yegella
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,113
- 1,102
Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Mkalama jimbo la Iramba Mashariki chini ya kamanda George Gunda akishilikiana na viongozi mkoa wa Singida, kimezidi kujijenga baada ya kufanya mikutano kwenye vijiji vya Msiu, Mwangeza, Msisai, Nkungina na kujizolea wanachama wapya zaidi ya 330, mabalozi wa CCM 5 walioamua kuhamia chadema na kufanikiwa kumrudisha mwenyekiti wa chadema aliyenunuliwa miezi michache iliyopita na kutubu kuwa hato rudia kukisaliti chama hii kwani tangu akihame amekuwa hana amani moyoni mwake ingawa kifedha alivuna za kutosha kujengea nyumba ambayo sasa anaishi.. chadema pia ilitoa misaada kwenye kijiji cha Nkungi waliopata maafa ya kuezuliwa paa za nyumba zao na mvua kubwa.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Msiu waliojitokeza kumsikiliza Kamanda George Gunda..
Wananchi wakijiandikisha ili wapatiwe kadi cha chadema
Akinamama wakimsikiliza kijana wao Kamanda George Gunda..
Hapa kijiji cha Msiu..
Kamanda Gunda akiwa na OCD wa wilaya ya Nkalama
Hapa ni kijiji cha msisai....
Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Singida ndg Shaban(Mwenye koti refu) akiongea na wahanga baada ya kuwapatia misaada.