Picha: Daktari wa ‘MOI’ muhimbili na nesi wake mbaroni kwa rushwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Daktari Matiko (katikati) akiongozwa na Afisa wa Takukuru (nyuma yake). Aliyetangulia ni wakili anayemtetea, Paschal Kamala.…Akielekea kiz
imbani kwa upole.Nesi KImwomwe (kulia) naye akielekea kizimbani kusomewa mashitaka yake.DAKTARI wa hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI), Deodata Kisasi Matiko (30) na nesi wake, Erick Petro Kimwomwe (28), leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakishitakiwa kwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja waliyomwomba Stanford Aaron Mhina ili wamfanyie upasuaji wa mgongo ndugu yake aitwae Fanuel Daniel Gideon aliyelazwa Wodi ya Sewa Haji namba (18) Kitengo cha Mifupa (MOI).

Imedaiwa kuwa mgonjwa huyo alipelekwa MOI baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani ambapo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Kibaha na kuvunjika mgongo.


PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

 

msemakwelii

JF-Expert Member
Sep 12, 2011
216
0
Japo wanasema Kila Mtu anakula Mezani kwake, Ubinadam kwanza, Kila unapoenda idara nyeti pesa mbele,Polisi, Mahakamani, Hospital, vyuoni , mashuleni.
 

Chimbuvu

JF-Expert Member
Jul 17, 2012
4,404
2,000
Hapa sioni mantiki yeyote na hata waandishi wa habari mngesaidia kwa hili,,pesa za epa,richmond,mabilioni ya uswisi wako wapi hao watu?
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Duu!!! au ndio wanafidia madai yao....Tanzania kila sehemu rushwa tu sijui tutakimbilia wapi.
 
  • Thanks
Reactions: PhD

Waambi

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
737
0
Rushwa, rushwa hadi katika kwenye maisha ya watu! Looooh. Tunakwenda waapii?
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
 

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,787
2,000
Tumechoka na hivi vidagaa jamani, twataka manyangumi! Bila manyangumi hatuwaelewi!
 

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
2,000
Hawa ni dagaa tu ndio TAKUKURU inwaona. CCM wanatoa rushwa katika chaguzi zao na TAKUKURU wanalijua hili lakini hawakamatwi.

POLE SANA DADaMIZAMBWA
INANIUMA SANA!!
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Binti anaonekana mpole msomi mzuri sijui hana haraka gani ya kupata pesa wakati bado ana umri mdogo, hayo ni matunda ya kuporomoka kwa maadili.
 

MLERAI

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
668
475
Pole dada yangu bahati haikuwa yako.Mali za nchi yetu zinapotea na kura zetu zinanunuliwa hawakamati mtu wanakuja kukukamata wewe uliokuwa unaokoa maisha ya mtu.
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
2,000
Binti anaonekana mpole msomi mzuri sijui hana haraka gani ya kupata pesa wakati bado ana umri mdogo, hayo ni matunda ya kuporomoka kwa maadili.

Pesa wanazopata wanasiasa vilaza kama nepi ndio zinawafanya wawe na speed. Angekuwa na akili akaenda kapigilia t-shirt ya "2010-ushindi ni lazima' hiyo kesi ingeishia hapo hapo kwenye kusomwa
 

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,701
2,000
kumbe mkuu Ritz unayaona haya
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
 

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,184
2,000
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.

Ritz, bado hatuna hakika Kama madai hayo ni ya kweli. Mh! Masikini dada wa watu.

Sina nyongeza.

Queen Esther
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,263
2,000
Lakini hawa Takukuru mie binafsi naona waganga njaa tu hata siku moja hawajawahi kumkamata kigogo yoyote zaidi ya kuwaonea mahakimu na watu kama hawa ambao hawana nguvu za kiuchumi.
mkuu wa takukuru amechaguliwa na nani?kumbe wakati mwingine unaakili na unatambua ugomvi wetu wataka mabadiliko,njoo chadema tupambane kufuta huu upuuzi wa ccm
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,901
2,000
Hawa Takukuru siwaelewi kabisa!! Wanakamata wala rushwa wa 1m wakati wa mabilion na wale wa hela chafu wa Uswisi na wa Dowans na wa Meremeta!! Yaani upuuzi mtupu!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom