Picha 7 za kusisimua zitakazokuacha mdomo wazi

Hiyo picha namba moja kuna account tofauti. Huyo mtoto alikuwa mita chache na ndege inayotoa msaada wa chakula. Mama yake alikuwa ana struggle kupata chakula cha msaada, na hivyo kumwacha nyuma. Ingawa huyo tai alishuka, asingeweza kumla kwa sababu watu hawakuwa mbali. Note ya Kevin Kujiua ilizungumzia mengi:

"I'm really, really sorry. The pain of life overrides the joy to the point that joy does not exist...I am depressed...without phone...money for rent...money for child support...money for debts...money!!!...I am haunted by the vivid memories of killings and corpses and anger and pain...of starving or wounded children, of trigger-happy madmen, often police, of killer executioners...I have gone to join Ken [recently deceased colleague Ken Oosterbroek] if I am that lucky”.

— Kevin Carter in his suicide note
Mkuu kwanza Asante kwa kutuwekea picha pamoja, hata hivyo picha zako ni kubwa kuliko Maelezo ulotoa.

Mfano picha no. 1
Huyo mtoto aliuwawa na huyo Tai anayeonekana kwa nyuma, Japo picha hii ilimpa Tuzo na heshima kubwa Kelvin Carter duniani kote, lakini baada ya siku kadhaa alijiua, na ni baada ya taarifa kutoka kuwa baada ya yeye kupiga hiyo picha na kuondoka, yule Tai alimuuwa yule mtoto, ilhari angeweza kumbeba na kumpeleka mtoto yule kwenye kambi ambayo ilikua umbali wa 1 km toka eneo la tukio!

Picha no. 5
Hii ni moja ya Picha iliyonivutia zaidi, Haihusiani na urafiki hapo, na hata lengo la mpiga picha sio Hilo, picha inawaonyesha watoto wa rika moja, wawili wanaoenda mbele wamevaa sare za shule means ama wametoka shule ama wanaenda, hawa wengine wanatafuta vitu vya kuokota barabarani (Chokoraa), hapa ndo msingi wa maisha unapojengwa....!
 
Hizi picha zimenifanya nimalize mwaka Kwa.kuwaza mengi. Mfano :picha ya Kwanza, ukifanya Jambo ambalo titakuwa linakutesa haswa unaweza chukua maamuzi ya kujidhuru.
 
Usimtakie mabaya mwenzako ndugu yangu, tumuombe mungu ili watu wabadilike Na wawe Na roho nzuri. Huyu mtu leo hii katuonyesha ukweli na hali halisi ilivyo kwenye vita, asingipiga hiyo picha leo hii tusingijua madhara kama hayo kwenye vita. Na lingine hawa wapuga
Nimekusoma Mkuu! Inaumiza sana hata uwezo wa kufikiria haya yote unapotea
 
1.Picha hii ilichukuliwa mwaka 1993 Sudan kipindi cha mapigano huko Darfur hali iliyopelekea njaa Kali maeneo ya Darfur .Aliyechukua picha hii ni Kevin Carter raia wa Africa kusini na April 1994 Kevin Carter alipokea tuzo ya Pulitzer ambayo hutolewa USA kila mwaka kwa waandishi,wapiga picha bora,baada kumpiga picha mtoto Huyo aliyekuwa anaviziwa na Tai.Mara Baada ya kuchukua picha hiyo Kevin alimfukuza ndege huyo na hakutaka kumgusa mtoto huyo "alimwacha hapo alipo na kuondoka" kwa kuhofia ataweza kuambukizwa magonjwa endapo mtoto huyo angekuwa mgonjwa..Bado haijajulikana kama Tai yule alimrudia yule mtoto na kumla au laa

7ca8dd3aac9ce0e6e08c9eed3e234893.jpg


2.Picha hii ilichukuliwa mwaka 2006 ikimuonyesha kijana mdogo wa kike akipambana na wana usalama, "one against many", akipinga unyanganyi wa ardhi yao iliyokuwa irudishwe serikalini

09a0f3bb4fca1530aa6580c1a788369d.jpg



3.Picha hii ilichukuliwa nchini Liberia kipindi cha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.Mji wa Monrovia ulijaa risasi ,kijana huyo akitembea kwenye barabara iliyojaa risasi

5735d761ab70e7ac65bbceab8e2124b6.jpg


4.picha hii ilichukuliwa mwaka 2012 kipindi rais wa china alipotembelea india na muandamanaji huyu wa Tibet alijichoma moto na kukimbia huku akipiga kelele kama ishara ya kupinga mateso ya wa Tibet wanaoyapata huko China lakini polisi wa India walifika mapema na kuzuia maandamano hayo.kijana huyu alimwagiwa maji na kupigwa na nguo na moto ulizimika lakini alifariki

31553e52b18c5672f869cb969054d444.jpg



5.Picha ya watoto wakitembea pamoja na majunia yao wakielekea kwenye mahangaiko huku wakipishana na watoto wenzao wawili wakienda shule

c31f500927a0ef0939959de40b537faf.jpg


6.picha hii ilichukuliwa kipindi cha maandamano huko Burkinabe .Huyo kwenye picha ni mhadhiri wa chuo akipambana na baadhi ya wana usalama

f67f08bc575c74e2cf74fdda6acdb3d7.jpg


7.Picha hii ilipigwa maeneo ya morogoro ,picha inaonyesha wananchi wakimpiga picha majeruhi aliyekuwa anahitaji msaada

ee069c5fadb2e302b8c19a6e5cab12e1.jpg
Mmmh duniani kuna mambo
 
Calvin Carter raia wa Afrika Kusini alijiua ..inasemekana ni kutokana na hiyo picha maana angeweza kuokoa maisha ya huyo mtoto aliyekuwa akisubiriwa na ndege Tai afe ili amle
 
Hiyo namba saba ndiyo utanzania halisi,
Watanzania wenye moyo wa kusaidia ni wachache Sana,

Wengi tunapenda kusaidia kwa sifa ili tuonekane kiunafki nafki!
 
Back
Top Bottom