Picha: Bweni lililomliza Naibu Waziri Mahiza Tanga

uwiiiiiiii!!!!! Maskini sijui wanasomaje hawa watoto. Sasa mvua ikinyesha si hatari, ndio maana naibu katoa machozi maana inasikitisha mno.

...Pretty 'umeona' mvua, mimi naona janga la moto hususan kwa hayo makuti!

...Kilio cha Shauritanga bado kinasikika masikioni mwangu!...
 
Jamani!!!!.... Huyo mama analia unafiki mtupu!! Hilo alilijua siku nyingi ni vile tu anajaribu kutafuta kura 2010.
 
Hapo bado walimu hawajalipwa mishahara yao....rais yuko tour US....wawekezaji wana pewa tax heaven....mafisadi wanapeta na kesi kutoeleweka....je uchaguzi unaokuja tuko makini nao?
 
...acheni story nyingi,malalamiko na kujifanya mnashangaa sana hali hiyo,sasa mnaonaje tufanye fundraising kwa kutumia hii jamiiforum kujenga hilo bweni?
 
Lakini kunawakati sisi tupo nje ya hali halisi kabisa, tunashangazwa na bweni hilo wakati kunawatoto wanapanga mitaani na vijijini maana shule hazina mabweni! Ushafikiria kuona mtoto wa form one anapanga kwenye nyumba ya udongo? Umeshafikiria watoto wanaotembea zaidi ya saa moja kwenda shule?

Elimu inatakiwa kufikiriwa kwa mapana yake - kuhakikisha watoto wanaishi salama na kusoma katika mazingira bora. Hili linawezekana kabisa kwa juhudi za serikali na wananchi.
 
...acheni story nyingi,malalamiko na kujifanya mnashangaa sana hali hiyo,sasa mnaonaje tufanye fundraising kwa kutumia hii jamiiforum kujenga hilo bweni?
Mie naona JF ichukue shule kabisa, uwe mtaji wa Jf. Nadhani wanachama watakuwa tayari kuchangia.
 
Kalia kinafiki tu, ama yeye anatoka Tanzania ya CCM ipi.
Hali duni ya mashule yetu, hospitali etc ni matokeo ya usimamizi wa CCM - Tanzania si Kilimanjaro tu.
 
Machozi ya uchaguzi 2010 hayo... alisoma hapo hapo... Zingibari Primary School Primary Education 1962-1966 CERTIFICATE
Source: Parliament of Tanzania

Machozi ya mamba amtafunapo mtu na pia machozi ya samaki huenda na maji! wenyewe baada ya kutirirsha machozi wakapanda mashangingi yao na kuondoka huku wakiongea na watoto wao wanaosoma kwenye shule zenye hadhi ya shule na kuwaacha maskini watoto wale kwenye mazingira ya bweni lilelile. MACHOZI YA MAHIZA YAMEBADILI CHOCHOTE KWENYE HILO BWENI?
 
kikwete kaenda majuu kuomba msaada akirudi vijana maisha tambarale.....
 
...acheni story nyingi,malalamiko na kujifanya mnashangaa sana hali hiyo,sasa mnaonaje tufanye fundraising kwa kutumia hii jamiiforum kujenga hilo bweni?

Fundraising ya kuiweka hewani JF tu inatushinda,ndiyo itakuwa ya mabweni hayo ambayo hayatugusi moja kwa moja! maneno yetu yaambatane na dhamira ya kweli siyo kujua kutype tu maneno mazuri.
 
...acheni story nyingi,malalamiko na kujifanya mnashangaa sana hali hiyo,sasa mnaonaje tufanye fundraising kwa kutumia hii jamiiforum kujenga hilo bweni?

Wazo lako zuri lakini mimi naona kwanza Rostam et al wakamatwe ndo tuanze kuchanga kwa sababu tukichnga sasa hivi watazifisadi tena.
 
Hivi hii ni shule ya serikali, Wazazi au Private???

Inasikitisha kwelikweli!!!!!!!!!!!!!
 
Fundraising mkuu hapana bana, tuna historia mbaya hapa kijiweni Mzee Mwanakijiji analijua hilo mpaka leo hajatoa hesabu ya ule mshiko wa vijana wetu wa Ukraine. Na haya mambo ya credit crunch ndio kabisa ufisadi siku hizi kila mahala
 
Jamani!!!!.... Huyo mama analia unafiki mtupu!! Hilo alilijua siku nyingi ni vile tu anajaribu kutafuta kura 2010.

Ni ukweli kuwa huo ni unafiki, ina maana hana picha halisi ya matokeo ya utawala mbovu katika nchi hii? Matokeo ya ahadi hewa, na wizi wa mchana kweupe wa rasilimali na kodi zetu. Hali ni mbaya zaidi ya hapo kwa walio wengi Tanzania. Akamweleze bosi wake hiyo stori, halafu mwakani aende kuomba kura kwa kuwaahidi maisha bora. Halafu wanatuambia kama hakuna mikate tule keki?
 
Fundraising mkuu hapana bana, tuna historia mbaya hapa kijiweni Mzee Mwanakijiji analijua hilo mpaka leo hajatoa hesabu ya ule mshiko wa vijana wetu wa Ukraine. Na haya mambo ya credit crunch ndio kabisa ufisadi siku hizi kila mahala

Ulichangia?
 
Duuu kwa kweli inasikitisha sana tena ikizingatia huyo mama ndio mbunge wao akiangalia maisha anayoishi ,anavyo wish azidi kuwa juu zaidi na kuishi standard life....watoto wake wanakosoma...duuu kama mzazi mwenye machungu....lazima alie na anajua kabisa uwezo upo wa kuwasaidia...wapiga kura wake..............jamani inasikitisha sana....hapa ndipo pa kuwachangia kwa harambeee wabunge wote wa mkoa wa tanga na wa tz wote kwa ujumla
 
Bweni lenyewe hili hapa. Inasikitisha sana.

Nafikiri huu ni ufisadi mbaya zaidi kuliko ule wa "BOT Twin towers". I just feel like watanzania wote tuko uchi hapa. Hivi ni kwa nini viongozi huwa wanavaa suti mara nyingi? Eti na wabunge wetu, mawaziri, wakurugenzi mawizarani na mimi mwenyewe huwa tunavaa suti.. ni nini huwa tunaficha teh he he he!:mad:!!
By the way Ni kitu gani kinahalalisha tuwe tunasheherekea siku kuu ya Uhuru kwa mtindo huu?

Ah naona nisiendelee kuongea... mimi siwezi kulia lakini hii image imenitia hasira sana leo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom