Philip Mangula: Wale wote walioshinda kwa Rushwa watashughulikiwa ndani ya Miezi 6 kuanzia sasa

Nimemsikia mwenyekiti wa ccm bara akinadi sera hii kwangu mimi huu ndio mwisho wake utamtoa nani na utamuacha nani kwa hili labda wenzangu nambieni kaulio hii ni ya kweli au yaleyale ya kuvua gamba.
"Barking Dogs Seldom Bites"
Msitegemee mapya hapo.
 
Wakati kikwete anaingia kugombea kwa ufisadi mkubwa ambao haujawahi kutokea kwenye nchi hii, mangula alikuwa katibu mkuu wa chama. Kama yeye ni makini kwa nini ndani ya miezi sita hii aliyotangaza asianze na mwenyekiti wake aliyeasisi mtandao wa kifisadi? Pia, wakati chama kinachukuwa mabilioni ya epa ndiye alikuwa katibu mkuu. Kwa nini asitoe majibu ya mambo haya kwanza kabla ya kuanza na porojo za miezi sita kusafisha chama?
 

Wednesday, November 28, 2012

headline_bullet.jpg
Asema wamepokea malalamiko mengi mno
headline_bullet.jpg
Watawafanya kama wale 31 wa mwaka 2000


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, amesisitiza kuwa chama hicho hakitakuwa na suluhu wala huruma na mgombea yeyote aliyeshinda kwa njia ya rushwa na kwamba kitatengua matokeo pindi itakapothibitika kwamba ushindi ulipatikana kwa njia hiyo.

Amesema chama kimekwisha kupokea malalamiko mengi ya wanachama wake kuhusu rushwa ilivyotawala kwenye uchaguzi na kwamba kwa sasa wanayachambua.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mangula alisema chama hicho hakitamwonea huruma mshindi yeyote aliyepata nafasi ya uongozi kwa njia ya rushwa katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni.

"Tumepokea malalamiko mengi sana. Hivi sasa yanaendelea kuchambuliwa; uchambuzi ukimalizika tutatuma timu ya kwenda kuona hali halisi ambayo italeta ripoti kwenye kamati ndogo ya maadili ambayo mimi ni Mwenyekiti wake," alisema.

Alisema suala la rushwa ndani ya chama hicho halihitaji hata nguvu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), bali ni ‘political management' (utawala wa kisiasa) kumaliza tatizo hilo, kwa kuwa siyo jinai.

Mangula alisema: "Kwa hiyo timu yetu itakwenda kuangalia haya malalamiko ni ya kweli? Nani alifanya nini. Hatupeleki timu moja, baada kukabidhiwa na kamati yangu kupitia ripoti, tunaipelekea Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC-Nec), ambayo itafanya maamuzi."

Alisema ikithibitika kuna mtu alishinda kwa rushwa, matokeo yatatenguliwa na uchaguzi kurudiwa hata kama ni washindi wa nafasi za ujumbe wa Nec.

"Kama mtu anajijua aliingia kwa rushwa atanyang'anywa ushindi, yaani matokeo yatafutwa na uchaguzi utarudiwa. Na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni zetu za uchaguzi," alisema.

Kuhusu taarifa za kuwapo kwa rushwa ndani ya CCM kwa muda mrefu na uwezo wake wa kuiondoa, Mangula alisema atafanya kazi kwa kuzingatia kanuni na pia atashughulikia malalamiko yatakayolewa kwa sababu lazima kuwapo kwa malalamiko rasmi.

Kuhusu rushwa ya mtandao ambayo inadaiwa kuibuka ndani ya CCM, Mangula alisema haifahamu kwa kuwa wakati tuhuma hizo zinaibuka, alikuwa shambani kijijini kwake akilima.

Mangula alisema chama hicho kitatekeleza uamuzi huo kama ambavyo kiliwahi kutengua matokeo ya uchaguzi mwaka 2000, walipoengua wagombea 32 waliokuwa wameongoza kwenye kura za maoni.

Alisema mwaka huo, CCM kilitengua pia matokeo ya majimbo matatu ya uchaguzi ambayo ni Morogoro Mjini, Singida Mjini na Bukombe.

