Picha - Design ya apartment iliyotulia India, nakunwa kichwa

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
Hili jumba ambalo lingali katika ujenzi (under construction) huko Mumbai - India lina mvuto pekee na wa aina yake. Mainjinia wetu wana nini cha kujifunza hapa? Hii kwangu imetulia.

ATT00001.jpg
ATT00002.jpg


Design iliyotulia inakonga nyoyo na kuvunjwa wapita njia shingo zao.
Kila apartment ina belcon swimming pool hadi kule juu mawinguni

ATT00005.jpg
ATT00004.jpg


Sehemu ya kukutania majirani kupunga upepo na kubadilishana mawazo, kukitulia kupo wazi, kama hali ya hewa inabadilika basi tunakava tusivurugwe na mabadiliko ya hali ya hewa.






ATT00003.jpg


Taswira yake baada ya kukamilika itakavyosumbua macho ya watu.
 
By Wilbert1974 Sababu uwezo wao ni designs za mbavu za mbwa na migongo ya tembo tu!

Ni kweli Broda kwasababu hawa wenzetu badala ya kujaribu kuleta mabadiliko katika fani yao, cha ajabu wao mainjinia wa Kibongo nao wameingia katika mkenge wa wanasiasa eti wanadai kuitwa Mheshimiwa Injinia Copy n Paste
 
Hii kitu imetulia balaa!!
Lakini hii kitu nayo inahitaji hela ndefu sana kuijenga, sio sawa na jengo la umoja wa vijana wa chama cha mabwepande.
 
Tutatafuta njia ya kupeleka Bwagamoyo kitu namna hii kama mbili hivi.
 
Sababu uwezo wao ni designs za mbavu za mbwa na migongo ya tembo tu!

Mimi ni Mhandisi wa umeme (Electrical Engineer),Ngoja niwape shule kidogo sio mnaropoka ropoka tu kama majuha;
1. Jengo hubuniwa na Msanifu majengo (Architect) kulingana na mahitaji, matakwa na uwezo wa mteja wake ili mradi sheria za miji zinaruhusu; jengo unaloliona hapo ni matokeo ya kazi ya Msanifu majengo ambaye hubuni na kuliweka katika taswira inayoeleweka wazi kwa mteja wake (3D view) kama linavyoonekana hapo juu

2. Baada ya jengo kubuniwa Mhandisi ndio anaanza kazi yake. Hapa kuna wahandisi wengi lakini muhimu sana ni Structural Engineer (nimeshindwa kiswahili chake). Huyu ndiye anayeweza kusema hili jengo linawezekana kujengeka au la. Kumbuka Architect anaweza kubuni umbo lolote analoona linampendeza lakini je linaweza kujengeka likafaa kwa matumizi au la hiyo ni kazi ya huyu Mhandisi.

Huyu ndiye atakayesema kulingana na umbo hili la jengo basi linatakiwa liwe na chuma au nondo au mchanga au saruji au kokoto gani, kiwango gani na kiasi gani katika kila sehemu ya jengo hilo ili kuliwezesha umbo hilo litokee na matumizi yanayokusudiwa yawezekane pamoja na kuhimili changamoto mbalimbali kama uzito, upepo, mafuriko na matetemeko.

3. Mjenzi (Contractor). Huyu ndie anayelijenga jengo. Huyu kazi yake yeye ni kujenga kila kitu kulingana na matakwa ya Engineer na Architect. Kama kaambiwa weka nondo sita za zaizi flani ataweka hivyo tu na si vinginevyo hadi jengo linaisha.

Baada ya kukupa shule hiyo nadhani utakua umehamishia kejeli kwa Architect. Tambua kwamba hakuna jengo liloshindikana kubuniwa na kujengeka Tanzania kwa wataalamu wa Kitanzania. Tatizo ni Mteja gani anayeweza kumudu ghalama ya kulijenga hilo jengo Tanzania? Au mnadhani wataalamu ndio wenye hela za kujengea kila aina ya jengo!

Nakumbuka kuna Mwalimu alipoambiwa umeme unaozalishwa Tanzania hautoshelezi mahitaji akadakia harakaharaka eti "sasa nynyi Wahandisi wa umeme kwa nini hamjengi mitambo ya kutosha"! Ikabidi nimuwahi kwa kumuuliza swali hilo yeye "sasa nyinyi walimu mnaona shule hazitoshi kwa nini hamjengi shule za kutosha"!

Tuache kudharauliana bila sababu.
 
Mumbai wameifunga goli Dubai..Kali sana.

Zamani majengo ya kifahari yalikuwa nchi za Ulaya na Marekani, leo hii ulimwengu ulivyo duara mambo yamegeukia upande wa nchi za pembezoni, kwani ulaya gharama za kiwanja tu ni bei ya kufa mtu. Gharama za ujenzi balaa ndio maana wanatumia zaidi miti kujengea nyumba zao hadi ghorofa tano kama ni residential building. Tatizo nchi za magharibi zilizoea majengo to import raw material form third and second world, lakini leo gharama za kusafirisha mali ghafi hyo inawagharibu na ndio wenye nafasi wanaamua kuwekeza huko huko kwenye source ya raw material.

Ughali wa maisha ndio unaoigharimu Ulaya na Marekani, kwani makampuni makubwa yanavyofunga biashara hasa retail and whole sale stores na manufactures na hivyo kusababisha lay off idadi kubwa ya wanaokosa kazi kuzidi kupaa na hivyo kuigharibu serikali gharama za kuwalisha na kuwapatia hifadhi ya kuishi kwa sababu ni walipa kodi waliokosa ajira si kwa kosa lao ila hali ya uchumi duniani.

Jengo kama hilo ukifuatilia utaona ni la wawekezaji toka nchi za magharibi, bora kujenga huko litalipa kuliko Ulaya ambako litapangishwa robo tu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom