Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,885
- 6,885
- Thread starter
- #21
Wewe, unajua maana ya ever green?
Nimeishi mkoa huo kwa miaka ishirini(20).....Idodomya, phew!
Nimewinda sana pimbi kwenye hicho kilima.
Acha tu nijibanze huku niliko.
Naijua Dodoma (Idodomya) kutosha, mlima huo ni karibu na Iringa Road kama sijashau. Hapa unaona Dodoma Airport ya miaka mingi sana tu upande wa kulia ni njia iendayo kule Msalato na ukitaka kuendelea hadi Kondoa-Babati-Arusha kazi kwako.
Nimeikumbuka Dodoma kuna wakati nimeendesha kwenye vumbi na mchanga gari toka Shinyanga - Nzega - Singida - Dodoma kwenya mashimo, mchanga, vumbi usiombe, ukiona tu Dodoma unajisikia uhueni kwani lami ndo ukombozi unajua Dar ni karibu. Safari nyingi bora kuzungukia Kwamtoro kwenda Singida utokapo Dodoma kuliko kupitia Manyoni balaa tupu.
Dodoma pazuri kama pangeendelezwa, na waliochagua hapo waliona mbali, ingekuwa Washington DC ya Afrika kama ilivyo Arusha mfano wa Jiniva ya Africa.
Ukiteremka kwa gari moshi pale station utachoka mwenyewe na zabibu nzuri hadi usahau kama uko safarini na kutamani safari ingeishia hapo.
Maji ndio tatizo, labda kama siku hizi wamelitatua, la sivyo ndoto za Mkapa kuyaleta ya kule Ziwa Nyanza ingekuwa ukombozi.