Alisema kazi hiyo itafanyika ndani ya miezi sita kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la mwaka 2012 kifungu cha 33 (2) na (4), cha miiiko ya kuzingatiwa wakati wa uteuzi na uchaguzi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kifungu cha 33 (2), kinaeleza kwamba ni mwiko kwa mgombea au kiongozi yeyote kutoa au kupokea rushwa na kwamba ikithibitika ametumia rushwa kupata nafasi husika atapokonywa ushindi.

Kadhalika, kifungu hicho kinaeleza kwamba mtu huyo atazuiwa kugombea uchaguzi mwingine wowote kwa muda utakaoamuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM au atapewa adhabu kubwa nyingine zaidi ya hiyo kama itakavyoamuliwa na kamati hiyo.

KUUNDA MITANDAO
Kifungu cha 33 (4) kinaeleza zaidi kwamba ni mwiko kwa kiongozi au mwanachama yeyote wa CCM kuunda vikundi visivyo rasmi ndani ya chama au kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chini chini kinyume cha ratiba ya uchaguzi na taratibu rasmi zilizowekwa.

Hata hivyo, Mangula hakutaja kiasi cha malalamiko ambayo yamepokelewa na chama wala hatua ya uchambuzi ilikofikia.

Msimamo huo wa Mangula umekuja siku chache tangu kumalizika kwa chaguzi za ndani za CCM ambazo zililalamikiwa na baadhi ya makada kwamba baadhi ya walioshinda walitumia kiasi kikubwa cha fedha kununua kura.

Miongoni mwa chaguzi zilizolalamikiwa ni katika baadhi ya wilaya na mikoa, lakini zaidi zile za jumuiya za chama hicho; Umoja wa Wanawake (UWT), Umoja wa Vijana (UVCCM) na Jumuiya ya Wazazi.

Itakumbukwa kuwa ni kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, alisema waziwazi wakati akifunga mikutano ya UWT na Wazazi na wakati wa kufungua ule wa UVCCM kwamba vitendo hivyo vitakipeleka chama hicho kubaya ikiwa havitakomeshwa.



CHANZO: NIPASHE
















 
tangu ulipochaguliwa uliahidi wote waliopata madaraka kwa rushwa mnawajua na baada ya miezi sita wataondoka wote, mchakato ukoje mh...?
 
Hakuna lolote analoweza kufanya. Hizo zilikuwa ni bla bla za furaha ya kuukwaa ulaji. Kwa akili yake anadhani miezi 6 ni mingi itakwisha halafu ataanza kujiuma uma kama huyu hamnazo Nepi. Hao anaotaka kuwaondoa ndio waliomuweka hapo, sasa atawaondoaje bila yeye kuondoka kwanza? Afadhali ameanza na gia ya kuoa kwanza! Kiongozi mtendaji huwa hatangazi bali utaona vitendo tu. Ukiona kiongozi anabwabwaja na ahadi kibao ujue kesha shindwa hata kabla hajaanza! Amuuelize Jk wale jamaa wa EPA na majina ya wauza unga. Naye alinza kwa mbwe mbwe hizo hizo. Lakini sasa yuko kimya kama aliye ndani ya jeneza! Time will tell!
 
Wanajitahidi kuipotezea ishu hii kwa kuwaweka watz busy na mambo ya kijinga lakini CCM mtwambie magamba part2 vipi ?????
 
Kwani miezi sita haijaisha au atakuja kudeal nao baada ya kufunga ndoa???
 
alipogombea uwenyekiti wa ccm mkoa wa iringa na kushindwa alitamka kwamba ameshindwa kwa sababu ya rushwa.hatimae akafutwa machozi kwa kupewa usaidizi wa mwenyekiti taifa.akakumbuka machungu ya kuukosa uwenyekiti mkoa na kutangaza kuwashughurikia wale wote waliopata uongozi kwa rushwa tena ndani ya miezi 6 tu.je haijafika!? Au kasahau.
 
njaa jamani ni mbaya,yaani njaa inayozidi uzalendo ni mbaya huyu mimi siku ile nilimwona mapengo afya mbaya vile muda mrefu hata uisi ilikuwa tabu. anaahidi kuwaadabisha watu wanakunywa juisi miaka yao yote nilishangaa sana
 
Dah jf ni kiboko ya wasaulifu....watu mnajua kufukunyua...yaani manyinyiemu yotee ni matapeli ya ahadi kuanzia chini mpaka juu hakuna anayetoa ahadi za ukweli....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom