Philip Marmo ameandaliwa wadhifa(cheo) gani baada ya kustaafu ubalozi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Leo hii katika Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma,Raisi Kikwete amemuapisha lut.Shimbo na mteule mwingine kuwa mabalozi ambapo Shimbo ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini China kuchukua nafasi ya Philip Marmo ansestaafu.

Kama mnavyofahamu,Philip Marmo aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini China baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo aligombea ubunge na kama sikosei ilikuwa katika jimbo la Mbulu.Hapa hamna cha ajabu hapa kwani huu ndio utawala wa Kikwete na CCM kwa ujumla ulivyo.Ni utamaduni wao wa kupeana ulaji utazani hakuna watu wengine.Kwakweli inakera na kuudhi sana.

Sasa swali ni kuwa baada ya kustaafu ubalozi mnampa cheo gani(kazi? kingine?

Ukweli ni kuwa katika nchi hii kuna watu wana hati miliki za ajira!
 
Chezea CCM wewe, atapachikwa tu pahala
 
Philip Marmo anaendelea kuwa Balozi lakini kahamishiwa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani

NB:
Watanzania wenzangu tuweni wachunguzi kabla ya kuweka jambo lolote hapa jukwaani.

Leo hii katika Ikulu ndogo ya Chamwino mjini Dodoma,Raisi Kikwete amemuapisha lut.Shimbo na mteule mwingine kuwa mabalozi ambapo Shimbo ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini China kuchukua nafasi ya Philip Marmo ansestaafu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro. Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

Bw. Wilson M. K. Masilingi;
Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora.

Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

Bw. Modest Jonathan Mero, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva. Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang’ka Marmo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.

------MWISH0-----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

12 MEI, 2013
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mabalozi Wapya kujaza nafasi zilizo wazi na kuanzisha Ofisi za Ubalozi nchini Uholanzi na Comoro. Aidha Mheshimiwa Rais amefanya uhamisho wa Balozi kutoka kwenye kituo kimoja.

Mabalozi wateule na aliyehamishwa kituo ni kama ifuatavyo:-

Bw. Wilson M. K. Masilingi;
Ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi. Bw. Masilingi ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, Arusha, (AICC) na aliwahi kuwa Mbunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 1995 – 2010. Aidha, katika kipindi cha mwaka 1998 – 2005 alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais mwenye dhamana ya masuala ya Utawala Bora.

Bw. Chabaka Faraji Ali Kilumanga, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro. Hadi uteuzi huu unafanyika, Bw. Kilumanga alikuwa Balozi Mdogo katika ofisi ya Ubalozi nchini Uingereza.

Bw. Modest Jonathan Mero, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva. Kabla ya uteuzi Bw. Mero alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mwandamizi kwenye Ubalozi wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, New York.

Kadhalika, Mheshimiwa Rais amemhamisha Balozi Philip Sang'ka Marmo kutoka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na kwenda Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.

------MWISH0-----

(John M. Haule)
KATIBU MKUU,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

12 MEI, 2013
majina yale yale......
kama siyo baba.... mtoto.... mjukuu....
hivi majina yetu sisi yatatoka lini? ndo kusema kuna kakundi ambako kamebobea kuongoza nchi hii?
wengine wanamwagwa huku wanapewa kule... wanaharibu huku, wanahamishiwa kule......
hii nchi nakaribia kuichoka sasa
 
Sisi tutaendelea kuwa wananchi watiifu tu...hahahah
ha haaa, nimeipenda hiyo....
ila utiifu unajua utafika mwisho! haiwezekani kila siku wao tu.....
mimi sitaki kuwa huko juu lakini natamani siku nisikie majina mengine. mbona haya yameshajirudia sana? hawazeeki hawa watu?
 
Ndio maana naunga mkono kupunguza madaraka ya Rais ili huu upuuzi usiendelee.Lini Na mimi nitatajwa kwenye nafasi hizi kama kila kukicha ni wale wale hata kama walishindwa mahali na kuharibu kabisa idara.
 
Philip Marmo anaendelea kuwa Balozi lakini kahamishiwa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani

NB:
Watanzania wenzangu tuweni wachunguzi kabla ya kuweka jambo lolote hapa jukwaani.

Well done mkuu, hili jukwaa siku hizi limekuwa kama jalala la kariakoo, kila mtu mwenye uchafu wake anatupia humu bila hata kutumia akili kidogo kufanya utafiti. Jukwaa limepoteza hadhi kabisa na halina heshima tena kama ile ya zamani.
 
Katiba mpya imeongelea hili suala la uteuzi wa mabalozi?
Au sio suala la muungano?
 
Well
done mkuu, hili jukwaa siku hizi limekuwa kama jalala la kariakoo, kila
mtu mwenye uchafu wake anatupia humu bila hata kutumia akili kidogo
kufanya utafiti. Jukwaa limepoteza hadhi kabisa na halina heshima tena
kama ile ya zamani.

maneno ya mpumbavu toa vivid,shauri, ukilaumu haujengi lazma tuseme kurithishana nchi yetu tumeshachoka
 
Well done mkuu, hili jukwaa siku hizi limekuwa kama jalala la kariakoo, kila mtu mwenye uchafu wake anatupia humu bila hata kutumia akili kidogo kufanya utafiti. Jukwaa limepoteza hadhi kabisa na halina heshima tena kama ile ya zamani.
Ulichosema hapa hakibadili hoja ya msingi licha ya kukosea kwangu katika hii jambo.Nchi hii kuna ukoo unaoitwa "CCM grade one members" wanaotawala nchii hii.Wengine kazi yenu kuwapigia debe kwa ujira kiduchu!
 
Philip Marmo anaendelea kuwa Balozi lakini kahamishiwa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani

NB:
Watanzania wenzangu tuweni wachunguzi kabla ya kuweka jambo lolote hapa jukwaani.
mkuu nimecheka mpaka bas yaaani duuh
 
labda atapelekwa tacaids soon ama miradi mingine kama tasaf nk.....kwi kwi kwi nani kamwaga pombe yangu nauliza sioooo mimiiii eeeee siooo mimiii eeeee@@@@
 
Mimi nina mpango wa kuongezea jina mbele...kuanzia sasa naitwa watu8 N'kapa hiyo itarahisisha kwa mimi kupewa kitengo nyeti muda si mrefu...

ha haaa, nimeipenda hiyo....
ila utiifu unajua utafika mwisho! haiwezekani kila siku wao tu.....
mimi sitaki kuwa huko juu lakini natamani siku nisikie majina mengine. mbona haya yameshajirudia sana? hawazeeki hawa watu?
 
Alikuaga mbunge wa Mbulu aise,alisema tumchague miaka 5 iliyobakia wakati binti yake anamalizia masomo ili amwachie kiti,kauli zake ndo zilizompeleka China na sasa Ujerumani ubunge ukamtoka
 
Back
Top Bottom