Picha: Aliyedhaniwa amekufa kwenye ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jumamosi afunga ndoa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, December 17, 2012


Bwana harusi Emmanuel Mwangosi akiwa na mkewe Magreth Mtebe mara tu baada ya kufunga pingu za maisha jana katika kanisa la Agape jakaranda jijini mbeya


Hii ndiyo ajali aliyopata bwana harusi emmanueli aligongwa na gari aina ya Toyota GX 100 Emmanuel yeye alikuwa anaendesha pikipiki usiku wa kuamkia jumamosi mida ya saa sita nanusu usiku alikuwa anaenda kwenye mkesha kanisani ndiyo ajali hiyo ikatokea maeneo ya mafiati mbeya wengi wa mashuhuda hao walijua mwendesha pikipiki hiyo amekufa papo hapo

Hii ndiyo hali halisi iliyotokea siku hiyo ya ajali mbeya yetu tulifika usiku huo eneo la tukio na kukuta tayari majeruhi wametolewa na kupelekwa katika hospitali ya rufaa Mbeya ndipo jana tukaamua kufuatilia majeruhi hao na kukuta kuwa Emmanueli ameruhusiwa kwa muda akafunge ndoa kwani jana ilikuwa siku ya yeye kuoa ndipo tukaenda kufuatilia harusi hiyo katika kanisa la agape


Bwana harusi Emmanueli na mpambe wake Frank wakiingia kanisani

Hakika ni furaha hapa bwana harusi anamtambua mkewe kwa kumfunua shela kabla ya ndoa kufungwa
kwa picha zaidi bofya read more

Sasa bana na bibi harusi wanaingia kanisani tayari kwa ibada ya ndoa

Mchungaji Emmanuel Mwasota toka E.A.G.T toka DSM ndiyo aliyofungisha ndoa hiyo

Hapa bwana harusi akimvisha mkewe pete huku bibi harusi akiwa katika furaha kubwa na kumshukuru mungu kwa kumuepusha mumewe katika ajali iliyotokea

Hapa wakipata mibaraka ya ndoa kutoka kwa wachungaji mbalimbali wa kanisa hilo la AGAPE

Sasa tu mwili mmoja kitakachotutenganisha ni kifo tu jina la bwana libarikiwe

Bwana harusi akipokea cheti cha ndoa toka kwa mchungaji Mwasota


Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa

Maharusi wakiwa na familia na wazazi wao

Sherehe fupi ya kuwapongeza maharusi ilifanyika katika bustani ya ccm jijini mbeya

Ndugu jamaa na marafiki walihudhuria sherehe hiyo ingawa maharusi hawakuweza fika kwenye sherehe hiyo kutokana hali yake haikuwa nzuri alihitaji kupumzika na kurejea tena hospitali kuendelea na matibabu

Picha na Gwasa wa Mbeya yetu



 


Wow... Unbeliavable kapona kwa KUTEMBEA kwenye AJALI HIYO!!!
Kama kweli SIKU zako HAZIJAFIKA kweli HAZIJAFIKA...
 
Nampa pole sana bwana harusi, na hongereni kwa kufanikisha azima yenuuuuu
 
Ukiiangali hii picha na kama haijawekwa maneno ambayo yana story ya hiyo ajali basi unaweza kuhisi kua jamaa alipata kipigo kutoka kwa huyu mkewe na ndipo wakafunga hii ndoa! Lakini yote ni 9 Mungu ni mkubwa!


DSC00062.JPG
 
Back
Top Bottom