Phila Ndwandwe: Binti mwenye akili kubwa aliyechagua kufa kuliko kumtumikia Kaburu!

FROWIN

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
213
84
*Binti Phila Ndwandwe: Akili Kubwa aliyochagua kufa kuliko kumtumikia Kaburu!*

Kwa nini usife?
Ukifa utaacha nini?
Maswali ya namna hii hujiuliza watu wema

Denis Mpagaze

Kipindi cha Ubaguzi wa Rangi Afrika ya Kusini, mwanadada Phila Ndwandwe alikataa kuishi katika jamii ambayo mwenyeji aliishi kama ngedere na mgeni kama malaika, mgeni alikuwa huru kuua na mwenyeji huru kufa, jamii ambayo mwenyeji alipangiwa cha kusema na mgeni alipanga nani aseme nini, lini, na wakati gani, jamii ambayo mgeni alifikiri kwa niaba ya mwenyewe na mwenyeji alitenda kama msukule. Phila akaamua kungia msituni kumpinga kaburu kwa vitendo, akatendwa vibaya, wakamkata matiti, wakamtoboa macho, wakampiga risasi akafa na kuacha mtoto wa miezi miwili akililia nyonyo! Phila alikufa kishujaa, je na wewe unasababu ya kufa? Ukifa utaacha nini?

Habari za apartheid kila mtu anazijua, lakini mashujaa walijitoa kupambana na apartheid si kila mtu anayajua,hasa kama ulikuwa busy kuchora grasshopper shuleni! Mbali na Nelson Mandela aliyefungwa jela miaka 27 na Steve Biko aliyefia gerezani kwa kipigo, ni huyu shujaa wa kike; Phila Ndwandwe . Mwaka 1985 ,huyu binti akiwa chuoni alijiunga na Umkhonto we Sizwe yaani Mkuki wa Taifa, kikundi kilichoanzishwa na akina Mandela baada ya lile tukio la mauaji ya Sharpeville. Lengo ilikuwa ni kwenda kuwachoma mkuki makaburu! Baada ya kuanzisha kikundi hicho Mandela alitupwa jela. Walimfunga Mandela la fikra zake ziliendelea kuchipuka mpaka watoto wa juzi kama kina Phila wakazisimamia.

Makao makuu ya Mkuki wa Taifa yalikuwa Swaziland kwa sababu makaburu walitangaza hicho ni kikundi cha ugaidi hivyo kila aliyejulikana alikuwa halali yao. Hata Phila na wenzake walikua arrested. Phila akaachiwa kwa masharti ya kuwa kibaraka wa makaburu. Akawa amepata mwaya wa kukimbilia Swaziland kuwajoin wenzake. Akiwa SwaziIand, Phina alikwenda kula mafunzo ya vita vya msituni huko wa Angola kwa Savimbi na kurudi kuliamsha dude! Aliongoza mashambulizi mengi ya vituo vya polis na kuchukua silaha na pesa! Binti akawa tishio kwa makaburu Afrika na Duniani kote! Aliwapunguza usipime!

2256543_FB_IMG_1577696487308.jpeg

Phina alikuwa binti mahiri kuanzia msituni mpaka chumbani. Ujasiri wake, akili zake na urembo aliojaaliwa vilimvutia bosi Bheki Mabuza, kada mwezake wakaishi pamoja na mwaka 1988 walipata mtoto wa kiume, wakamuita jina lake Thaban yaani Gift of God. Phila alibeba mtoto mgongoni, bunduki begani na mume kifuani kuonyesha yeye ni mwanamke shupavu tena wa kiafrika. Mwanamke wa kifrika ni maarufu kwa kubeba mtoto mgongoni, mzigo wa kuni kichwani, kidumu cha maji mkononi, mimba tumboni na nyuma yake ni baba akimfuata nyuma taratibu! Haya yako vijijini, mjini ni ubakaji wa haki za binadamu. Phila hakusubiri awezeshwe ndipo aweze! Siku hizi wako busy na insta, wahtsapp haivutii sana, chips kuku na bongoflava, wakisubiri kuwezeshwa. Ajabu!

Siku moja Phila aliaga kwenda mkutanoni ndo ikawa ntolee! Hakurudi tenaaa! Ilikuwa 1988 hiyo. Kumbe alitekwa na magorila wenzake walioungana na makaburu na kupelekwa Kwazulu Natal kufa. Kutoweka kwake kukawa njaa kwa mtoto wake aliyelia nyonyo, huzuni kwa baba kukosa mke, simanzi kwa wazazi kupoteza mtoto na pengo msituni kumkosa kamanda. Kuna wakati wazazi wake walipokea taarifa za mtoto wao kwamba alikimbilia Tanzania. Pamoja na kuishi kwa matumaini wakimsubiri mwanao walikuja kuambulia fuvu liliotoboka kwa risasi.

Ilikuwa hivi. Mandela alivyoukwaa urais wa South aliendesha nchi kwa samehe saba mara sabini. Aliishangaza dunia. Hata mimi alinishangaza mpaka nikaamini kumbe si kila binadamu alitoka mavumbini, wengine walishuka moja kwa moja kutoka mbinguni. Yaani mtu umefungwa jela miaka 27, umepigwa baridi mpaka ukapata kifua kikuu, familia yako ikavurugika, mke wako wakaoa halafu eti unasamehe! How? Walahi Mandela hakuwa binadamu wa kawaida.

Siku moja polisi alimtandika teke takatifu, Mandela akaanguka chini, akainuka huku akijifuta mvumbi halafu akauliza ,vipi kiatu chako hakijaharibika? Pamoja na kuambiwa visasi ni kazi ya Mungu lakini kwanza ndiyo tunaongoza kwa visasi!

Kupitia tume ya UKWELI NA MARIDHIANO aliyoianzisha Mandela wahalifu na waliokimbia nchi walianza kurudi.Walipewa nafasi ya kutubu na kusamehewa. Naposema kutubu nadhani unanielewa. Unataja dhambi zako zote! Ni kupitia tume hiyo wale askari waliomuua Phila walijitokeza hadharani, wakaungana na wazazi wa Phila, maafisa wa serikali, yule mtoto wa Phila aliyeachwa akiwa na miezi miwili sasa alikuwa na miaka nane, wakaelekea Phina alikofukiwa. Wakati muuaji anachimba kutafuta mabaki ya Phila alisema, “She was very brave, very brave.”

Anasema pamoja na mateso yote waliyompa Phila kamwe hakusaliti mtu. Walivyoona hakuna jibu wakaamua kumuua tu. Wauaji walisimulia walivyomvua nguo Phila, wakampiga Phila, wakamtoboa, wakamkata matiti Phila, wakamtoboa macho Phila, wakamchimbia kaburi Phila, wakatupia kaburini akiwa hai Phila, wakampiga kitu kizito kichwani Phila, akapiga magoti Phila, wakampiga risasi ya kichwa Phila, wakamfukia Phila, wakamtupia na chupa za bia walizokuwa wanakunywa, Phila akalala Kaburini. Mama wa Phila machozi yakamdondoka na kusema, “Tulimsubiri sana mtoto wetu tukijua atarudi kumbe alikuwa hapahapa akiteseka namna hii? Na akazikwa karibu na tunapoishi tusijue? Wala hata fununu kweli?

Mabaki ya Phina yalionekana akiwa amejifunga plastic begs kuzunguka kiuno kuonyesha liheshimu na kujali mali za mume wake. Katika zile siku kumi za mateso, Phili alivuliwa nguo zake zote, akabaki uchi wa nyama, binti wa miaka 23 tu uchi mbele ya wavuta bangi. Hivi kweli yalimuacha salama hayo majitu? Aliteseka sana binti yule lakini kamwe hakutoa siri. Aling’atwa na mbwa lakini hakutaja, walimwaga makaa ya moto Phina akakanyagishwa lakini hakuwataja magorila wenzake. Binti alipitia mateso! Mwenzangu mumeo anarudi usiku wa manane unatangaza kwamba unapitia mateso. Hivi mateso unayajua au unayasikia? Siyo kila mwanaume anayerudi usiku ametoka Sodoma na Gomorah, wengine wametoka kusaka pesa ili upendeze. Sifa ya mwanamke kupendeza, mwanaume kazi. Acha siku hizi ambapo vijana kuombaomba vocha kwa wadada badala ya kupiga kazi, mtaolewa.

