(Picha):Ajali ya lori liliobeba mbolea kupeleka Songea eneo la Lukumbulu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Ajali ya gari imetokea eneo la Lililokaribu sana na mpaka wa Mkoa wa Njombe na Ruvuma.
Kutoka Njombe ni Kilometa 68 tu.
Utaona jinsi wasamaria wakijitahidi kupakua baadhi ya mifuko iliyobaki baada ya lori hilo kupinduka.
Mbolea hiyo ilikuwa ifikishwe Mkoani Ruvuma.
 

Attachments

  • Lory limepinduka.JPG
    Lory limepinduka.JPG
    204.2 KB · Views: 309
  • Lory2.JPG
    Lory2.JPG
    197.7 KB · Views: 257
  • lory3.JPG
    lory3.JPG
    199.5 KB · Views: 179
  • lory4.JPG
    lory4.JPG
    202.2 KB · Views: 142
  • lory5.JPG
    lory5.JPG
    195.1 KB · Views: 166
duh sasa hapo kapindukaje . Mbona kweupe sana harafu barabara pana. Au ndio mambo ya ganzi.
 
narudia tena! madereva wawe makini kipindi hiki!! MUNGU WETU ATULINDE WASAFIRI WOTE, ATUVUSHE SALAMA 2013, AMEN!!
 
KUPE ajali haina peupe wala papana wala pamenyooka ila kwa nyakati hizi umakini kwa madereva wengi umepungua sana na wengi hawako commited na kazi zao! Angalizo: Chondechonde madereva nawaombeni muwe na mda mwingi wa kulala usingizi maana siku hizi usingizi umekuwa chanzo kikubwa cha ajali japo kuwa watu wa usalama barabarani na wadau wengine siwasikii wakiliongelea hilo, na mara nyingi aina za vyakula tunavyokula siku hizi vingi vinauchosha mwili haraka na mwili ukichoka basi hata utendaji wa ubongo huwa afifu matokeo yake ni kupelekea kusinzia pasipokujijua mtu akiwa anadrive, na ndio maana kupe anasema '' mbona kweupe kapataje ajali'' chanzo cha ajali hasa kama hiyo binafsi naamini ni usingizi nachelea kusema hata kifo cha msanii SHARO MILIONEA kilichotokana na ajali mbali na hisia za wanausalama kuwa ni mwendo kasi lkn na mimi naongezea kuwa hata kama kulikuwa na hisia za mwendo kasi basi kuna uwezekano mkubwa Sharo alipitiwa na usingizi, na mbaya zaidi alikuwa peke yake na pia alianza safari alasiri means tayari kachoka na mihangaiko ya mchana kutwa then anakaa kwenye driving seat anaendesha gari umbali zaidi ya km 350 ni lazima apitiwe na kiusingizi na kwa kuwa magari yaenyewe ya siku hizi ni yale ya kutojishughurisha sana na gia (automatic) na ukijumlisha na utulivu wa kuwa peke yako na uchovu wa mchana lazima ubongo ulale! JAMANI MM NI DEREVA TENA MZOEFU NAOMBA MADEREVA WENZANGU JITAHIDINI KUZINGATIA SUALA LA KULALA USINGIZI KABLA YA SAFARI WA KUTOSHA LKN PIA UKIONA DALILI ZA KIUSINGIZI BASI PARK GARI PEMBENI THEN LALA HATA DK 20 ZINATOSHA SANA KUUPUMZISHA UBONGO NA KUWA ACTIVE TENA!!
 
Back
Top Bottom