PhD ya Magufuli na wanasiasa wengine zichunguzwe upya!

Huyu bwana tuliambiwa ni msomi sasa najiuliza kisomo chake ni cha kweli am si cha kweli? na je ameelimika au hajaelimika? Au ilikua kukariri tu Inorganic? Msomi lazima awe ni mtu mwenye uwezo wa kung'amua mambo na pia kuchuja mambo katika uzito wake huku akifanya mambo kwa upeo tofauti na yule asiyesoma.

Kwanza kauli za Mh kama ile ya mjini msiponikubali nakubalika Vijijini ni kauli ya aibu kubwa sana kwa mtu aliyeelimika, kwanini? kwasababu, aliyeelimika hufanya jitahada za kila namna kuona ni jinsi gani anaweza akawashawishi hata wale waliomzidi elimu na kuziunga mkono hoja zake, lakini msomi anayetaka kujilinganisha na watu waliokosa elimu japo sisemi waote walioko vijijini hawana elimu la hasha lakini kundi kubwa ni la wale ambao ni wakawaida changamoto za nini kinaendelea duniani wanapishana.

Uwezo wa huyu bwana kung'amua mambo ni mdogo mno ndo maana hataki changamoto na yeyote anayempa changamoto anatamani malaika washuke wamzime mara majo. Kwanini nasema ung'amuaji wake wa mambo ni mdogo sana? siku alipoingia ikulu tu mara moja aliwaambia watanzania kwamba nchi ni tajiri sana hatuhitaji misaada ya wazungu, kwanza wanatusaidia alafu wanatunyanyasa, angekua mtu mwenye uwezo kiupeo asingeshindwa kuelewa kwamba utajiri wa Tanzania unahitaji mikakati ya muda mfupi na na muda mrefu na kuwatumia vizuri wasomi hasa wa mambo ya uchumi ili kurekebisha mambo, alidhani kwa kuongea tu uchumi utabadilika? huu ni upeo duni...Ona sasa anavyolamba miguu wazungu.

Kushindana na watu wanaompa changamoto badala ya kuzitumia kama furusa ya kujiimarisha na kujirekebisha ili awe bora, ni alama nyingine inayonifanya nitilie shaka kisomo cha huyu bwana...Huwezi kukamata kila anayepingana na kile unachokiamini badala ya kuja na hoja za msingi zitakazoionyesha jamii kwamba anayekupinga hana hoja za msingi.

Wenye upeo hupingana kwa hoja lakini wale wengine hupingana kwa ngumi na mtutu wa bunduki, je katika karine hii ya watu waliochangamka namna hii unaweza kuwanyamazisha kwa kuwapiga vitako vy abunduki? au je unadhani kwa kuwapiga vitako vya bunduki utaweza kuwaamisha wwafuasi wao kwamba umewapiga kwasababu hawafai?

Tanzania umasikini umeongozeka na ndo maana unaona watawala wanachekelea misaada ya wale waliowaita mabeberu. Swali la nyongeza kwa bwana mkubwa Je ulivunja mikataba hovyo au haukuvunja?, Je tunadaiwa Canada au hatudaiwi? je Lisu amesema ukweli kuhusu vikao vya siri huko Canada au la? kwama yote ni ndio kwanini Umemkamata?

Siku zote werevu hupingana kwa hoja wale wengine hupingana kwa mtutu wa bunduki.
 
Yawezekana unajua alipo yulee bwana saa eight Oclock. Naona uraiani kumekushinda. Kuna wasio jaribiwa
 
umechoka kuishi nchi hii mkuu,
Kuna mtu aliwai kuuliza maswali haya:
1. Alihitimu mwaka gani PhD yake na nani alimtunuku doctorate yake?

2. Mbona kwenye maktaba ya UDSM hakuna PhD Thesis yake?
3. Kwenye vitabu vya wahitim kuanzia waka 1983 jina lake halimo
4. akiwa UDSM aliwai kutaja title ya thesis yake , watu walikimbia fasta maktaba ya UDSM wakakuta ni thesis ya profesa mwingine.

majibu ya muuliza maswali hayo ilikua ni: Kupotezwa nchini, mpaka leo hajulikani maali alipo and no body cares. UTAWALA WA SASA HIVI UNATUMIA FALSAFA YA MAKIAVELE. UNAJUA NI FALSAFA GANI? BUKUA UTAJUA MWENYEWE.
 
Yanayotokea Libya yanawatia taabu baadhi ya wakuu wa vyuo huko Ulaya. Kwa mfano huu;

The director of the London School of Economics (LSE), Sir Howard Davies has resigned over its links to Libyan leader Col Muammar Gaddafi. ...

He said the decision to accept £300,000 for research from a foundation run by Col Gaddafi's son Saif had "backfired".

