phone arena awards 2013 (award za simu na vihusianavyo na simu)

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
30,703
39,776
wiki hii yote phone arena wamekua wakitoa award zao. zipo interested sababu wamejaribu kutoa kwenye maeneo tofauti.

1. best phablets
phablet ni simu zenye display zaidi ya inch 5 lakini hazifiki inch 7 hivyo zipo kati kati baina ya smartphone ya kawaida na tablet.


-nafasi ya kwanza ikaenda kwa galaxy note 3 kama best phablet mwaka huu 2013

note-3.jpg


-nafasi ya pili ikaenda kwa lumia 1520
-nafasi ya tatu ikaenda kwa sony experia z ultra

2. best cameraphone
cameraphone hizi ni simu zenye camera nzuri zaidi

-mshindi alikua ni nokia lumia 1020 na camera yake ya megapixel 41

lumia-1020.jpg


-nafasi ya pili ikaenda kwa galaxy note 3
-nafasi ya tatu ikaenda kwa iphone 5s

3. best product design
hizi ni simu/tablet ambazo wamedesign vizuri na zina muonekano wa kuvutia kwa nje

-mshindi ni htc one kwa flagship yake iliotoka mwanzoni mwa mwaka huu

htc-one.jpg


-nafasi ya pili ikaenda kwa ipad air
-nafasi ya tatu kwa iphone 5s

4. best application
hizi ni application bora za smartphone kwa mwaka huu 2013

-mshindi ni nokia camera app ambayo ilileta uwezo wa digital camera kwenye simu

Nokia-Camera.jpg


-mshindi wa pili google dash
-mshindi wa tatu yahoo weather

5. game of the year
haya ndio magame mazuri kwenye smartphone

-mshindi alikua ni asphalt 8 airborne
Asphalt-8-Airborne.jpg


-nafasi ya pili modern combat 4 zero hour
-nafasi ya tatu despicable me: minion rush

6.dissapointment kubwa
hizi ndio tech mbaya kabisa mwaka huu

-mshindi ni htc one na kamera yake mbaya ya ultrapixel yenye megapixel 4

-wa pili ni blackberry na simu zake za bb10
-wa tatu ni smartwatch zote wakiongozwa na galaxy gear

7.best value for money
hizi ni bidhaa ambazo unalipa kidogo unapata kikubwa

-mshindi ni nexus products za 2013 yaani tablet ya inch 7 na simu.

-mshindi wa pili ni motorola g
-mshindi wa tatu ni lumia 520

8.innovation bora
hivi ndio vitu bora vilivyogunduliwa 2013

-mshindi ni coprocessor hizi ni chip za simu ambazo zimekua optimized kufanya task maalumu mfano x8 ya motorola na a7 ya apple

-nafasi ya pili touch id ya apple
-nafasi ya tatu self healing ya lg flex

kwa wale wanaopenda kujisomea zaidi
http://www.phonearena.com/news/PhoneArena-Awards-2013-All-categories_id49988
 
Nimechoka kuona camera ya 4s ni kali zaidi hata ya matoleo ya mbele yake (iPhone 5, 5c & 5s)

kaka sidhani kama apple ni wajinga kiasi waeke sensor nzuri kwenye 4s na kueka mbaya kwenye 5s.

ni review gani umeangalia au umefanya ikaleta result hio kua camera ya 4s ni bora kuliko 5s?
 
kaka sidhani kama apple ni wajinga kiasi waeke sensor nzuri kwenye 4s na kueka mbaya kwenye 5s.

ni review gani umeangalia au umefanya ikaleta result hio kua camera ya 4s ni bora kuliko 5s?

ImageUploadedByJamiiForums1386183957.795615.jpg

Sijafungua hiyo link ila ni sababu ya hiyo namba tatu hapo👆
 
kaka nimechemka mimi ni iphone 5s sikuona na nikadhan pia wewe umesema camera ya 4s ni bora kuliko 5s.

nimeshabadilisha hapo juu

thanx
 
Hivi Nokia wanavyoangaika na hizo camera wanataka kupoteza soko la DSLR cameraz nini? Maana nasikia hiyo 1020 Lumia ina setting za Camera ki-preoffesional kabisa ova zikina Canon DSLR D500..
 
Hivi Nokia wanavyoangaika na hizo camera wanataka kupoteza soko la DSLR cameraz nini? Maana nasikia hiyo 1020 Lumia ina setting za Camera ki-preoffesional kabisa ova zikina Canon DSLR D500..

imechukua miaka 5 toka nokia waanze kuifanyia kazi pureview toka mwaka 2007 mpaka simu ya kwanza nokia 808 kutoka mwaka 2012, hapa utaona jinsi watu walivyojikaza.

na nokia sasa hivi anafanya kazi na pelician na invisage kuna uwezekano mkubwa hio flagship ya nokia mwanzoni mwa 2014 ikawa ya maajabu sana kwenye upande wa camera. na hizi ndio posibilities.

1. camera yenye megapixel zaidi ya million
hawa invisage wanafanyia kazi camera yenye resolution kama ya jicho la mtu ambayo itakua na mamilioni ya pixel. maybe inaweza isifae 2014 lakini huwez jua inaweza kuja.

2.camera inayoona usiku
tayari pureview ya sasa bi best usiku lakini hili halimfanyi nokia aishie hapo. pelician wao wanafanyia kazi sensor itayotumia infrared ili kuona usiku. kama miwani za kijeshi vile uwezo huo unakuja kwenye camera.

3.camera inayoona/kuhisi kitu cha nyuma kilichozibwa.
hawa ni pelician tena na kampuni ya singapore inayoitwa heptagon wanafanyia kazi kamera ya kuona kitu cha nyuma.

4.kufanya flash ifanye kazi
moja kati ya kitu kinachoharibu picha ni flash hasa usiku huwa hazitoki vuzuri. hawa heptagon wasingapore tena wanafanyia kazi hii ishu kwa kutengeneza flash inayotoa rangi mbali mbali ili kubalance rangi za mwanga na muelekeo wa mwanga.

5.kupata maelezo ya picha papo hapo
hii ndio complicate naitaja tu hapa ila inaweza isifanikiwe. tunajua sasa hv picha zinaweza tuambia maeneo, zikawa 3d na mambo mengi sasa kampuni inaitwa luminate inataka kuongeza maelezo mengi kwenye picha kiasi ambacho kinafanya jepg iwe haina kazi na format mpya inatakiwa itengenezwe.

kati ya hizo tano expect mojawapo au zaidi ya moja kuwepo kwenye flagship ijayo ya nokia
 
Back
Top Bottom