PICHA: Cheti cha chanjo dhidi ya pandemic kipindi cha utawala wa Sultan Abdulhamid II wa Ottman mwaka 1908/1326 AH

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau...!
Katika pita pita zangu maktaba nimekutana na hii document ya chanjo kumbe haya mambo ya kuchanjana yalianaza kitambo sana sasa sijuhi hawa wanaokataa kuchanja wanapata wapi ujasiri.

Chanjo ilikuwa dhidi ya ugonjwa wa Plague ugonjwa ulisumbua sana dunia ukaenea Afrika mpaka Ulaya mwisho wake watu wakaamua kuchanjwa.

Historia inasema hapo Ottman Empire ugonjwa ulikuwa unaua si chini ya watu 2000 kwa siku.

image_00030c5a-d28a-435c-8bfd-2d8d9fefc1b520210919_081132.jpg
 
Dunia inapitia mambo mengi sana na sasa kila mmkja anacho mile anachokiamini na asilazimishwe wala kutukanwa kwa kile anachokiamini

Kila mtu ashughulike na anachokiamini kikubwa ni afikwe na ujumbe tu, sasa kuchanjwa au kutokuchanjwa ibaki kwake muhusika na si matusi wala kulazimishana
 
Hii ya corona inamashaka sana kumbuka zamani tofauti na sasa
Nchi km Congo walishageuzwa maabara za utafiti baada ya kukubali kila chanjo
 
Habari wadau...!
Katika pita pita zangu maktaba nimekutana na hii document ya chanjo kumbe haya mambo ya kuchanjana yalianaza kitambo sana sasa sijuhi hawa wanaokataa kuchanja wanapata wapi ujasiri.

View attachment 1944234
Wanapata ujasiri kwa vile ni binadamu wasiokuwa tayari kufanyiwa majaribio, pia kwa sababu chanjo hii ukichanjwa bado unaambukizwa, unaambukiza, unaugua na kufariki kwa ugonjwa huo huo uliochanjwa nao.
 
Ni wajinga tu.mtoto mpaka akue anaenda kuchanjwa clinic mara tano wanajua kilichomo?au hiyo pepsi unayokunywa unajua formula yake?
Ni kujifanya ujuaji tu

Vitu vingapi wanabugia kutwa kucha bila kuhoji…

Kwenu Covid wanajifanya wanayajua mengi

Maarifa madogo
 
Habari wadau...!
Katika pita pita zangu maktaba nimekutana na hii document ya chanjo kumbe haya mambo ya kuchanjana yalianaza kitambo sana sasa sijuhi hawa wanaokataa kuchanja wanapata wapi ujasiri.

View attachment 1944234
Kwani wasipochanja wewe inakuuma nini? Wewe peleka Tak*** lako likapigwe chanjo,mbona unatumia nguvu nyingi kulazimisha watu kufanya mambo ambayo ninyi Hamna faida nayo?

Si Bora wakatae chanjo ili wafe na korona ili wewe uliyechanja ubaki na kumiliki Mali zote zitakazo achwa na hao watu!! Hauoni kuwa hii inafaida kwako kwa kuwa Wewe umechanja?

Rais kashasema it is the matter of life and death so kila mtu afanye maaamuzi yake na hata lazimisha watu kuchanja,wewe peleka familia yako mkachanjwe.

Shubamiti!!!

NB sikatai chanjo Ila nakeleka na watu wanaotumia nguvu nyingi kulazimisha ng'ombe anywe maji ilihali Ni kwa faida yake.
 
Ni wajinga tu.mtoto mpaka akue anaenda kuchanjwa clinic mara tano wanajua kilichomo?au hiyo pepsi unayokunywa unajua formula yake?
Process ilizopitia chanjo za watoto tumeridhika nazo.. Na wala hakuna kulipana ili mtu achanje... Na hizo chanjo za watoto umeshaona zina ile form ya kujazwa kabla?

Kwenye Pespi, tuna mamlaka za chakula zimeshafanya taratibu zao hadi ikawa kwenye soko.. Hiyo chanjo ya korona inapigiwa chapuo sana na kwa namna mbalimbali... NA SIWEZI KUIMAINI CHANJO YA KORONA KISA NINA CHANJO YA NDUI.. HUKO NI KUSHINDWA KUJENGA HOJA
 
Mzungu akiamua kukua ni sekunde tu kuna njia nyingi,hizo za watoto unasema umeridhika nazo na hujui content yake,unakumbuka ukimwi kabla ya ARV hali ilikuwaje
 
Mzungu akiamua kukua ni sekunde tu kuna njia nyingi,hizo za watoto unasema umeridhika nazo na hujui content yake,unakumbuka ukimwi kabla ya ARV hali ilikuwaje
Kwani hali ya kabla ya ukimwi ilisababishwa na chanjo?
 
Back
Top Bottom