(Picha) CDM ilitumia malori kusomba watu Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(Picha) CDM ilitumia malori kusomba watu Iringa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachanchabuseta, Sep 4, 2012.

 1. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  katika hali ambayo siku zote ilikuwa mbinu ya kujificha kukusanya watu
  atimaye mbinu ya chadema imebainika baadaya kukutwa inapakia watu
  kweye lori (katika picha)

  Kutokana na mtu aliyenidodosa ni kuwa Daudi mwandosi alikuwa anachukua
  picha kwenye gari la chadema ambalo linapakiza watu kuwaleta kwenye sehmu
  ya kufungua tawi, hiki kitendo kiliwakasilisha chadema

  Sasa hapo guess nini kilifuata

  Tazama hii picha kwa umakini kwanini Daudi alikuwa anapiga picha Lori lililobeba watu?

  Inakuwa Chadema wanasomba watu kuja kwenye mikutano yao?  [​IMG]
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo unataka kusema nini? go straight to your point gay!
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  AHADI YA 'UWAZIRI MKUU' KWA MWANACHADEMA UTAUA WENGI HADI KUNAKOFKA 2015:
  KIFO CHA DAUDI MWANGOSI KULE KIJIJI CHA NYOLOLO MKOANI IRINGA NI KWAMBA KIJANA KANASA KWENYE MTEGO SI WAKE


  Mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, afia msalaba si wake kwa kuchinjwa kinyama kwa kuwa tu moyo wake ulimtuma kutetea kile chenye maslahi kwa taifa dhidi ya maslahi ya CCM wilayani Mufindi.

  Mauaji haya wenye ukatili mkubwa na kudhalilisha utu wa Mtanzania kule katika kijiji cha Nyololo wala hayakutokea tu kama ajali bali ukweli wa mambo ni kwamba dhamira hii ilifahamika masaa 48 kabla ya zoezi la CHADEMA kwenda kufungua mashina ya kichama wilayani hapo. Swala kwamba polisi wanafanya maandalizi kwenda kuua Mufindi ni jambo lililoenea kwingi kwa zaidi ya asilimia 70 ya watu wa Mkoa wa Iringa isipokua undani wa akina nani wanaenda kuuaua na kwa mtindo gani pekee ndicho kilichobakia siri kuu kwa jeshi hilo.

  Kwa mujibu wa taarifa nyeti tulizonazo toka nyuma ya pazia, mhanga Daudi Mwangozi, kilichomuua ni kule kugundulika kuingiwa moyo wa upendo na kuamua kutahadharisha mapema na taarifa nyeti kuokoa MASLAHI YA UMMA mauaji ya kutisha yaliopangwa na nguvu zilizodhamiria kutetea CCM kwa gharama yoyote ile dhidi ya uongozi wa juu CHADEMA walioko mkoani hapo kwa ziara ya kikazi.

  Ndugu yetu Mwangosi ambaye alifika mapema katika eneo la kazi pale kijiji cha Nyololo na kuonekana kubadilishana utani na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA, wala hakua hataa na chembe cha taarifa kwamba umati wote uliokusanyika mahali pale majuzi ulikua ni wa kumhudhurisha yeye katika harusi ( harusi nyinginezo katika maisha ni kule kuzaliwa na pili kuoa au kuolewa) yake ya mwisho katika maisha.

  Siku zote wakati ukuta, wahenga husema, muda wa Malika Israeli kuchukua roho ya Mwangosi ulipowadia, mwenzetu alimaziza hatua zote za kutendewa haki kikatiba kwa maana ya kwamba ndani ya kitu kipindi cha wastani wa dakika kama 35 hivi kijana mwenzetu alishakutana na (1) polisi waliomnasa kwa kosa ambalo jamii ya Tanzania bado inasubiri kufahamishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani na jeshi lake, (2) akaswekwa rumande ndani ya dakika 5 tangu akamatwe, (3) dakika ya 21 tayari Mkurugenzi wa Mashitaka nchini alikwishaandaa faili yake kule Dar es Salaam na kuirudisha Iringa kwa (4) hakimu Kamuhanda (mdogo wake Seth Kamuhanda wa Ikulu) tayari kwa kutoa hukumu juu ya hatima ya kijana Daudi sawasawa na mapenzi ya makao makuu nchini.

  WaTanzania wenzangu, hukumu ya kifo kilopotolewa na Kamanda Kamuhanda kupitia kwenye radio call pale kwenye gari la umma lililokua limeegeshwa pembeni kidogo tu kutoka machinjioni Nyololo, kijana mmoja kati ya vijana watatu wa 'vikosi maalum' nchini waliopelekwa Iringa siku tatu tu kwa shughuli maalum ndiye aliyetekeleza agizo la Kamuhanda tena kwa ufundi wa hali ya juu iliowaduaza hata vijana chipukizi kwenye jeshi la FFU pale Iringa.

  Ndio, ukweli wa mambo ni kwamba huyu kijana mwenzetu Daudi Mwangosi kamwe hakunyimwa haki ya kusikilizwa na jeshi makini chini ya mzalendo namba 6 kitaifa kwa viwango vya CCM Chamwino, Saed Mwema, kama katiba inavyoelekeza kwa mtuhumiwa wa kosa lolote lile, bwana huyu hakunyimwa muda wa kuita mwanasheria wake kuja kumtetea dhidi ya hii nguvu kubwa yenye maelekezo moja tu; maslahi ya CCM kwanza, maslahii ya taifa itategemea na hali itakavyoruhusu.

  Naam, nasema kwamba si siri kwamba Mwangozi hakunyimwa haki ya kuwaaga marafiki zake hata Ken Simbaya analitambua hilo, hakunyimwaa haki ya kuwaaga wazazi na familia zima kwa maana kwamba mzazi wake wa Magogoni alionekana kumpenda zaidi kitaifa.

  Ukweli wa mambo ni kwamba mwenzetu Daudi Mwangosi kimsingi aliruhusiwa na hakimu Kamuhanda kutekeleza mambo mengi sana tu ndani ya kipindi hicho cha dakika 35 isipokua tu ni kwamba ilimezwa na zile za jopo lililokua likimsafirisha toka hapa duniani kwenda ulimwengu mwingine huko ahera.

  Hakika baadhi ya chipukizi hawa walionekana wazi kutokuamini macho yao jinsi gani kijana mwenzao Daudi Mwangosi waliomuona chini ya dakika 15 zilizopita akiwa amependeza ajabu na kitendea kazi yake begani (kamera) jinsi gani alivyogeuka rundo tu la nyama mahali pale.

  Kwa taarifa tulizo nazo hadi hivi sasa, baadhi ya hawa vijana wanahali mbaya mno kisaikolojia tangu siku waaliporejea mjini Iringa wakitokea kwenye hiyo kazi nyeti Mafinga, mji mdogo nje kidogo ya Iringa lakini yote juu ya yote WaTanzania wengi bado wanaendelea kutanabahi juu ya nini hasa kilichomfikisha huyu mwenzetu mahali hapo.

  Sote tunajua kwamba tangu CHADEMA kiamue kwamba utani wa kuwa chama cha uchaguzi au cha msimu ndio basi tena, ni ukweli kwamba viongozi wa CCM hawajakaa wapate kufahamu kitu amani moyoni wala kule kujistarehesha kitu kwa kiburi cha kobe kugoma kutembea pindi aguswapo isipokua mambo ni mchakamchaka ulimi nje afadhali ya siku jana kwao kisiasa nchini.

  Katika hali ya kuonyesha hayo mafanikio makubwa na kuendelea kukubalika kwa chama cha upinzani nchini hakika linaonekana kuleta tabasamu na nuru ya maisha iliopotea miaka mingi tangu Mwalimu Nyerere, kiongozi pekee aliyewadekeza sana wananchi wa taifa hili, atutoke.

  Licha ya msururu huo mrefu wa mafanikio kwa CHADEMA, mtazamo kwa upande wa pili ni huzuni kuu kuona CDM kuonyesha kukubalika kupindukia kila kukicha tayari kumesababisha songombingo si tu katika kundi la wanasiasa wa kambi ya chama tawala bali pia kwa theluthi ndogo ya wanasiasa chipukizi ndani ya CHADEMA yenyewe ambayo nayo inajitafsiri kuumizwa sana kisiasa na mafanikio haya ya tangu kuzaliwa mtoto 'Movement for Change (M4C)' ambayo kila siku wanaonekana kulipiga chenga kutokushiriki shughuli zake lakini bila mtu yeyote kuhisi utupu wowote wa uhiari wao huu kutokujipanga wazi wazi na jeshi la kisiasa la chama chao ambacho hivi sasa ni lulu kwa zaidi ya 70 % ya wapiga kura nchini.