The LSE has already announced it is investigating claims that Saif Gaddafi plagiarised his PhD thesis, which was awarded in 2008.

Huko Ujerumani nako kuna haya;
Germany's defence minister Karl-Theodor zu Guttenberg was forced to resign today after admitting plagiarising large chunks of his doctoral thesis

Zu Guttenberg, 39, agreed to drop his doctor title nearly a fortnight ago over allegations he copied chunks of his PhD thesis from newspapers and the Internet.

Hapa kwetu je?
Huyu anayeitwa Dr Magufuli inaeleweka kabisa hakuingia maabara kufanya kazi iliyompa Ph.D.

Hatua gani ichukuliwe kwa profesa aliyesaidia udanaganyifu huu kama ilivyomtokea Sir Howard Davies?

UD kama chuo, kimechukuwa hatua gani?

Yeye mwenyewe Magufuli kama ilivyo kwa Zu Guttenberg amechukuwa hatua gani.

Mwisho hao wengine waliotajwa na Mr Msemakweli ktk kitabu chake wako wapi na Ph.D zao?

Na usisahau, Grace Mugabe naye alipata PhD; nadhani aliyesimamia mpango huo kapata msukosuko sasa.
Ben Saanane alihoji hili, hatujui kwa nini aliamua kupotea.
Chuo Kikuu Dar es Salaam kilikuwa mojawapo wa vyuo bora sana kielimu, lakini sijui kumetokea nini hapo katikati.
Lakini tuseme ukweli, mbona nakala ya maandishi ya utafiti uliopelekea PhD hii ipatikane haionekani kwenye maktaba?
Mwenyewe alisema alifanya ugunduzi wa kitu alichotaka taifa hili linufaike nacho; na kulaumu kwa nini ugunduzi wake huo haujaendelezwa!
 
Duh!
Hapo kwenye red font ndo umenimaliza. Hiyo ni ishara ya ushabiki wa ndoa. Yaonekana una ndoa na Magufuli maana hoja ilikuwa pana ikiwahusisha wanasiasa woote pamoja na vyuo vyao.

Kwako wewe tatizo ni Magufuli hata kama wengine wakiondolewa Ph.D, haikupi taabu.

Sasa unatetea kwa pointi za kizembe! PhD inapatikana kwa kula cafeteria na kupiga stori za kianafunzi? takataka!

Nakupa task ili ushabiki ukutoke. Unamfahamu aliyesimamia hiyo Ph.D? Unafahamu sasa hivi yuko wapi?

Ukilazimisha nitakupa mambo ya aibu ya shule hiyo lakini hapa ni kwa wanajamii. Tunataka utu na akili itumike.

Usimuinue mtu bila sababu maana hiyo CV ya magufuli iko wazi kuliko unavyoificha.
Unafahamu Master aliisoma miaka mingapi?
Kweli jf ya zamani ilikuwa nondo hatutii mguu
 
Jamii Forum ya kipindi hicho.
Waimba taarabu walikua wachache sana.
 
Napenda kufahamu kama huu mjadala ulishafungwa ama ni hofu tu ya wanajamvi kupotea kwa kuhoji PhD ya "Bwana huyu?"

Nakumbuka Ben Saanane (Mungu aendelee kumtunza huko alipo), ilikuwa ndo kabisa anakaribia kulifikia na kulifungua "Pandora Box", lakini kufumba na kufumbua akatekwa na " wasiojulikana" na mpaka leo haijulikani yuko wapi......hai ama marehemu!!

Kwa maoni yangu ni kuwa, siku zote mtu anatambuliwa kwa kauli ikifuatiwa na matendo yake.....

Kufikiri > kauli > matendo

Ndo kusema, kauli na matendo ya Bwana mkubwa huyu yanathibitisha walakini wa uelewa na ufahamu wake uliojengwa kutoka katika malezi yake na elimu yake ya darasani...!!..

And sometimes this can be a genetical disorder created and accelerated by spiritual world.......

This problem can not be solved by a person going to school attaining diplomas or doctorate degrees.......!!

All in all, we have to accept that, lipo tatizo juu ya mtu huyu na linapaswa litatuliwe.....
 
Achaupumbavu wewe? wewe umesoma wapi??? mimi Magufuli nimemshuhudia live pale UDSM na tunakula msosi wote cafeteria kipindi anasoma PhD and i was in the final Year doing Masters...............Acha propaganda za ki.pu.mba.vu unakesha huku kuandika upuumbavu kama huna kazi za kufanya tafuta wanaume wakushikishe ukuta
Hapa uliwadhalilisha sana wana UDSM.
Mwana UDSM hawezi kuwa na akili mbovu kiasi hiki.
 
Habari wana JF,

Ni siku ya jana nilibandika andiko la kutafuta chapisho la PhD holder Rais Magufuli. Sikuwa na maana mbaya kama baadhi walivyodhani na kudai sina haja na chapisho bali kuzungumzia elimu yake. La hasha hiyo haikuwa maana yangu.

Nilikuwa na malengo ambayo mimi naweza kupambanua kama ifuatavyo:

Kwanza kabisa nilitaka kujua kama kweli hawa wasomi wetu wanazitendea haki elimu zao, au ndiyo tunasoma kwa ajili ya "title tu". Pili nilitaka kuonesha ni aina gani ya elimu tuliyonayo hapa nchini hasa sayansi kama nitakavyoeleza kwenye aya zinazofuata hapo chini. Kwa mtazamo wangu mimi naona bado tunasoma historia ya sayansi. Kama research za PhD. zinakuwa ni research ambazo zinaongelea jambo lilishasemwa na wanasayansi wengine, je hii si historia ya sayansi? Kwa nini tuendelee kung'ang'ana na upangaji madaraja na viwango vya elimu na si kuhangaika kubadili mfumo wa elimu ili uwe ni ule utakaompa mwanafunzi ujuzi na maarifa katika tasnia husika?

Thesis ya Mh. ina title ya "The potential of anacardic acid self assembled monolayer from Cashew Nut Shell Liquid as corrosion protection coatings".
Kwa wanakemia hasa wale wa organic chemistry wanajua hizi ni alkenylphenols ambazo zinapatika kwenye maganda ya korosho. Hiyo anacardic acid ndiyo inapatika kwa wingi katika hayo maganda. Hata aliyemsimamia research hiyo Dk. Magufuli ambaye ni Dk. Joseph Buchweishaija aliwahi kufanya kazi ya kuitenganisha yeye na wenzie walifanikiwa ku-isolate kwa asilimia 82% wakitumia sample ya 3g ndani ya dakika 150.

Ni kweli moja wapo ya kazi ambayo hiyo acid inaweza kufanya ni kuzuia kutu kwa kuzuia oxidation. Si lengo langu kufundisha kemia kwenye uzi huu, point yangu ni hii;
Mtwara kuna korosho, bahati nzuri aliyefanya research hii ndiye Rais wa nchi hivi sasa. Imeshindikana je kuitafsiri research hii katika vitendo na badala yake imehifadhiwa kwenye makablasha hapo UDSM? Mimi nilishangaa sana jana watu walivyokuwa wananiambia nikaitafute kwenye library ya UDSM. Hivi kweli hilo ndiyo lengo la kufanya research? Tutaendelea kufanya tafiti za kutunukiwa degree tu na kuachana nazo mpaka lini?

Kwa mtazamo wangu mimi naona mfumo mzima wa elimu yetu unakasoro bila kujali ni level ipi. Unahitaji kushughulikiwa ili kuondoa fikra za nadharia zilizotawala vichwa vyetu. Ufike wakati tutafsiri nadharia kwa vitendo, hapo tutasonga mbele na si kupangua alama za ufaulu na sifa za kwenda Vyuo vikuu.

Tunapong'an'ania kuwa elimu bora ni kupata "A" tu kwenye karatasi ni kujidanganya kuwa tuna maarifa kumbe ni maarifa ya nadharia tuliyoyaacha kwenye karatasi. Ni nani asiyejua kuwa hizi "A" zinapatikana kwa kukesha tukisolve lundo la mitihani iliyopita? Hata huko vyuo vikuu watu wanahangaika kupata mitihani iliyopita wakibahatisha basi ni "As" na GPA za 4.5 hewa? Katika chuo kikuu kimoja hapa nchini vijana wanasoma Bsc. Physics mwaka wa kwanza hadi wa pili practical kubwa wanayofanya kila semister ni ya Cathode Ray Oscilloscope kustudy frequency za source za umeme kama DC generator, halafu hawa ndiyo watakuwa technologists kweli?

Natoa Rai kwa serikali hii kama kweli ina nia ya dhati katika kuboresha elimu isihangaike tu na madaraja na viwango vya ufaulu, bali twende kwenye elimu ya kutenda zaidi si ufaulu wa karatasi tu. Tunahitaji falsafa mpya ya elimu. Inawezekana je mtu anasoma mechanical engineering miaka minne lakini aingie workshop mwaka mmoja tu? Ni hayo tu, sikuwa na maana ya kukosoa elimu ya bwana mkubwa bali falsafa ya elimu tuliyong'ang'ania ya ufaulu wa makaratasi.
Hii hoja yako ilikua inahitaji uzi wake kabisa.
Elimu ya JMT ina shida kubwa sana.
 
Back
Top Bottom