Picha: Daktari wa ‘MOI’ muhimbili na nesi wake mbaroni kwa rushwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Daktari Matiko (katikati) akiongozwa na Afisa wa Takukuru (nyuma yake). Aliyetangulia ni wakili anayemtetea, Paschal Kamala.

…Akielekea kiz
imbani kwa upole.

Nesi KImwomwe (kulia) naye akielekea kizimbani kusomewa mashitaka yake.

DAKTARI wa hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI), Deodata Kisasi Matiko (30) na nesi wake, Erick Petro Kimwomwe (28), leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakishitakiwa kwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja waliyomwomba Stanford Aaron Mhina ili wamfanyie upasuaji wa mgongo ndugu yake aitwae Fanuel Daniel Gideon aliyelazwa Wodi ya Sewa Haji namba (18) Kitengo cha Mifupa (MOI).

Imedaiwa kuwa mgonjwa huyo alipelekwa MOI baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani ambapo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Kibaha na kuvunjika mgongo.

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

Japo wanasema Kila Mtu anakula Mezani kwake, Ubinadam kwanza, Kila unapoenda idara nyeti pesa mbele,Polisi, Mahakamani, Hospital, vyuoni , mashuleni.
 
Hapa sioni mantiki yeyote na hata waandishi wa habari mngesaidia kwa hili,,pesa za epa,richmond,mabilioni ya uswisi wako wapi hao watu?
 
Duu!!! au ndio wanafidia madai yao....Tanzania kila sehemu rushwa tu sijui tutakimbilia wapi.
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Rushwa, rushwa hadi katika kwenye maisha ya watu! Looooh. Tunakwenda waapii?
 
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
 
Tumechoka na hivi vidagaa jamani, twataka manyangumi! Bila manyangumi hatuwaelewi!
 
Hawa ni dagaa tu ndio TAKUKURU inwaona. CCM wanatoa rushwa katika chaguzi zao na TAKUKURU wanalijua hili lakini hawakamatwi.

POLE SANA DADa

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!
 
Binti anaonekana mpole msomi mzuri sijui hana haraka gani ya kupata pesa wakati bado ana umri mdogo, hayo ni matunda ya kuporomoka kwa maadili.
 
Pole dada yangu bahati haikuwa yako.Mali za nchi yetu zinapotea na kura zetu zinanunuliwa hawakamati mtu wanakuja kukukamata wewe uliokuwa unaokoa maisha ya mtu.
 
Binti anaonekana mpole msomi mzuri sijui hana haraka gani ya kupata pesa wakati bado ana umri mdogo, hayo ni matunda ya kuporomoka kwa maadili.

Pesa wanazopata wanasiasa vilaza kama nepi ndio zinawafanya wawe na speed. Angekuwa na akili akaenda kapigilia t-shirt ya "2010-ushindi ni lazima' hiyo kesi ingeishia hapo hapo kwenye kusomwa
 
kumbe mkuu Ritz unayaona haya
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
 
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.

Ritz, bado hatuna hakika Kama madai hayo ni ya kweli. Mh! Masikini dada wa watu.

Sina nyongeza.

Queen Esther
 
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
mkuu wa takukuru amechaguliwa na nani?kumbe wakati mwingine unaakili na unatambua ugomvi wetu wataka mabadiliko,njoo chadema tupambane kufuta huu upuuzi wa ccm
 
Hawa Takukuru siwaelewi kabisa!! Wanakamata wala rushwa wa 1m wakati wa mabilion na wale wa hela chafu wa Uswisi na wa Dowans na wa Meremeta!! Yaani upuuzi mtupu!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom