelewana hasa kama hujui kirusi na wao wanajua maneno machache ya kiingereza.
Kwahiyo ulikuwa unajipigia tu Mkuu!
 
Back
Top Bottom