Picha: Gari la serikali na mafuta ya serikali mtu anatumia shangingi hilo kwenda kulewa na kubebea malaya kwa Kodi za walala hoi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Kuna watu wamepinda nyie acheni. Pamoja na mkwara wa waziri mkuu lakini wapi!

SHANGINGI hilo, jana usiku mtu kalewa nalo chakali!

IMG_20200704_183635_011~2.jpg
 
Kwa hiyo akienda kuburudika asiende na gari?

Gari la serikali ni kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya serikali.
Hata ukimbeba mwanao kumpitisha shule wakati unaelekea kazini likitokea la kutokea ujue imekula kwako.

Watu wengi wenye kupenda umwinyi hutumia magari ya serikali kinyume na muongozo wa utumishi.

Hapo atakuwa njiani kutoka Bar kulewa anamwambia dereva awashe taa za tahadhari kumbe ndani kuna mlevi flani tu
 
Kazi na dawa wewe!-Zitto.
 
SU maana yake ni SOMA ULE.
Muache ale huyo boss.

In the serious note, hatuwezi kumtolea tuhuma huyo driver au boss aliyekuwa kwenye hilo gari kwa kuwa hatujui alikuwa kwenye mazingira gani mpaka alipofika hapo.

Huenda alipomfikisha boss somewhere, driver alitoka kutafuta chakula au maji kwa kuwa boss hulala executive lodges and on the way kwenda guest house driver alipofikia akaamua kujipatia kitu cha kula au jujichukulia maji hapo, au hata ukute huyo boss ndio alimtuma huyo driver akamchukule nyama choma mahali au ukute walikuwa safarini wakaingia hapo kula au kunywa.

Kosa kubwa baada ya kutoka hapo ni kuendesha hilo gari akiwa amelewa na asababishe ajali.
 
Kuna watu wamepinda nyie acheni. Pamoja na mkwara wa waziri mkuu lakini wapi!

SHANGINGI hilo, jana usiku mtu kalewa nalo chakali!

View attachment 1498150
Hiyo picha haiwezi kutushawishi kuamini kuwa huyo mtu alienda kulewa.
Tunaomba kama una maelezo au ushahidi zaidi ikiwa ni pamoja na majina ya huyo mtu uweke hapa ili watu wawezekuhukumu au kutokuhukumu muhusika
 
Hii picha haiwezi kutumika kuprove unachokisema,
Mtu anaweza akawa amepaki mbele ya Bar kisha akaenda sehemu nyingine kufuata huduma aitakayo,kupaki nje ya Bar hakutoshi kua ni ushahidi kamili kwa unachokituhumu mkuu.
Upo Sahihi Mkuu.
Wakati mwingine anaweza kuwa ameenda kumchukua Boss wake hapo..
Na pia kuwa Bar si kwenda kulewa tu..
 
Back
Top Bottom