PICHA: Chukua tahadhari; ukiona hivi usisogelee bahari, ni hatari!

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,077
17,208
Kuwa makini sana kipindi uwapo Beach!

Kabla ya kuingia kwenye maji, angalia vizuri bahari. Ikiwa utaona nafasi iliyojitenga kama uwazi katikati ya mawimbi, usiingie!

Ni mkondo wa chini na utavutwa ndani.

Mkondo huu unaweza kuwa UNDERTOW au RIP CURRENTS (unaweza uka-google kwa maelezo zaidi)

Wajulishe familia, marafiki. Hii inaweza kuokoa maisha.

View attachment 2024928
IMG_1637999483974.jpg
View attachment 2024929
imagesjpeg.jpg
 
Hiyo hali kwenye picha inaweza kutokea katika beach yoyote hata kama unaifahamu
Fafanua vizuri hapo mkuu

Nilichokielewa mimi kwenye hiyo picha ni kwamba hilo ni kama shimo lenye kina kirefu, sasa ukisema hata sehemu unayoifahamu shimo hilo linaweza kutokea unakua unanichanganya, yani leo nitose mguu baharini maji ya goti halafu kesho eneo hilo hilo pajichimbe pawe na kina kirefu

Au sijakuelewa?
 
Sio lazima liwe shimo.
Mkondo unaozungumziwa hapa unaweza kutokea hata sehemu ambapo hapana shimo

Ni maji yanakuwa na nguvu ya kuvuta kuelekea kwenye kina kikubwa cha bahari
 
Hiyo hali kwenye picha inaweza kutokea katika beach yoyote hata kama unaifahamu
Mkuu mimi nimewahi kuishi pembezoni mwa bahari kwa miaka kadhaa, Sawa tahadhari yako inaweza kuwa inamaana lakini labda uniambie kuwa bahari inaweza kuzalisha sinking holes mahali popote, vinginezo hicho unachokiongelea hapa ni cha kinadharia sana.
 
Kuwa makini sana kipindi uwapo Beach!

Kabla ya kuingia kwenye maji, angalia vizuri bahari. Ikiwa utaona nafasi iliyojitenga kama uwazi katikati ya mawimbi, usiingie!

Ni mkondo wa chini na utavutwa ndani.

Mkondo huu unaweza kuwa UNDERTOW au RIP CURRENTS (unaweza uka-google kwa maelezo zaidi)

Wajulishe familia, marafiki. Hii inaweza kuokoa maisha.

View attachment 2024928View attachment 2024930View attachment 2024929View attachment 2024937

Asante kwa taarifa Mkuu
 
Fafanua vizuri hapo mkuu

Nilichokielewa mimi kwenye hiyo picha ni kwamba hilo ni kama shimo lenye kina kirefu, sasa ukisema hata sehemu unayoifahamu shimo hilo linaweza kutokea unakua unanichanganya, yani leo nitose mguu baharini maji ya goti halafu kesho eneo hilo hilo pajichimbe pawe na kina kirefu

Au sijakuelewa?
HApo penye maji ya goti likija wimbi lenye mita mbili katikati ya wimbi kuna hiyo hali kwenye picha,ujue wimbi hilo linauwezo wa kukumeza.
 
Mkuu mimi nimewahi kuishi pembezoni mwa bahari kwa miaka kadhaa, Sawa tahadhari yako inaweza kuwa inamaana lakini labda uniambie kuwa bahari inaweza kuzalisha sinking holes mahali popote, vinginezo hicho unachokiongelea hapa ni cha kinadharia sana.
Umeongea litaalamu mkuu, underneath activities zinahusika!
 
Ndugu popote pale ulipo Asante sana kwa Elimu yako Kubwa uliyotupa hapa bila Uchoyo. Ubarikiwe!

Nimeamua kurudisha Nguo zangu za Kuogelea na sasa nageuza naenda Kijiweni tu Kucheza zangu Draft na Bao kwani ningeenda Kuogolea bila Kuusoma huu Uzi wako leo huenda KEROZENE ningekuwa no more duniani.

Wale wapenda Kula Uroda Mademu baharini Kazi mnayo nadhani Mawimbi hayo mmeyaona Shauri zenu.
Nenda kapozee machungu hata kwenye swimming pool kiongozi
 
HApo penye maji ya goti likija wimbi lenye mita mbili katikati ya wimbi kuna hiyo hali kwenye picha,ujue wimbi hilo linauwezo wa kukumeza.
nakumbuka kipindi cha nyuma bado bwa'mdogo tulikuwa tunaenda kucheza baharini, Unaweza kutembea hata zaidi ya mita 50kwenye maji kuelekea kina kirefu ndio maji yakufike kifuani au mabegani, hapo tunasubiri mawimbi makubwa kama haya unayoyazungumzia linapokuja kwa nguvu unajirusha katikati(mchomo)basi linakubeba kwa kukubingirisha mpaka juu kabisa kusipo na maji halafu yenyewe yanarudi kwa kasi nasisi tunanyanyuka na kuyafuata tena, jambo moja gumu la kuzingati wakati umapojirusha kwenye wimbi la aina hiyo hutakiwi kuvuta pumzi, Mpaka litakapokuacha. Maji ya chumvi ukiyavuta puani au ukiyanywa kwa wingi wakati unapoogelea ni rahisi sana kukuua.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom