PICHA: Godbless Lema alivyotingisha Jiji La Arusha Jana

wahamishie Ubelgiji....wapeleke Yugoslavia.....kinachomatter hapa ni nini kinajiri kuhusu mbunge wetu.....tunataka kujua kila kitu......labda hukumu itoke na tusielezwe.....wafanye siri....vinginevyo.....lazima kieleweke.....
Preta nimekuona kwenye picha za matukio ..
 
Last edited by a moderator:
kila nikiona mwitikio wa wana Arusha na ukomavu wakisiasa ,huwa na kumbuka JK nyerere na azimio la Arusha.Mikoa yote ingekuwa hivi Tz ingakuwa huru tayari.Big up wana Apolo safi sana Jombaa

Mkuu kitero, umetusahau Mbeya, Magamba yanajuta mkoa huu kuwa sehemu ya tz.
 
Inapendeza sana chalii yangu, nimeamini arusha ndiko mapinduzi ya kweli yalianzia, Mungu ibariki CDM
 
Mkuu big up sana kwa kurusha hiz photo tukajionea yaliojiri, kwel mkuu unaitendea haki kaz yako. safi sana jombaalai
 
102_6503.jpg


Nimeipenda sana hii ina ujumbe tosha!

Hivi hapa wale wamama wa Meru hawakushiriki? Waliona hii lakini ndo wakaenda kutoa tamko?
 
Tutakusanyika the new machinga complex (NMC), wengine Sanawari stand ya tax
Wengine. Tindigani Kimandolu
Wengine Mianzi
Wengine Ngarenaro
Wengine Patandi
Wengine Leganga
Na kila mahali, tutafunga Big Screens afu tutastrwam Live. Tutalia au kushabikia pamoja. Hata wakaisomee hiyo hukumu Iraq.


Sijui watuziaje habari. Sijuiiiiiiiiii

kwa hakimu mwenye akili atakuwa anajua raia wanataka nini kwahiyo kuwanyang'anya raia hao haki yao ni kama kujipiga risasi kichwani
 
Mkuu utasababisha CCM wasiwe na imani na polisi, ukizingatia kuwa polisi walipisha maandamano yapite. Na hiyo Mercedes ya Lema sijui ya mwaka gani!
...Model ya 1954 mkuu inatumia staff gear na bench seat ( hazina head rest)...Ni mchuma halisi ukilinganisha na C-Class za sasa ingawa ni more sophiscated...
 
102_6482.jpg


102_6497.jpg

Msafara wa aliekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjii ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama


102_6503.jpg

102_6507.jpg

Picha juu na chini wamama wakiwa wanapita njiani wakishangilia aliyekua mbunge wa arusha mjini -Chadema Mh,Godbless Lema wakati akipita kutoka mahakamani

102_6528.jpg

102_6487.jpg

Msafara wa aliekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini-Chadema Godbless Lema ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama
102_6472.jpg

Gari ya aliyekua mbunge wa Arusha mjini(CHADEMa)Godbless lema likiwa inasukumwa na mashabiki mara baada ya kutoka mahakamani
102_6537.jpg

Aliyekua Mbunge wa arusha mjini(CHADEMA)Mh Godbless Lema akiongea a wananchi nje ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani leo

102_6540.jpg

wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza aliyekua mbunge wa arusha mjini-Chadema Mh Godbless lema
102_6527.jpg

Hawa ni makamanda waliokuwa wamevalia Tisheti za M4C huku mungine akiwa ameshona kanzu kabisa
102_6480.jpg

Gari ya polisi ikiwa inapisha maandamano yapite
----
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake, Natalia Kimaro na Salum Massatiumesikilizwa ila kesi imearishwa.


Kesi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi jana imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali kupata matatizo ya kufiwa na baba yao mzazi


Jaji mkuu alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.


Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alongea na wananchi walikuwa wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki.


“mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi”alisema lema


Alibainisha kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo itajulikana kufa au kupona ,mkutano ambao utafanywa nyumba kwa nyumba pamoja na kitongoji kwa kitongoji

Hizi picha umekomesha kabisa wazee wa zamani mfano mr dhaifu aka vasco da gama na fisadi wenza.
 
Tutakusanyika the new machinga complex (NMC), wengine Sanawari stand ya tax
Wengine. Tindigani Kimandolu
Wengine Mianzi
Wengine Ngarenaro
Wengine Patandi
Wengine Leganga
Na kila mahali, tutafunga Big Screens afu tutastrwam Live. Tutalia au kushabikia pamoja. Hata wakaisomee hiyo hukumu Iraq.


Sijui watuziaje habari. Sijuiiiiiiiiii

labda waturoge tusijue kinachoendelea maana wanaarusha tuna mzuka ile mbaya kwa hukumu yoyote watakayotoa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom