Philip Mangula: Wale wote walioshinda kwa Rushwa watashughulikiwa ndani ya Miezi 6 kuanzia sasa

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
Nimemsikia mwenyekiti wa ccm bara akinadi sera hii kwangu mimi huu ndio mwisho wake utamtoa nani na utamuacha nani kwa hili labda wenzangu nambieni kaulio hii ni ya kweli au yaleyale ya kuvua gamba.
Makamu Mwenyekiti wa CCM ameapa kwamba Ndani ya Miezi sita wale wato walioshinda kwa Rushwa na wale walio kuwa wakitumwa kupeleka Bahasha za Rushwa wafukuzwa ndani ya CCM, na amedai hawahitaji ushahidi wa TAKUKURU wala Polisi,

Hii inatukumbusha Programa ya Kujivua Gamba iliyo pewa siku 90 na matokeo yake sasa ni miaka zaidi ya miwili imeisha

source ITV habari saa mbili
Habari yenyewe ndo hii hapa chini:

19th November 2012

Mangula Aja na Gia Mpya

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philip Mangula, amerejea na gia mpya katika uongozi wa chama hicho huku akiahidi atawang'oa viongozi walioingia katika uongozi wa kwa njia za mkato.

Mangula, ambaye aliondoka katika nafasi ya Ukatibu Mkuu mwaka 2007 baada ya kuishika kwa miaka 10, alisema jana kuwa hana kundi lolote analoliunga mkono ndani ya Chama hicho hivyo atahakikisha viongozi wote waliopata madaraka kwa njia za hovyo hovyo katika uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, wanang'olewa na kubakiza waliopata nafasi hizo kwa njia za halali.

Amesema baadhi ya wanachama wa CCM katika uchaguzi wa chama hicho uliohitimishwa wiki iliyopita, walinunuliwa kama sambusa na watu wachache wenye fedha ili wapange safu zao na kwamba ndani ya miezi sita, kila kitu kitajulikana na atafanya hivyo bila kumuonea mtu wala kumuogopa.

"Mimi nilikuwa nalima nyanya na mapalachichi huko kijijini kabla ya kuombwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ili kukisaidia Chama hiki kukitoa hapa kilipo kwa kuwa rushwa imekithiri ndani yake na kazi hii nitaifanya na kuikamilisha ndani ya miezi sita kuanzia sasa," alisema katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa lengo la kuwapongeza viongozi wapya wa juu wa chama hicho.

"Malalamiko yapo kwa ngazi mbalimbali za Chama, nimeyakuta mezani kwangu, ndani ya miezi sita itajulikana na walioingia kihalali wataendelea, walioingia hovyo hovyo watatupwa nje," alisema.

"Viongozi wameingia kwa rushwa na hii nimeipenda na nitaifanyia kazi vizuri sana bila ya kumuonea mtu na kumuogopa mtu yeyote ndani ya Chama chetu ili kurudisha heshima yake," alisema.

Pamoja na Mangula kuahidi kupambana na rushwa, safu iliyomaliza muda wake akiwamo aliyekuwa Katibu Mkuu, Wilson Mukama na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa, waliahidi kuwa wangewawajibisha makada wenye tuhuma za rushwa kupitia dhana ya kujivua gamba, lakini walishindwa.

Akihutubia mamia ya wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikiri kwamba chama hicho kwa sasa kimepoteza mvuto na kina taswira mbaya kwa jamii.

Rais Kikwete alisema njia pekee ya kurudisha heshima ndani ya CCM, ni kutafuta majawabu ya matatizo yaliyokifanya chama hicho kiwe na taswira mbaya na huo ndiyo ukweli.

"Mkigundua chama cha siasa hakiungwi mkono na watu wengi kama ilivyo sasa, lazima tujiulize na kutafuta majawabu hali hiyo imetokana na nini ili kupata fursa ya kujirekebisha na kukijenga," alisema.

"Kuna watu hawataki kukubali ukweli huu kwamba CCM kimepoteza mvuto kama kilivyokuwa zamani, lakini huu ndiyo ukweli na kazi iliyo mbele yetu ni kukijenga kupitia mradi maalum ambao umeanzishwa na Chama hiki kwa sasa," aliongeza Rais Kikwete.

Alisema kazi ya kukisafisha Chama itafanyika kwa muda wa miezi mitano kuanzia sasa na mageuzi ya kukibadili yameainishwa vizuri kinachotakiwa ni utekelezaji madhubuti.

Alikitaka chama hicho kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara ili kuzungumza na wananchi kama wanavyofanya wenzao wa upinzani badala ya kuacha wananchi waendelee kuwa na maswali mengi bila ya kupata majibu ya matatizo yao.

"Vyama vya siasa kazi yao ni kutupiga madongo sasa kama tutakaa kimya muda wote hatuwezi kupona, viongozi wa CCM mna mashangingi kwa nini msiyatumie kwenda kwa wananchi?" Alihoji Rais Kikwete.

Alisisitiza kwamba kazi ya kukijenga chama hivi sasa ni `mwendo mdundo na nginja ngija' lengo lake kubwa likiwa ni kukijenga Chama na kurudisha heshima.

KAMATI KUU JANUARI

Kuhusu uteuzi wa wajumbe wa Kamati Kuu (CC), Rais Kikwete alisema kazi hiyo itafanyika Januari, mwakani.

Alifafanua kuwa Chama kimetoa muda huo ili kuangalia wasifu wa kila mjumbe anayestahili kupata nafasi hiyo.

Awali akimkaribisha Mangula katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahman Kinana, alisema kuna kundi la wanachama wachache wananunua uongozi ili kupanga safu zao na kwamba muda wa kuwatimua umefika.

CHANZO: NIPASHE
 
Huyu mzee asitafute sifa za kijinga,kwa hiyo yeye ndiyo anayewajua waliochaguliwa kwa rushwa na si TAKUKURU wa Mahakama!teh teh teh!
 
Haya maigizo tumeshayazoea.
Hivi zile siku 90 za kujivua gamba zimeishia wapi??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huyu mzee kaanza kuzeeka akili kama ni jasiri anzie kwa mwenyekiti wa chama cheke
 
Katibu mkuu wa CCM wa zamani na Makamu wa CCM taifa Philip Mangula, ameahidi kuwashughulikia viongozi wote waliochaguliwa CCM kwa rushwa kwa kuwafukuza ndani ya miezi sita. Ameongea leo Dar katika mkutano wa hadhara wa kupongeza uongozi wa juu wa CCM kwa kuchaguliwa.

Namkumbuka katibu aliyepigwa chini bwana Mukama jinsi alivyokuja na moto wa kuvua gamba, kumbe gamba ni yeye mwenyewe. Miezi sita siyo mbali, ngoja tuone mfupa uliomshida fisi kama atauweza
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM ameapa kwamba Ndani ya Miezi sita wale wato walioshinda kwa Rushwa na wale walio kuwa wakitumwa kupeleka Bahasha za Rushwa wafukuzwa ndani ya CCM, na amedai hawahitaji ushahidi wa TAKUKURU wala Polisi,

Hii inatukumbusha Programa ya Kujivua Gamba iliyo pewa siku 90 na matokeo yake sasa ni miaka zaidi ya miwili imeisha

source ITV habari saa mbili
 
source habari tbccm,ningemshauri mangula atulie arudishe maisha yake kwenye mstari jk ni msanii sana anawaingiza watu chaka tu,alianza na mkama saiz yuko wapi? nape katulizwa,msekwa,nw naona kahamia kwa mangula na kinana.
 
Asipokuwa makini huyu watampoteza kwenye uso wa ardhi.
Kazi anayotaka kujipa ni kubwa mno.
 
Wenzie wamemulengesha nae akaingia kichwa miguu na mikono, angemuuliza mukama kwanza!
 
Baadaye tutamsikia Nape akisema "...'waliohamia CHADEMA' ni miongoni mwa viongozi waliochaguliwa kwa rushwa C.C.M., na bado wapo wengine; tutawatoa tu"
 
Wenzie wamemulengesha nae akaingia kichwa miguu na mikono, angemuuliza mukama kwanza!

Namuonea huruma huyu mzee amabye hata shati la kubadilisha alikuwa hana uwezo nalo, leo kaingizwa mjini nae kaingia, ccm yake ya 2004 si hii ya leo ataanza kutofautiana na mwenyekiti kesho asubuhi ndipo atajua kuwa CCM si chama tena ni kokoro. namshauri tu asilewe pesa ya kunyoa ndevu na kununua shati jipya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom