Philipo Mwakibinga atoa Siri ya Sakata la Viti Maalum Chadema

pendolyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
524
500
SIRI YA SAKATA LA VITI MAALUMU CHADEMA HII HAPA. MDEE 19 NA SPIKA WANAONEWA BURE.

Na Philipo Mwakibinga
0758910403

Tatizo siyo Mdee 19 bali ni nani anapelekwa baada ya akina mdee kuondolewa. Viongozi waandamizi wa CDM wamepanga kuwa wanataka kupeleka sura mpya kabisa Bungeni na siyo hawa akina Mdee 19. Sababu kubwa ambazo zinafanya ni ileile tabia ya Maslahi Binafsi mbele, chama baadaye.

Baada ya Wabunge Nguli na Viongozi wa CDM kushindwa uchaguzi ndipo, uliibuka mkakati wa kupanga safu ya kupeleka Viti maalumu watakavyo nufaika navyo wao binafsi kwa miaka 5. Hali hii ilipelekea kuanza kwa mkakati wa kutaka kupora haki ya BAWACHA ya kupendekeza majina kwenye CHAMA kwakuzingatia vigezo vya nani awe mbunge na, kwasababu zipi.

Mfano Aliyekua Mbunge wa Iringa kwa upande wake tayari ameapa kumpeleka Mwanaye ili akawe Mbunge kiti Maalumu. Tayari keshaanza kumpigia chapuo hata kwenye media ili aonekane anauwezo. Mwamba kama kawaida yake yeye anao wake na ndugu zake ambao kukosa Ubunge, kwake anaona kama hajatendewa haki kwani kwake imekua kama sheria kwamba lazima bibie mdogo awe mbunge kila baada ya uchaguzi.

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime, yeye anao Wabunge wake mabinti ambao alishakubaliana nao kuwa, kila mmoja akiingia bungeni atalazimika kukopa milioni 300 kisha jamaa anachukua milioni 200 na bidada anabaki na milioni 100 na ubunge wake unakua chini ya uangalizi. Hii ndiyo sababu ya kwamba wanapeleka sura mpyaa kabisa. Unaweza kujiuliza sura mpya kabisa kwa chama kama CDM kule bungeni kutakua na tija!?

Ndipo ukweli unabaki kuwa, kumbe tatizo siyo kwamba CDM haitaki nafasi za viti Maalumu pamoja na kwamba walisema hawatambui ule uchaguzi na kusema kuwa ulikuwa ni uchafuzi hapana, Wanachotaka ni kupeleka majina ya watu wao wengine watakao nufaisha viongozi na siyo Chama.

Katika hili nilazima kwa mpenda Demokrasia yeyote kutetea akina Mdee 19 kwasababu, viongozi wa CDM wanatumia nguvu kubwa kuendelea kuwashambulia ili ionekane hawafai. Hii siyo tabia nzuri na Wanachama wa CDM wanapaswa kujua kiundani hili jambo.

Wanajaribu kumchafua Spika wa Bunge Ili aonekane kawabeba akina Mdee 19 wakati, WAO CHADEMA wanajua kuwa barua yao rasmi ya kupeleka majina ipoTUME YA UCHAGUZI na siku wakienda mahakamani upo uwezekano wa Mahela kuwaumbua ndiyo maana wanahofu kubwa ya kupeleka jambo hilo mahakamani kama alivyokuwa ameahidi MNYIKA.

Kuna madudu mengi sana kwa hawa jamaa. Mfano Wanaitumia vibaya sana BAWACHA ilikujaribu kushinda hiyo vita yao...

Hadi sasa Bado Mdee 19 wananguvu kubwa na kila kukicha jamii inazidi kuelewa ukweli hili nalo ni pigo jingine kwa Team Mnyika mzee wa kulilia viti 19 vya WANAWAKE.

Nitaendelea kuwajuza

Sent from my EVA-L09 using JamiiForums mobile app
 

Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
463
1,000
Ndugai ameidharau Sana katiba, bunge kuongozwa na mgonjwa wa akili Ni tatizo, ashugulikiwe huyu kizee kilichokosa matumaini
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,650
2,000
Ndiyo nani huyo Filipo??
Anatuwekea na simu, ili iweje?
Zama zimebadilika! Uteuzi haupatikani kwa njia hiyo.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,879
2,000
... pumbavu! Ni Chadema walienda kumtoa Nusrat Henje gerezani usiku kisha masaa machache akaapishwa kuwa mbunge? Ujinga ni mzigo kweli kweli. Mods unganisha hii takataka na ile nyingine iliyomo humu JF tangu jana. pendolyimo leo yuko zamu ama hajapata briefing au hakuelewa wenzie LB7 walicho-post jana.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,776
2,000
Tungekuwa tukiweka hoja zetu humu JF tunaweza na picha na anuani ya makazi basi kuna watu wangekuwa wanazomewa mitaani na wengine kukimbiwa na wake zao kwa kuona aibu dume kuwa pumbaf
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,561
2,000
Huyu Mwakibinga ni nani? napenda kumfahamu historia yake kabla sijaanza kujadili huu upuuzi wake.
 

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
1,940
2,000
Huyu mleta mada ni Punda with a very high degree of Pundidity!! Hajui wachina weshaleta butcher za Punda! Mazoea Propaganda za Paschal wa Njaa!
 

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
884
500
Ndiyo nani huyo Filipo??
Anatuwekea na simu, ili iweje?
Zama zimebadilika! Uteuzi haupatikani kwa njia hiyo.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Mwana ACT kwa sasa na X-CHADEMA,alifukuzwa UDOM kwa kosa la kuleta harakati za kisiasa kwa shule mkuu.Kitambo Sana hajasikika,naona Kaja sasa
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
29,475
2,000
Filipo huu uzushi mbona kitambo tu umesemwa lakini wote wenye akili wameuupuuza , maisha yameshakushinda sasa unajaribu kujiuza naona umeweka na namba za simu. Kwa taarifa yako awamu hii hakuna teuzi za kimalaya malaya. Hivi shule ulienda kusomea ujinga? We graduate mzima unataka uishi kwa kubahatisha, Baba yako hiyo hela aliyotumia kukupeleka shule bora angenunua nguruwe afuge kuliko huu upuuzi unaofanya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom