PICHA: CHADEMA walivyoisambaratisha Ngome ya Magufuli CHATO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA: CHADEMA walivyoisambaratisha Ngome ya Magufuli CHATO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Jul 20, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kagera kimeisambaratisha ngome ya Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, baada ya kufanikiwa kuwahamisha viongozi na wanachama 80 wa CCM akiwamo kada maarufu, Dk. Benedictor Lukanima.

  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Vua gamba vaa gwanda ndani ya Chato.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  
  Viongozi na wanachama hao wa CCM wakiongozwa na Dk. Lukanima, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na mtafiti katika Chuo Kikuu cha Norte kilichopo nchini Colombia, walitangaza rasmi kuvua gamba na kuvaa gwanda katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chato mjini, na kuongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kagera, Alfred Mganyizi Rwagatare.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Dk. Lukanima[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jimbo na wilaya hiyo ya Chato, Wana CCM hao waliohamia CHADEMA walikiponda vikali chama tawala, kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa kuwasaidia wananchi kuondokana na kero nyingi, ukiwemo umaskini wa kupindukia unaozidi kuota mizizi hapa nchini.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa CHADEMA Makonzela Phinias.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Baadhi ya viongozi wa CCM waliohamia CHADEMA ni pamoja na Makonzela Phinias ambaye alikuwa mjumbe wa UVCCM na mwakilishi wa mkutano mkuu wa Vijana Mkoa wa Geita, Masunga Maswanzali, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Nyasenga, Kijiji na Kata ya Ilemela, Josephat Manyenye ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM pamoja na Dk. Benedictor Lukanima, ambaye mwaka 2010 alishika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya chama hicho tawala.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Makusanyo ya kadi yakiendelea.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare alimrushia kombora zito Waziri Magufuli kwa madai kwamba, kiongozi huyo ameshindwa kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, ikiwamo ya uhaba wa huduma ya maji, afya, elimu na fursa za kiuchumi jimboni humo.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Kadi zilizorejeshwa.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Lwakatare alimuita Dk. Magufuli bingwa wa takwimu aliyeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake, licha ya kuwa waziri kwa muda mrefu serikalini. "Magufuli ni bingwa mkubwa wa takwimu. Anaweza kuwaambieni hadi samaki walio na mimba Ziwa Victoria. Lakini ameshindwa kutoa takwimu za wanafunzi wanaokwenda shuleni bila viatu wala ‘yebo yebo'.


  "Wakati umefika sasa wananchi wa Chato kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za hasira baina ya CCM na huyu Magufuli, kisha kuwachagua viongozi wa CHADEMA kwa maendeleo yenu," alisema Lwakatare.
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio nayo amani ikatawala.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Kuhusu bei ya pamba, Lwakatare ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), kabla hajahamia CHADEMA, alisema: "Serikali ya CCM pamoja na Magufuli imeshindwa kuwasaidia wakulima wa zao hili la pamba."
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Dk. Lukanima na wenzie wakitoka kwenye mkutano.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Kwa upande wake, Dk. Lukanima aliituhumu CCM na serikali kwa kukosa mwelekeo wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
  "CCM imekosa mwelekeo. Mimi na usomi wangu huu siwezi kuendelea kuwa ndani ya CCM ambayo naiona haina faida kabisa kwa Watanzania wenzangu. Hivi niwaulize ni yupi mwenye unafuu aliyeshika chuma cha moto na aliyeshika ubao?

  "Jibu ni aliyeshika ubao...kwa hiyo njooni tujiunge na CHADEMA kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii. Mfano, hapa Chato hakuna fursa za kiuchumi, mashirika yamekufa, huduma za kijamii mbovu, na anayeng'ang'ania CCM ni sawa na usaliti mkubwa wa maendeleo ya taifa hili," alisema Dk. Lukanima.

  Aliwaomba wananchi wa Chato, mkoa na taifa kwa ujumla kukiunga mkono Chama hicho cha CHADEMA, ili kujikomboa na adha mbalimbali zinazolikabili taifa na wananchi wake, na kwamba kilichomsukuma kuhamia chama hicho cha upinzani ni kwenda kuongeza nguvu katika vuguvugu la mabadiliko.
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  buriani magamba
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu hiyo ya kadi ya njano naiona vibaya! ni kama ina nembo ya JW vile? Lol Vuguvugu la mabadiliko noma!!
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Magufuli anaishia kutaja mavilometer na mavifungu ya sheria Huku chato ikiwa inamponyoka
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  M4c for life!
   
 6. MD24

  MD24 JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hali ikiendelea hivi huko chato, soon magufuli atasema "sitagombea tena ubunge, nataka nipumzike"
   
 7. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hizo kadi za CCM zinazorudishwa si wanazichoma moto? Hazina maana kabisa
   
 8. MD24

  MD24 JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  "chadema ni chama cha kaskazini"-Nape, sasa sijui chato iko kaskazini ipi...
   
 9. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Good bye CCM.
  MAGAMBA wamepoteza jimbo la chato Mh.Magufuli jipange 2015.
   
 10. k

  kichakare Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni nouma! jamani MIMIEM yangu inakufa mchana kweupe. nape kafukie mashimo pliiiiz
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Magufuli ajipange upya.....
   
 12. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkulu ....KUNA KADI YA NJANO HAPO NA YA BLUE HAPO NA NYEUPE HAPO...Mkulu tuelezee ni za vyama Gani!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hiyo ya njano ni UVCCM,Blue ni NCCR na nyeupe ni ya CUF.
   
 14. Wilawela

  Wilawela Member

  #14
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu ni kadi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) siyo JWTZ!
   
 15. KV LONDON

  KV LONDON JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 904
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Kitaeleweka tu'
   
 16. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Unajua sisi Watanzania tuna kasumba mbalimbali, kwa mfano..Uwezo wa kukariri wa Magufuli unatufanya tumkubali na kusahau majukumu anayopaswa kufanya. Ila tuwe waungwana, The man (Magufuli) does the Job. Japokua alinitpka rohoni kwenye kashfa ya kuwauzia nduguze nyumba za serikali kwa bei ya debe la Mtama.
   
 17. E

  Eddy GEng Member

  #17
  Jul 20, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo ni ya vijana...na co JW
   
 18. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu Dk. Benedictor , ni daktari wa philosophy au binadamu? Na vipi kuhusu CV yake hapo CHATO anaweza kutufanyia mageuzi mkuu?
  Na dulu za siasa zinasemaje hapo kuhusu mchakato wa chaguzi za serikali za mitaa na vijiji pamoja na viongozi ndani ya nyama vyote kwa ujumla?
   
 19. S

  SHIMBONONI Senior Member

  #19
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mkuu, Hiyo ni kadi ya UVCCM inayoongoza na Mwana Kishapu mwenzio Shigela!
   
 20. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safi sana ma kamanda go on M4C forever,
   
Loading...