Spika wa Bunge, Dkt. Tulia: PhD za Heshima zina walakini

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
69,344
94,505
Watu wengi wanalipa pesa kupewa Degree za Heshima.
Amesema kuwa Taifa litapotea kwa kuendekeza kukubali Degree za Heshima.
Amesema kuwa wabunge wanasomesha watoto wao, ila wao wanaenda kulipia kupewa Degree,hivyo kuondoa molari kwa wanaosomea
Wengi wao wamepewa Degree na vyuo visivyo tambuliwa.
Kasema inabidi Tanzania iweke muongozo mzuri kuhusu hizo degree
Kasema kuwa hizo Degree hupatikana kwa malipo ya Dollar 2500
Amesema hizo Degree zinauzwa kama Pipi
Kasema Taifa linajivunjia heshima kwenye Elimu na kwa wanaopata Degree kwa kusomea.


==========

Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson ameshauri Taifa kufahamu utaratibu mzuri wa kutumika linapokuja suala la utoaji wa Degree za heshima kwa kuwa kuna wakati zinatolewa kama pipi na kutolewa kwa kila Mtu, jambo ambalo amesema halikubaliki kwa kuwa linalivunja heshima ya Taifa kwenye eneo la elimu na kwenye kuwapa heshima wanaostahili.

Kauli hiyo ya Spika Dr. Tulia Ackson inakuja baada ya Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi kuomba mwongozo kwa Spika kutaka kufahamu Vyuo vinavyotoa udaktari wa heshima ni kwa kiasi gani vinatambulika katika Mmlaka zinazosimamia elimu nchini pia baadhi ya Wabunge wenye muda mfupi Bungeni kutunikiwa Degree za heshima na Wakongwe kutopata hivyo ametaka kujua ni vigezo gani vinatumika.

"Alipopewa udaktari wa heshima, Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia walifanya utafiti wa kina wa kazi alizozifanya sio tu tangu amekuwa Rais, bali tangu alipoanza kufanya kazi. Walikusanya kazi zote na kupima kwa vigezo vilivyowekwa wakaona inafaa wamtunuku"
 
Pamoja na hayo, shule ya Sekondari imefutiwa matokeo ya wanafunzi 66/67 baada ya majibu ya wanafunzi 66 kufanana kwa kila kitu, Mwanafunzi 1 pekee ndo matokeo yalikuwa tofauti hivyo yeye pekee ndo majibu yake yameachiwa...

Kaongelea pia kuna shule ilifungua mitihani kabla ya muda, ikawapa wanafunzi wakafanya, Serikali ina mpango wa kuifunga hiyo shule.

Watumishi 12 waliohusika na udanganyifu wa mitihani wakamatwa, kufukuzwa kazi

Wazazi wa Thaqafa na Twibhok kuoneshwa mitihani ya watoto wao
 
Kwa maelezo hayo ya Spika, Dkt. Mhe Hangaya ni miongoni ya walionunua PhD...............!
 
Hayo wakemeane wao kwa wao CCM maana wao ndiyo wanaongoza Msukuma, Abood, na zingine zenye walakini Jaffo, Biteko
 
Zile halisi kama zingetokeza uhalisi nani angezijali za kununua? Shida imeanzia kupoteza uhalisi wa PhD za darasani kwa watu wenye nazo kuishi kama wasio nazo
 
Kasema kuwa hizo Degree hupatikana kwa malipo ya Dollar 2500
Ina maana hata SSH alilipia hizo $ ?

Msiwaangalie na kuwahukumu hao wabunge wanaonunua u Dr wakati yupo mkuu kapewa u Dr pasipo jasho.

Mmelikoroga wenyewe sharti mlinywe 😁😁
 
Back
Top Bottom