Picha aliyonayo Rais Magufuli Kuhusu Magereza Siyo Picha Halisi Iliyopo kwenye Jeshi hili

Nov 26, 2016
9
43
Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyemuumba wa Mbingu na Nchi, kwa kutukilimia pumzi ya uhai ambapo kwa neema hiyo tunaweza kufanya mambo yote katika Yeye atutiye nguvu. Nitapenda leo nielezee baadhi ya mambo kuhusu Jeshi la Magereza, mambo ambayo yanawahusu askari na siku nyingine nitaelezea kwa kina mambo yanayowasibu wafungwa ambao ni ndugu zetu huko uraiani pindi watumikiapo vifungo vyao magerezani.

Pili nichukue nafasi hii kumshukuru Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa ziara aliyoifanya wiki iliyopita katika jeshi la Magereza ambapo katika ziara hiyo ambayo imeambatana na kuachia ngazi kwa boss wa magereza au Kamishina Jenerali wa Magerereza John Casmir Minja ambaye katika utawala wake uligubikwa na mambo kadha wa kadha ambayo hayakuwa na majibu wala suluhisho kiasi cha askari na maafisa kushindwa kupata sehemu ya kuelezea matatizo na changamoto wanazokutana nazo ndani ya jeshi hili.

Mh. Rais ziara yako pale Ukonga ni ziara iliyoleta matumaini sana kwa wanyonge (askari wadogo) ndani ya Jeshi hili kwani ndio watu pekee wanaolipata joto la ugumu, mateso, dhihaka, vitisho, utumwa na manyanyaso katika kazi hii ya magereza kwakuwa tu ile misingi ya utawala bora na haki za binadamu kwa askari haifuatwi kama ilivyo katika idara zingine aidha za kijeshi au za Serikali kiasi cha askari na maafisa ndani ya idara hii kujiona wako katika ulimwengu mwingine huku wakiishi maisha ya kufungwa kindoto, kifamilia, kielimu, kiuchumi na kijamii.

Mh. Rais pamoja na hotuba yako nzuri ambayo uliweza kuitoa pale ukonga mbele ya askari wa vyeo vyote kuanzia warder mpaka cheo cha Kamishina Jenerali huku ukielezea namna ambavyo unaifahamu idara hii ya ulinzi hasa ukigusia changamoto na matatizo yake na kujibu maswali ya askari mbalimbali yaliyoulizwa, LIPO SUALA MOJA aidha kwa kutokupewa taarifa zilizo sahihi au kwa kutokuielewa idara ya magereza kwa undani kutokana na kujiweka kwake nyuma kwa viongozi wake kwa minajili ya kuhofia kutumbuliwa na kupoteza nafasi zao hivyo ulijikuta ukipiga jiwe mahali ambapo si penyewe.

Mh. Rais idara ya Magereza ina askari wa rika kuanzia miaka kumi na nane mpaka sitini, makabila mbalimbali, dini zote, na viwango vyote vya elimu kuanzia darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita na chuo kikuu. Jeshi hili kwa miaka ya hivi karibuni limesitisha utaratibu wake wa awali wa kuajiri askari ambao ni darasa la saba na kujikita kwa askari ambao wana elimu ya kidato cha nne ambapo askari hawa ndio wengi ndani ya jeshi na wamekuwa wakitolewa JKT.

Kutokana na taratibu za ajira zilivyo chini ya Idara ya Utumishi Jeshi la Magereza nalo limekuwa likiajiri wasomi toka vyuo mbalimbali ngazi ya shahada na stashahada kwa lengo la kuwatumia kulingana na taaluma walizonazo kama ambavyo sheria ya utumishi itakavyo, LAKINI hali halisi ndani ya jeshi imekuwa ni tofauti kiasi cha kupelekea kuua taaluma za askari hawa kwani unakuta askari kaajiriwa kama mtaalam wa takwimu au sheria lakini kazi anayoenda kufanya ni kazi ya uhasibu na uboharia, huku mtu aliyesomea uboharia na uhasibu akifanya kazi za sheria kitu ambacho kinaua ufanisi katika idara hii na kupelekea kuishi bila dira huku Serikali ikizidi kuingia gharama kubwa ya kuendesha magereza kwa kulisha wafungwa vyakula hewa.


SUALA MOJA AMBALO MWESHIMIWA RAIS NINGEPENDA ULITAFAKARI KWA KINA NA KULIFANYIA UTAFITI ni kama ifuatavyo;
Mh. Rais katika hotuba yako nilisikia ukiongelea na kulikosoa suala la askari kutaka cheo eti kisa ana degree(shahada) kwa madai kuwa hata mguu upande hajauelewa vizuri kwa lugha nyingine ukimaanisha hata uaskari bado hajaufahamu vizuri.

Mh. Rais Askari hawa wenye taaluma ambao unadai kuwa wanadai vyeo ni askari ambao wanatakribani miaka miwili kazini tangu waajiriwe na wamepta mafunzo ya awali katika chuo cha Magereza Kiwira na kuonekana kuwa wako timamu kwa kazi ya uaskari na hatimaye wakamaliza mafunzo na kutawanywa katika magereza mbalimbali nchini, LAKINI cha ajabu askari hawa mbali na kuwa na elimu ya shahada wamekuwa wakilipwa mshahara sawa na askari mwenye elimu ya kidato cha nne kitu ambacho si sahihi kabisa kwani kinawanyonya na kuwashusha hadhi, huku wenzao wenye viwango vya elimu sawa na taaluma zinazofanana katika idara zingine za majeshi mfano polisi na Jwtz wakilipwa mishahara inayoendana na viwango vyao vya elimu, na hili ni tatizo lililopo kwenye MFUMO WA MISHAHARA ndani ya Jeshi hili la Magereza,
HIVYO askari hawa mpaka kuamua kuomba wapewe vyeo vinavyoendana na viwango vyao vya elimu ni kutokana na sababu ya wao kutaka kupewa mishahara inayolandana na viwango vyao vya elimu na hii ni kutokana na kwamba mfumo wa mishahara ndani ya jeshi hili ni kandamizi kwa askari msomi mwenye cheo cha chini.


Mheshimiwa Rais askari mwenye degree au zaidi ndani ya jeshi mwenye cheo cha lank files anapata mshahara ambao haulandani na kiwango cha elimu yake mfano askari ambaye ni warder(private) mwenye degree anapata mshahara wa Tsh. 400,000/= kwa mwezi kama basic salary, katika hiyo pesa ondoa income tax(PAYE), GEPF, PSPF, LAPF, NSSF au PPF CONTRIBUTION, PRISON SACOSS CONTRIBUTION, alafu uongeze na 15% ya HESLB ambayo tunaamza kukatwa hivi karibuni, kiasi cha pesa ambacho tunabaki nacho mkononi ni kidogo sana ambapo inatia aibu hata kukitaja hapa, Mh. RAIS wakati huo huo sisi askari wako wenye taaluma ngazi ya shahada tukilipwa hivyo wenzetu jeshi la polisi kwa askari ambao ni private wenye elimu kama zetu wamekuwa wakilipwa Basic Salary Tsh. 860,000/=na ikiwa wenzetu hawa tupo nao Wizara moja, kitu hiki kinaleta ukakasi wa ajabu sana ndani ya akili zetu, roho zetu, nafsi zetu na familia zetu.


Tunaomba utusaidie Mheshimiwa Rais kwani suala hili linatuumiza sana, tunalileta kwako kupitia njia hii kwakuwa wakuu wetu kama ilivyo desturi yao si watu wa kuyasemea matatizo yetu aidha kwa kuwa hayawagusi wao au kwa kutokuona umuhimu na huruma juu ya dhuruma hii tunayoipata. Wametuajiri kama wasomi bado taaluma zetu hawazitumii na bado wasitulipe kweli mishahara iliyo stahiki yetu?????!!! Hata mbele za Mungu na Malaika hili suala linaleta ukakasi mno.