  Naam, ni siri ilio nje kabisa kwa Wana-CHADEMA walio wengi kwamba ni hili hili kundi dogo la baadhi ya wanasiasa chipukizi na wenye kuegemea udini wanaojihisi kwamba wao hawana chao katika mafanikio haya makubwa CHADEMA, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba kiota chao cha kutingishia kiberiti cha udini tayari kilishasambaratishwa na CDM mara baada kuingiza chamani jopo kubwa la wanachama mali zaidi, waaminifu zaidi na mahiri zaidi kwenye michepuo yao ya kitaaluma na kuheshimika sana kijamii, ambao ndio hivi sasa wameamua kuunda umoja na kundi mojawapo kati ya vikundi kibao ndani ya CCM kujaribu kutupa karata yao ya mwisho kabla ya kuinua rasmi mikono yao juu mbele ya nguvu ya umma wa Tanzania.

  Kama mtu atakua anadhani kwamba usemi kwamba 'hofu kuu na kiwewe humgeuza hata simba kuwa paka' ulikosewa basi kwa taarifa yako utakua umekosea sana tena ajabu. Mbali na CDM kuonekana kuwa ni tishio la uhakika kuendelea kwa utawala wa CCM kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa, mafanikio yake makubwa ya kufungua utitiri wa matawi kila kona ya dunia, kukubalika zaidi huko na hata kupewa michango mikubwa mikubwa ki-hali na mali ndio kabisaaaa kimeingiza hofu kuu ndani ya CCM vikundi vyake vyote nchini na hata kuamuliwa kufanyika kwa msururu wa vikao ndni na nje ya nchi kutafakari kwa pamoja NINI KIFANYIKE KWA KIWANGO MITHILI YA BIG BANG / AU GAME CHANGER ili kuzuia CHADEMA kukamata dola kiulaini kiasi hiki.

  Naam, ni hiyo hiyo hofu kuu na kiwewe cha ajabu kisiasa nchini kufuatia mabadiliko kisiasa kwa kasi mwangwi wa sauti inayofanywa na CHADEMA na washirika wake nchini na kiwewe chake ndio cha kile kilichowasukuma baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu CCM kufanya vikao vya siri kibao na kisha kuamua BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA inayokisubiri chama hiki kwenye sanduku la kura miaka michache ijayo.

  Lengo la kumsambaratisha mwili mwandishi huyu ilikua ni KUTIA HOFU UMMA WA TANZANIA kwa kuwa hiyo SILAHA YA HOFU NA KUTOKUJIAMINI ni silaha iliokilea vema CCM kukalia madaraka kwa zaidi ya miongo 4 hivi sasa bila mtu yeyote kupaza sauti juu ya kitu haki lakini kwa programu ya elimu ya uraia inayoendeshwa kote nchini na asasi zisizo za kiserikali na pia CHADEMA tena kwa mafanikio makubwa hadi vijijini, wana-Chimwaga kwa tathmini yao hivi majuzi wakuja kubaini kwamba wananchi, kwa viwango vya juu sana kiminyanyaso wamefikia mahala hawana hofu tena na serikali ya CCM pamoja vyombo vya dola vinavyotumika kiitikadi zaidi.

  Lengo la pili lililofanya NEC-CCM alioongoza rais Kikwete kwa notisi ya dharura Majuzi mjini Dodoma kuamua kufanya msururu wa mauaji kila CDM wanakofanyia mkutano wa kisiasa ni kule kutafuta kukishawishi chama hiki cha upinzani kukubali kuingia kwenye laini ya kufanya vurugu ili CCM kiweze kupata urahisi na kisingizio cha kuwadhibiti barabara na zaidi kuwaua baadhi ya viongozi tumainio na wenye msimamo usioyumba kwenye chama hicho.

  Itakumbukwa kwamba CDM wamejitahidi sana kukinyima nafasi hiyo CCM hivyo chama tawala kushindwa pakuweza kufaidi kutumia nguvu za dola kwa faida yao kukidhibiti wahasimu wao. Ni kweli kwamba wengi wetu wahatambui jinsi gani silaha hii ya CDM kujichagulia KUTOKUKUMBATIA VURUGU, hata kichokozwe na kuchokonolewa vipi, ilivyochangia sana tena sana kukiimarisha chama hiki na kukidhoofisha maradufu CCM angali anazo na silaha za kivita zilizoagizwa toka Iran na bila kusajiliwa popote. Katika hili la silaha ni faraja kubwa kwamba tayari Jumuia ya Kimataifa inakaribia sana kufanya jambo humo.

  Kwa kuahirisha tu taarifa hii juu ya kifo cha Mwangosi kwa msalaba wa wengine, ni muhimu kudokezea tu japo ki
  dogo kwamba maandalizi kutekeleza mauaji ya kisiasa kule Mufindi wala ilifanyika kwa hisani ya Mwana-CDM aliyeinya uia kuona viongozi wake wa juu wakiuaua ili ndoto ya ahadi ya Uwaziri Mkuu uweze kutimia kwa uhakika zaidi mnamo 2015.

  Kwa taarifa tulizo nazo hata hivi sasa kuna baadhi ya taarifa za chama na nyingine nyingi zikiwa ni za kupika zinaendelea kujadiliwa na kuwekewa mikakati hivi sasa nje. Haya yote ni sehemu ya maandalizi kambambe vikao vya siri vilichofanyikia mjini Dar es Salaam wiki moja Kamanda Lema alipokua Ulaya, baadaye kukafanyika nyingine Dodoma kabla ya kikao cha dharura cha NEC-CCM, na sasa sehemu nyingine ikiendelea kule Adis Abbaba Ethiopia.

  Mungu aziweke roho za Ally (Morogoro) na Daudi (Iringa) mahala pema peponi huku tukiendelea kufunga kwa sala kwa ajili ya na wale wengine wengi ambao CCM tayari kinainuia kuwapunja haki ya kuishi na uhuru wa maoni kwa kutetea maslahi binafsi na mabilioni yaliofichwa Uswisi.

  Wapenda mabadiliko wote, mapambano mbeeeeele kama tai mpaka CCM na mafisadi wake wote hata wale waliojificha ndani ya vyama vya upinzani wote kung'olewa madarakani kwa nguvu ya kura zetu kwa pamoja.
   
 4. joramjason

  joramjason JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Bila shaka utakuwa una ****** makubwa
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hivi uoni spika zile.....kweli kichwa umedugia nywele hata macho hayaoni?.........kazi mnayo hatuna ela ya kusomba raia sisi
   
 6. Jamiix

  Jamiix JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 817
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 80
  We nanii kweli!,huoni kama limebeba speaker kwa ajili ya shughuli husika!?
   
 7. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Acha ujinga huo. Hivi huoni kuwa hao ni makamanda.
  Hata mkikwepa ukweli utabaki kuwa mmeua na damu za hawa watu na machozi ya ndugu zao zitawaotea kichwani.
   
 8. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  rest in peace jeykey!
  aliyekutuma mwambie umewakuta wenyeji!
   
 9. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Acha ujuha
   
 10. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  inaonyesha uanasiasa wako ni wa shule za msingi enzi za tanu.Mbona inaonyesha hujui kuumba hoja.na pia aliuawa si mwadosi bali ni mwangosi.Kwakuwa huyo unalipeta taarifa ni mwandosi hakuna haja ya kusikitika kwa sababu hajauliwa na polisi.
   
 11. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hata kama CDM ingewasomba watu kwani kosa? Mbona CCM mmeishiwa hata common sense? Isitoshe gari lenyewe limebeba vyombo wewe unaweka lako. Hata mngesemaje ni kwamba mwisho wa CCM si ndoto tena wala hadithi bali ukweli usiopingika. Jiandalieni matanga yenu na mahali pa kuwazika kwani hata upinzani hamtauweza kwa vile mmezoea dezo.
   
 12. RICARDO KAKA

  RICARDO KAKA JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 867
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  naomba nikuulize!
  ulizaliwa kwenye danguro?
  wazazi wako wote wazima?
  una mchumba?
  una elimu gani?
  ..........................................
  ..........................................
  .........................................
  ..........................................
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wewe Jeykey ni majanga kama kikwete
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shigongo style Tehe Tehe Tehe
   
 15. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama unaweza kutofautisha kati ya Lori na Canter, ****
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe umepofuka?
   
 17. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ulitegemea waende vp kufungua matawi vijijini?.Serikali yako imeweka miundombinu? We fara nini
   
 18. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kwani uoni watu wanagombania kuingia kwenye gari?
   
 19. Mr Dhaifu

  Mr Dhaifu JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  wewe umejaza kamasi nyingi kichwani mwako haya na guess si kweli hilo ni gari la matangazo hao ni watoto vijijini hupenda kufuata magari ya matangazo.
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
   
Loading...