Wauaji wake wasamehewa. Tarehe 12 mwezi Machi 1997 taifa zima la Afrika Kusini liliungana katika ibada ya kuzika upya mabaki ya mwili wa Phila huko KwaZulu Natal, kwenye shamba la Elandkop walikozikwa mashujaa wengine. Nelson Mandela alikuwepo na alisimama nyuma ya mtoto wa marehemu.Kupitia msamaha wazazi wa Phila walionana na mjukuu wao na Mandela akasema hicho ndicho nilichomaanisha nilipoanzisha tume ya msamaha. Waliopotezana wakutuna, wagange yajayo! Tazama ilivyo vema na kupendeza ndugu wakikutana na kukaa pamoja.

Mwaka 1960 serikali ya kikaburu ya Afrika Kusini ilifanya mauaji ya halaiki kwa raia wasio na hatia waliokua wanaandamana kupinga udhalimu wa serikali hiyo kwa watu weusi. Mauaji hayo maarufu zaidi kama 'Sharpeville Massacre' yalitokea March 20, katika Mji wa Sharpville, ambao leo unajulikana kama Gauteng.

Baada ya mauaji hayo Chama cha ANC kiliamua kubadili mbinu ya mapambano, kwa sababu njia zote za kudai haki kwa amani zilifeli. Njia ya mazungumzo, maandamano na migomo hazikufaa tena katika kudai haki.Serikali ya kikaburu ilizuia watu wasiseme, wasifanye mikutano ya kisiasa, wala maandamano. Hakukua na uhuru wa vyombo vya habari wala uhuru wa maoni.

Yeyote aliyetoa maoni yasiyoifurahisha serikali aliishia gerezani ama kupotezwa.

Walioandamana walipigwa risasi na kufa. Serikali haikujali.

Kwahiyo, ANC wakaamua kubadili mbinu. Wakaunda kikundi cha kupigana msituni kiitwacho uMkhonto we Sizwe (MK), neno la kizulu lililomaanisha 'mkuki wa taifa'.Haraka sana serikali ya kikaburu ikatangaza kuwa kikundi hicho ni cha kigaidi na ikakipiga marufuku.

Ikawakamata viongozi wa ANC akiwemo Nelson Mandela na Walter Sisulu na kuwasweka jela kwa tuhuma za kuanzisha kikundi cha kigaidi.

Walikamatwa usiku wa tarehe 11 July, mwaka 1961 huko Rivonia, shambani kwa Muisrael mmoja aitwaye Arthur Goldreich aliyekua akiwafadhili ANC kwa siri. Goldreich naye 'alisukumwa ndani' pamoja na kina Mandela.

Baada ya kukamatwa Mandela aliwaambia wafuasi wake wasikate tamaa, waendelee na mapambano.

Alitumia maneno ya kizulu 'Ngethemba ngoba kusasa' ambayo tafsiri yake kwa Kiswahili alimaanisha 'kesho kuna matumaini zaidi kuliko juzi au jana. Kwa lugha rahisi ni sawa na kusema 'KESHO NI NZURI KULIKO JANA'Kikundi cha MK kiliendeleza mapigano dhidi ya serikali dhalimu ya makaburu.

Mapigano hayo yalichukua muda mrefu sana. Wakati Mandela akisota gerezani, kikundi hicho chini ya uongozi wa Muzi Ngwenya kiliendeleza mapambano kikiweka ngome yake huko Swaziland.'Kili-recruit' na 'kutrain' vijana kwa ajili ya mapambano.

Mmojawapo ni mwanadada Phila Ndwandwe aliyejiunga na MK mwaka 1985.

Alikua miongoni mwa wanawake wachache waliokua wapiganaji katika kikundi hicho.

Alishiriki kupigana vita vya msituni kuondoa utawala dhalimu wa kikaburu. Aliamini jukumu la ukombozi halikua la wanaume peke yao, bali la kila mtu.Bahati mbaya mwaka 1988 Phila alikamatwa na askari wa kikaburu akiwa anamnyonyesha mwanae huko msituni. Alipigwa na kuteswa sana akilazimishwa atoe siri za kikundi cha MK lakini aligoma.

Kabla ya kukamatwa Phila alikua askari shupavu ambaye licha ya kuwa na mtoto mchanga hakuacha kupigana.

Alishika bunduki mkono mmoja huku mkono mwingine ukinyonyesha.Baada ya kumshikilia mateka kwa siku kadhaa, serikali ya kikaburu ilitangaza kuwa ilimwachia huru na kwamba eti alikimbilia Tanzania.

Kwahiyo familia ya Phila iliamini binti yao yupo Tanzania, lakini ukweli ni kuwa alikua katika mateso makali sana akipigania uhai wake na mwanae huko Swaziland.

Askari katili wa kikaburu waliamuru mbwa wamuume, kisha wakamvua nguo zote na kumtandika mijeledi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mmoja wa askari aliyemtesa Phila alikuja kukiri na kuomba msamaha mwaka 1994, kwenye Tume ya Ukweli na Maridhiano baada ya utawala wa kikaburu kuangushwa. Askari huyo alisema kuwa walimuweka Phila katika chumba cha mateso akiwa uchi wa mnyama kwa siku 10.

Siku ya 6 ilimbidi Phila ajitengezee nguo ya ndani kwa kutumia mifuko ya plastiki iliyokua imezagaa kwenye chumba hicho.Walimuwekea makaa ya moto na kumlazimisha akanyage, na kuna wakati walimtoboa na misumari sehemu mbalimbali za mwili wake.

Baadae walimtoboa macho, na hivyo kushindwa kuona. Hata hivyo hakutoa siri za kikundi cha MK, licha ya mateso yote hayo.

Baada ya siku 10 za mateso makali walimkata maziwa ili asiweze tena kumnyonyesha mwanae. Kisha wakamfunga mikono na miguu na kumpiga risasi kichwani yeye na mwanae na kuwazika kwenye kaburi la pamoja. Baada ya Afrika Kusini kupata uhuru mwaka 1994, serkali ya ANC (black majority) iliandaa kumbukumbu ya mashujaa wake.

Mmojawapo ni Phila Ndwandwe, mwanamke shupavu ambaye damu yake ilimwagilia ukombozi wa taifa hilo. Rais Nelson Mandela aliagiza mabaki ya mwili wa Phila yafukuliwe huko Swaziland, na kuletwa Afrika Kusini yazikwe kwa heshima.Tarehe 12 mwezi March, mwaka 1997 taifa zima la Afrika kusini liliungana katika ibada ya kuzika upya mabaki ya mwili wa Phila huko Kwa Zulu Natal, kwenye shamba la Elandkop walikozikwa mashujaa wengine.

View attachment 1307181

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kizazi cha zamani kilikuwa kitakatifu,
Vijana wa kizazi hiki,ili kuleta maendeleo kwenye jamii zao,wanataka kwanza wateuliwe kuwa Ma DC,Ma RC,DAS,au wawe wabunge kwanza,
Hapa namkumbuka Ruge,alisaidia sana,na hakuwahi kutamani kuwa yote hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kweli ni shujaa. Ni wachache sana wenye hulka kama huyo binti. Mungu ampe pumziko jema huko aliko
 
FB_IMG_1577696487308.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wake na Shujaa Phila Ndwandwe ( R.I.P), yupo wapi!? ( Nimeishapata jibu tata la swali hili)
===
Nimeguswa sana.
 
Back
Top Bottom