Ili kupunguza mzigo wa kazi ya kusoma ujumbe huu naomba nimalizie kwa kukusihi mheshimiwa Rais kuwa utuangalie sisi wasomi wa Jeshi hili ili tuweze kupata stahiki zetu kwani hata professional allowance ambayo ni stahiki yetu na ipo kwa mujibu wa sheria hatuipati zaidi ya kuandika barua kuiomba kila siku huku utekelezaji wake ukiwa ni sifuri na kama idara inaona haiwezi kutulipa mishahara ambayo ni stahiki yetu basi watupeleke utumishi tukapangiwe majukumu kulingana na taaluma zetu katika idara zingine kwani huku hata taaluma zetu zinazidi kuuawa kwani hatuzitumii zaidi ya kudumazwa na maovyo ovyo ya jela.

Namalizia kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wasomaji wote huku nikiamini haya niliyoyaandika yatamfikia mheshimiwa Rais.

Angalizo naomba kama huna hoja ya kushauri usicomment kitu kwani kila kilichoelezwa hapa siyo uzushi bali ni hali halisi ambayo Watanzania wenzako, vijana wenzako, wasomi wenzako wanaipitia ndani ya idara hii ya Magereza.... Rai yangu kwako msomaji paza suti na sisi ili tuweze kusaidia hili jahazi lisizame kwa faida ya kizazi cha leo na kesho kwani kupaza kwako sauti kutasaidia kuwahukumu nafsi na mioyo ya wakuu wetu ndani ya Jeshi waliolala kiupendo, kifikra na kiutendaji kwani wapo kama hawayaoni yanayotusibu. (Itaendelea sikunyingine kuhusu changamoto za jumla ndani ya magereza na upigaji dili unaoendelea kupitia mabwana jela, maboharia, wahasibu, maRPO n.k.

Asante...
 
Kama usemayo ni kweli basi tofauti ya mshahara kati ya wasomi wa vyuo na wengine inatakiwa iwe at least 15% (ile bodi iitafune).
 
Sawa afande wada mwenye digrii kilio chako kimesikika afande kaimu kamishna jenerali Dr.Juma Malewa na wenzake wameshapata taarifa watafanya mabadiliko.
Afande Dr.Juma Malewa fanya mabadiliko kabla hujatumbuliwa walipeni mishahara ya ngazi ya digrii hawa askari wenye digrii hata kama hamtaki kuwapa nyota moja.
 
Magereza wamesahaulika tangu enzi za awamu ya 1......wanaishi kama mashetani awamu zote wanaponea kie chakula cha bure cha wafungwa! Wanaishi kwa mateso sana ila hawana jinsi wafanyeje na hali ni ngumu!
 
umeandika kwa kuhipendekeza kweli kweli,kila paragraph imejaa "muheshimiwa" tatu au nne,unafiki tu umekujaa,hovyo kabisa
Ndugu nashukuru kwa coment yako, ila nafurahi kwakuwa umeusoma ujumbe wangu, naimani kuusoma kwako itasaidia kupaza sauti ili umfikie mhusika... (Natamani ungekuwa unapitia katika bonde hili ili uweze kuzipima kauli zako).....
 
Hii ndio shida ya kufikiri kwa kukayika katika wakija wanataka kura wewe unajiona wa maana kuliko watanzania wenzako baada ya kuwaumiza wenzako unaanza kulilia kuipenda kwako nafsi yako. Tembea katika kweli ya hafsi mwendo lwa sasa ni kupasua majipu bhana bora upende tu usije ukapata predha haya nayo yatapita duniani tunapita njia
 
Kwa makato yote hayo bado ushinde juani na wafungwa hivi kwanini hamjiongezi enyi vijana?!

Piga chini mzigo kakomae na mishe nyingine...
Wewe sio wa kwanza kulalamika na usifikiri kuwa watawala hawajui kilio chenu la hasha ila wanatumia UDHAIFU WENU WA KUTOCHUA MAAMZI THABITI, WOGA WA MAISHA na UZEMBE WA KUFIKIRI.
Tanzania yetu bado BIKRA, THERE ARE MANY OPPORTUNITIES OUT THERE WAITING FOR YOU TO EXPLORE.
Mtalialia hadi lini? HUKO SHULE MLIENDA KUSOMEA UJINGA?
Imagine, umetoil 10+yrs kufukuzia hicho kijishada. Iweje unashindwa kukomaa kibishi kwa lau 3yrs kuboresha maisha yako nje ya utumwa?!
 
Kwa makato yote hayo bado ushinde juani na wafungwa hivi kwanini hamjiongezi enyi vijana?!

Piga chini mzigo kakomae na mishe nyingine...
Wewe sio wa kwanza kulalamika na usifikiri kuwa watawala hawajui kilio chenu la hasha ila wanatumia UDHAIFU WENU WA KUTOCHUA MAAMZI THABITI, WOGA WA MAISHA na UZEMBE WA KUFIKIRI.
Tanzania yetu bado BIKRA, THERE ARE MANY OPPORTUNITIES OUT THERE WAITING FOR YOU TO EXPLORE.
Mtalialia hadi lini? HUKO SHULE MLIENDA KUSOMEA UJINGA?
Imagine, umetoil 10+yrs kufukuzia hicho kijishada. Iweje unashindwa kukomaa kibishi kwa lau 3yrs kuboresha maisha yako nje ya utumwa?!

Kupiga chini kazi sio suluhisho.Ni maneno ya watu waliovimbiwa.Binadamu wa kweli huwa anapambana kuyaweka mazingira yake sehemu salama ya kuishi.Kwa hali ya kawaida ushauri wako ukifuatwa hakuna hata kidato cha nne atakayehimili hayo malipo.
 
Mkuu Poleni sana na natumai Kilio chenu kimefika Mahala husika.
Ingawa Mlitumika sana kwenye uchaguzi mwaka jana (Niliona Mdogo wangu mko nae akivalishwa uniform za Fungua fanta unywe) akipiga picha na ku share kwa Madaha kuonesha hajikubali na kazi yake Maana hajawahi kushare picha akiwa na gwanda la Jela.
Anzeni kujikubali kama ninyi na muache unyonge wenu.
Ninyi ni sawa na Askari wengine.
Ingieni kwa wingi JF na muwe mna shoot mambo yenu.
Yatafika tu Mahala husika
 
Kwa makato yote hayo bado ushinde juani na wafungwa hivi kwanini hamjiongezi enyi vijana?!

Piga chini mzigo kakomae na mishe nyingine...
Wewe sio wa kwanza kulalamika na usifikiri kuwa watawala hawajui kilio chenu la hasha ila wanatumia UDHAIFU WENU WA KUTOCHUA MAAMZI THABITI, WOGA WA MAISHA na UZEMBE WA KUFIKIRI.
Tanzania yetu bado BIKRA, THERE ARE MANY OPPORTUNITIES OUT THERE WAITING FOR YOU TO EXPLORE.
Mtalialia hadi lini? HUKO SHULE MLIENDA KUSOMEA UJINGA?
Imagine, umetoil 10+yrs kufukuzia hicho kijishada. Iweje unashindwa kukomaa kibishi kwa lau 3yrs kuboresha maisha yako nje ya utumwa?!
Wasomi wengi Akili zao zimeishia kwenye kukariri maKARATASI tu
 
umeandika kwa kuhipendekeza kweli kweli,kila paragraph imejaa "muheshimiwa" tatu au nne,unafiki tu umekujaa,hovyo kabisa


Omba Mungu usije kufungwa ukakutana na huyu Jamaa... Hakika atakusulubisha ....lol
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom