Picha Adimu Kutoka Maktaba ya Ally Sykes: Mwanamuziki Eduardo Masengo na Julius Nyerere Rais wa TANU 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
''Peter Colmore signed Edouard Masengo the gifted guitarist from Elizabethville, Belgian Congo to promote Coca-Cola.

Masengo had come to Nairobi with a group called Je-Co-Ke meaning, Jean Comedian Katanga.

Colmore who was already in broadcasting was informed that there was a young man in town who played terrific guitar.

Colmore went to the hotel where Masengo was lodging.
There he found Masengo in a dirty hotel at River Road.

He was sitting on the floor playing his guitar with people around him listening to his music.

This was the beginning of the association between Colmore and Masengo.
There was the famous poster of Masengo with his guitar and holding a bottle of Coca-Cola.''

(''Under the Shadow of British Colonialism...'')
Ally Sykes and Mohamed Said

Hakuna siku ambayo itaweza kupita usisikie muziki wa Eduardo Masengo katika radio.

Nalikumbuka tangazo lake akitangaza Coca Cola.

Nilikuwa nikipita Mtaa wa Swahili na Kitchwele (sasa Uhuru) kabla ya kufika Swahili na Stanley (sasa Max Mbwana) upande wa kushoto kulikuwa na duka la Muhindi nje ndipo lilipokuwapo tangazo la Eduardo Masengo.

Nilikuwa navutiwa sana na tangazo lile.

Lile koti la mistari alilovaa Masengo na guitar aliloshika vilivutia akili yangu ya kitoto.

Ally Sykes na Julius Nyerere walikuwa marafiki wakubwa sana.

Masengo alipofika Dar es Salaam alimchukua hadi Magomeni Maduka Sita nyumbani kwa Rais wa TANU Julius Nyerere kwenda kumtambulisha.






 
Back
Top Bottom