PICHA: Aibu Kalenga..,LEMA ahutubia watoto.

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Viongozi wa Chadema wamejikuta katika wakati baada ya mikutano yao kupwaya na kujikuta wakihutubia watoto wadogo ambao wamejitokeza kushangaa mvumo wa helkopta. Watoto hao ambao hata hivyo hawakuwa wengi walisikiliza kwa umakini mkubwa viongozi wa CHADEMA hasa Mbunge wa Arusha Mjini Mheshimiwa sana Godbless Lema.

Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiongozwa na Katibu Mkuu wao MHESHIMIWA sana Dr Wilbrod Peter Slaa ambae ameweka kambi Kalenga wamekuwa wakijikuta hawana watu wa kuwahutubia na badala yake kukusanya makundi ya watoto na kuwahutubia.

wakati hali ikiwaendea Kombo viongozi wa Chadema;

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Cham Cha Mapinduzi (CCM) Kaka yangu Geofrey William Mgimwa ameendelea kufanya kampeni zenye kishindo kikuu zikionesha uwezo, nguvu mpya na ari mpya, ambapo katika mikutano yake ya hadhara idadi ya wananchi imekuwa ni kubwa sio kawaida, wakati mwingine hata katika mvua kubwa bado wananchi wamekuwa wakitaka mgombea huyo aendelee kuwahutubia wananchi na wao hukaa kwenye mvua huku wakipata maneno yenye matumaini na mwangaza mpya utakaokuja kung'arisha maisha yao.
 

Attachments

  • IMG-20140311-WA0026.jpg
    IMG-20140311-WA0026.jpg
    124.1 KB · Views: 939
  • wanan.jpg
    wanan.jpg
    70.8 KB · Views: 655
  • wana.jpg
    wana.jpg
    70.5 KB · Views: 624
  • IMG-20140311-WA0007.jpg
    IMG-20140311-WA0007.jpg
    86.7 KB · Views: 699
  • IMG-20140311-WA0005.jpg
    IMG-20140311-WA0005.jpg
    94.4 KB · Views: 667
  • IMG-20140310-WA0047.jpg
    IMG-20140310-WA0047.jpg
    44.2 KB · Views: 684
  • IMG-20140310-WA0026.jpg
    IMG-20140310-WA0026.jpg
    33.6 KB · Views: 690
Embu weka picha ya huyo kaka yako Geofrey Mgimwa akihutubia umati kwenye mvua.
 
We binti una matatz sana...... lini unajifungua?...
hao ni watoto kwa akili ako....... huna ubavu wa kupambna na lema rudi upya
 
Nimeiona hiyo ITV nami imenishangaza kwa Lema kuhutubia watoto labda tu kama sikuona vizuri.
 
wanachonikera chadema ni kudharirisha watoto ? Whats wrong with you ?? Why why why hivi kuna mwanasiasa wa kuvisha watoto wa watu ??????? Acheni hizo bwana
 
Faya kazi za maccm wako, Chadema yaache, wawe watoto wakubwa. Lema kaonyesha nidhamu na busara kuwapa elimu ya uraia watoto.

Chadema tunamini vijana ni taifa la leo
 
wanachonikera chadema ni kudharirisha watoto ? Whats wrong with you ?? Why why why hivi kuna mwanasiasa wa kuvisha watoto wa watu ??????? Acheni hizo bwana
Mwigulu anapotembea na wagongwa wa akili kina Tesha kwako siyo udharirishaji?
 
Mikutano ya CCM ni ya kusomba watu na malori na inaeleweka, uzuri ni wapiga kura wachache wanaangalia TV na ukweli wao uko kwenye mioyo yao.
 
Faya kazi za maccm wako, Chadema yaache, wawe watoto wakubwa. Lema kaonyesha nidhamu na busara kuwapa elimu ya uraia watoto.

Chadema tunamini vijana ni taifa la leo
Duh sijui umerogwa au ni kile kinywaji kikali ambacho babu anataka kihalalishwe hapa nchini,,dah majanga.
 
Mikutano ya CCM ni ya kusomba watu na malori na inaeleweka, uzuri ni wapiga kura wachache wanaangalia TV na ukweli wao uko kwenye mioyo yao.
Mikutano ni ya kusomba watu..??? kama nanyi mnao hao watu wa kuwasomba mbona mnahutubia watoto..?? Sombeni sio mnakodi chopa la mabilioni kisha mnalala CCM inasomba watu.
 
Kweli wewe unaye shida,soma alama za nyakati tambua anachokifanya KAMANDA LEMA,hapo kamwita mtoto na ku-demonstrate kwa wanakalenga kuwa hali waliyonayo chanzo ni ccm,huoni mtoto hana hata yeboyebo na nguo zimechanika chanika. Je Mgimwa(marehemu) toka aingie madarakani amefanya kitu gani kwa Tanzania kukomesha umasikini wa kupindukia kama huo zaidi ya kuwa mzigo? Mtoto naye si anafuata nyayo za mzee? CC:Riz1
 
Tunawaambia kila mara.

Dhambi ya ubaguzi wa kikabila na kidini imeanza kuwatafuna CHADEMA kwa sasa nje ya CHADEMA baada ya kuimaliza ndani.

Huwezi kutoa maamuzi yenye misingi ya kikabila na kidini ukasalimika ndani ya chama. La hasha.

Law of Karma lazima ipitishe makali yake ili ikutafune kwa njia yoyote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom